Rais wa Zanzibar na Mwenyekiti wa Baraza la Mapinduzi Dk Ali Mohamed Shein,akizungumza na Waandishi wa Habari wa Bara na visiwani,kuhusu mafanikio ya mwaka mmoja tokea kushika nafasi ya Urais wa Zanzibar,Ikulu Mjini Zanzibar.
Waandishi wa Habari wa vyombo mbali mbali Bara na Visiwani wakimskiliza Rais wa Zanzibar na Mwenyekiti wa Baraza la Mapinduzi Dk Ali Mohamed Shein,(hayupo pichani) alipozungumza na Waandishi wa Habari wa Bara na visiwani,kuhusu mafanikio ya mwaka mmoja tokea kushika nafsi ya Urais wa Zanzibar,Ikulu Mjini Zanzibar.Picha na Ramadhan Othman,IKULU

Serikali ya mapinduzi Zanzibar imesema itamchukulia hatua mtendaji yeyote wa serikali ambaye atavunja sheria na kanuni zilizowekwa na serikali

Kauli hiyo imetolewa leo na Rais wa Zanzibar dk Ali Mohammed Shein wakati akizungumza na Waandishi wa habari kwa mara ya kwanza katika utaratibu aliojiwekea wa kukutana na waandishi kila baada ya miezi mitatu huko Ikulu Mjini Zanzibar.

Amesema kila kiongozi anaelewa vilivyo juu ya sheria na taratibu ziliopo katika nyendo zake zote akiwa kazini au pengine popote hivyo atakayevunja sheria atawajibika.

Hali hiyo imekuja baada ya kupata taarifa kutoka kwa waandishi wa habari kwamba wapo baadhi ya watendaji wakuu wa serikali ambao hutumia gari za serikali katika muda usio wa kazi na wengine huzitumia kwa kazi za kibinafsi.

Akizungumzia suala la maendeleo yaliopatikana katika kipindi cha mwaka mmoja tangu kuwa rais dk shein amesema serikali ya mapinduzi Zanzibar chini ya mfumo wa umoja wa kitaifa umeweza kupiga hatua kubwa katika nyanja mbali mbali ikiwemo uchumi afya, elimu, kilimo,huduma za jamii na utalii.

Amesema hivi sasa sekta ya utalii inaipatia Zanzibar kiasi cha asilimia 70 ya fedha za kigeni na kukamata nafasi ya kwanza katika kuipatia Zanzibar fedha za kigeni badala ya zao la karafuu hapo nyuma.

Kuhusu kilimo Dk Shein amesema serikali imetoa kipa umbele katika kilimo ili kuiwezesha Zanzibar kwa kiwango fulani kujitegemea kwa chakula ili kuweza kukabiliana na tatizo la uhaba wa chakula unaoikabili dunia hivi sasa.

Amesema nchi kamaThailand na nchi nyengine ambazo zinazalisha mpunga kwa wingi hivi sasa zinakabiliwa namatatizo mbali mbali ikiwemo mafuriko mambo ambayo yataathiri uzalishaji wa zao hilo.

Hivyo amesema serikali itajikita katika kuwapatia wakulima pembejeo za kilimo kwa wakati na kuongeza matrekta na mbegu za kisasa ili kuweza kuzalisha zaidiili angalau kufikia asilimia hamsini ya mahitaji yote ya uzalishaji wa mpunga ambapo zaznibar hivi sasa inazalisha tani 16,000 tu wakati mahitaji ni tani 80,000.

Aidha amesema kuwa serikali ya china na serikali ya mapinduzi Zanzibar imekubaliana katika kusaidia Zanzibar katika Nyanja mbali mbali zikiwemo upanuzi wa jengo jipya la uwanja wa ndege wa kimataifa wa Abeid Amani Karume Zanzibar. 

Pia kuiwekea vifaa hospitali ya abdalla mzee ilioko Pemba pamoja na kuweka vifaa mbali mbali vya kisasa katika chumba cha wagonjwa mahatuti kwenye hospitali kuu ya Mnazi Mmoja Zanzibar

Michuzi Blog

Tanzanian blog operating since 2005, covering International news and Local News, including Politics, Fashion, Social Scenes, Interviews, Movies, Events, personalities and anything positive happening worldwide. Written in Swahili and English targeting both Swahili and English readers.

Toa Maoni Yako:

Kuna Maoni 1 mpaka sasa

  1. Waandish wa habari wengi wazuri na wenye afya tu Tanzania lakini walishindwa kuwajibika vilivyo kutoa habari za maafa ya meli huko visiwani kwa wakati muafaka na kwa kina. Tafadhalini wajibikeni kama waandishi wa habari wa nchi nyingine. mnashindwa na majirani zenu Wakenya!!.

    ReplyDelete

Hii ni Blog ya Watanzania popote walipo duniani kwa ajili ya kuhabarisha, kutoa/kupokea taarifa na kuelimisha mambo yote yaliyo chanya kwa Taifa letu. Tafadhali sana unapotoa maoni usichafue hali ya hewa wala usijeruhi hisia za mtu/watu. Kuwa mstaarabu...