Kaka michizi na wadau habari zenu? kwanza napenda kukupongeza kwa kazi nzuri unayoifanya juu ya jamii yetu. Naomba uniwekee hoja yangu Uncle.
o nina hoja ya haja hapa kidogo. Hivi nataka kujua huu uhuru unayosheherekewa ni wa Tanzania au ni wa Tanganyika? kwasababu mimi ninavyojua neno au jina Tanzania limekuja pale Tanganyika tulipoungana na Zanzibar mwaka 1964 kama sikosei, na ninavyojua Tanganyika imepata uhuru 1961, na Zanzibar imepata uhuru 1963/1964 kama sikosei.
Kwa hiyo sidhani kama Tanzania ina uhuru kutoka tulipoungana pande zote mbili tulikuwa tushapata uhuru wetu, tuliitangulia Tanganyika na baadae Zanzibar wakafuatia.
Sasa je hizi sherehe zinazosheherekewa za uhuru ni uhuru wa Tanzania au kwa Tanganyika? na kama ni wa Tanzania kivipi? wakati unagombaniwa uhuru kwa nchi zote mbili hakukuwa na Tanzania?
Mdau Mwenzenu
Fesali Jadi
ndugu yangu mwandishi hiyo mada yako inanipa hedache kilasiku.
ReplyDeleteMaana tangu sherehe za uhuru zilipoanza sijamsikia hata kiongozi mmoja akisema km tunasherehekea uhuru wa tanganyika wote wanasema sherehe za tanzania bara, kisha ukiangalia wenzetu wazanzibar wanasherehekea uhuru wa zanzibar.
Nionavyo viongozi wetu wa tanganyika wameipoteza na wanaipoteza tanganyika lakini viongozi wa zanzibar wanailinda zanzibar yao.
viongozi wetu watambue itakuja kutucost baadae hali hii ya kuipublish tanzania instead of tanganyika.
ReplyDeleteCoz zanzibar wana bunge lao,mahakama yao, wimbo wao wa taifa, bendera, rais, mawaziri nk.
But tanganyika we dont hav any thing. Tutambue life z long journey, hakuna aliyejua kama siku moja sudan kusini na kaskazini watatengana, au ireland km itajitoa ktk muungano wa united kingdom.
Swali la kujiuliza, mungu asijaalie,
Zanzibar na tanzania bara zikitengana, tanganyika itaanza wapi?
Ni uhuru wa Tanzania bara. Hao wazanzibar kwanza huwa hawaitambui Tanzania kwa ujumla, kwani ukienda unguja au Pemba kama unatokea bara watakuuliza "weye watokea Tanzania". Hilo ni swali la kawaida kabisa kwa wenzetu wa visiwani. hivyo hata muungano ukifa kesho asubuhi wao haitawaathirika kwani fika wao hawapo Tz wapo Pemba au Unguja kama ukipenda Zanzibar.
ReplyDeleteTatizo kubwa watu mnaojaribu kuja na hoja hizi za ajabu! ajabu,mnaelewa wazi ni miaka 50 ya uhuru wa Tanzania bara(ex-Tanganyika) ndio unaosherekwa, Uhuru wa Unguja hakutambulika na wanzibari walio wengi ndio maana pakatokea mapinduzi ya mwaka 1964,na jina la Tanganyika alitumiki tena kila moja anaitaja Tanzania itakua ni bara na Visiwani au Bara pia,na Unapotaja Zanzibar ni kiungo cha Tanzania,Tanganyika kiserekali haipo bali Tanzania bara ndilo jina Rasmi,sasa pasiwepo hoja za ajabu hapa kwa kujitafutia umaarufu.Tafuteni kazi za kufanya
ReplyDeletehii ni hatari tena sana ila mimi ninavyo ona watu wa tanganyika hawaitaki tanganyika ya lakini wazanzibar kila siku wanapiga kelele na zanzibar yao
ReplyDeleteIt does'nt matter...nchi zikishaungana kila kitu ni kimoja,,kwani wewe huwezi sheherekea birthday ya mke wako sababu tarehe zenu za kuzaliwa ni tofauti,,, mfano mzuri...... AMERICA origanal states zilizopata uhuru 4th July 1776 from British colony .. zilikuwa 13leo hii USA ina states zaidi ya 50 hizo zote zilikuwa ni nchi zinazojitegemea... na kila state ina sheria zake..lakini wakisheherekea uhuru ni Taifa moja..
ReplyDeleteAcheni Uzanzibari wenu na Utanganyika hausaidii chochote..,
Tanzania Bara na Tanzania Visiwani...
ReplyDeleteafadhali mumegundua hili wenyewe watanganyika,sisi hatuutambue huu munaouita uhuru wa tanzania bara/Tanzania....sisi wa zanzibar tunasema kwa pamoja hivi sasa tunataka zanzibar yetu na ipo siku tutaipata kuanzia cku hizi hakuna mzanzibar anejitambulisha km yeye ni Mtanzania bali ni Mzanzibari.................ahahahhaha
ReplyDeleteHiki kizungumkuti kinachanganya kwelikweli.
ReplyDeleteMiaka 50 ya uhuru, means Tanganyika ilipopata uhuru 09.12.1961, lakini leo Tanganyika haipo.......
Sioni mantiki ya sherehe zenyewe. Ni ubabaishaji mtupu.
Mimi navyoona muungano tulio nao si tofauti sana na kule ulaya wa United Kingdom(UK.)
ReplyDeleteLeo hii bado ENGLAND imebaki kama England, SCOTLAND kama Scotland, WAILES kama Wailes, na IRELAND kama Ireland.
Nashangaa kwanini sisi leo tunaona aibu au kama dhambi kuita TANNGANYIKA.
Tanganyika bado ipo na itakuwepo tuwe wawazi kutumia jina hilo.
Na pia jina TANGANYIKA lilifahamika zaidi ya Tanzania.
nyie watoto mliozaliwa leo hamjui watu walikotoka. Wengine tumekuja ugenini tukapokelewa alhamdulillahi mahali popote unapopata riziki ndio hapo hapo, mambo ya uzanzibari na utanganyika uko futi 6 chini ya ardhi. Bora niwe mdanganyika kuliko huo uzanzibari wenu mnaogombea, kwani wandengereko na wanyamwezi walioko huko zanzibar leo wanaikataa nchi yao ya asli. Msituletee ujinga sisi.
ReplyDeleteHapa naona watu wengi hawajasoma elimu ya uraia. Mnapodai kuwa serikali ya Tanzania bara haipo, siyo kweli. Kuna serikali ya Tanzania Bara, Serikali ya Tanzania Visiwani, na Serikali ya Jamhuri ya Muungano wa Tanzania. Hata ukichunguza kwa umakini, kuna wizara zilizo ndani ya Muungano na zisizo ndani ya Muungano. Kinachowapoteza walio wengi ni kuwepo kwa Rais wa Zanzibar, na huku Tanzania bara ikiwa haina rais. Hapo kuna tatizo. Maana Tanzania Bara ipo lakini ni kama imefichika kiaina. Muhimu ni Katiba iseme pia kuwa kutakuwepo na rais wa Tanzania Bara. Ili serikali zote tatu zionekana mbele ya macho ya hata ya vipofu.
ReplyDeleteWEWE UNAYESEMA HOJA HIZI ZA AJABU WEWE NDO WA AJABU,JIBU HOJA TANGANYIKA ILIUNGANA NA ZANZIBAR TUKAPATA SERIKALI MOJA YA TANZANIA.HII SERIKALI YA MAPINDUZI ZANZIBAR INATOKEA WAPI?
ReplyDeleteSIKU ZANZIBAR IKIJITENGA(LAZIMA ITATOKEA TU KAMA SI LEO BASI KESHO)HUKU BARA TUTAJIITAJE?
WATU WAMESOMA SIO NGUMBARU KAMA MLIVYOZOEA ZAMANI AU TANZANIA NDO ILIYOUNGANA NA ZANZIBAR????????
Hoja ni ya haja mpaka imewachanganya baadhi ya watu na kuandika UHURU WA UNGUJA.fact ni uhuru wa zanzibar uliyopatikana December 1963 na baadae mapinduzi kupora serikali ya kidemokrasi January 1964 ikisaidiwa na hayati Nyerere Rais wa Tangayika wakati huo.
ReplyDeleteHii ni tosha kuonesha uhuru huu unaosheherekewa ni wa Tanganyika juu ya jina Tanzania plus bara.
Kisa cha wazanzibari wengine kutotambua uhuru wa 1963 sio kibali cha Tanagika au Tanzania plus bara kusheherekea uhuru wake kwa jina Tanzani kwani ni kupoteza muelekeo na historia ya nchi hii.
Jibu: Ni uhuru wa Tanganyika kwa gamba la Tanzania linalokwaruza wazanzibari.
EE mdau hapo juu!naona hata mkisafiri pass zenu ni chapa 'Zanzibar' wala sio 'Tanzania'...EEe na hali ilivyongumu mtaweza kweli kusurvive wenyewe kwa wenyewe?
ReplyDelete