MAREHEMU MZEE SABINUS P. KWEKA

LEO UMETIMIZA MIAKA SABA TOKA ULIPOTUAGA UNAKWENDA KUMWONA MGONJWA ARUSHA HALAFU UKARUDI UKIWA KWENYE JENEZA. HATUNA CHA KUSEMA ILA TUMEBAKI KUMSHUKURU MUNGU TUU KWANI AMEPENDEZEWA NAWE ZAIDI YETU.

BABA, ULIPIGANA VITA VILIVYO VIKUU NA ULIVISHINDA.TUNAKUKUMBUKA KWA MENGI LAKINI KUBWA KULIKO YOTE NI JINSI ULIVYOPIGANIA ELIMU YETU AMBAYO IMETUFIKISHA HAPA TULIPO.PIA ULIAMINI KUWA BILA SALA NA UPENDO WA MUNGU, HATUWEZI KUFIKA POPOTE. TUPO KAMA ULIVYOTUACHA. TUNAENDELEA KUKUENZI KWA HAYO INGAWAJE BADO MAJARIBU NI MENGI.

UNAKUMBUKWA SANA NA MKEO MPENZI URSULA, WANAO JANE, FESTO,EUGENIA, ELIZABETH,CECILIA NA THADEI, DADAKO MPENDWA SR. DEVOTHA KWEKA, WAJUKUU, WAKWE ZAKO, WANA UKOO WOTE WA KWEKA, WANARUMU, NDUGU, JAMAA NA MARAFIKI.

RAHA YA MILELE UMPE EEE BWANA, NA MWANGA WA MILELE UMWANGAZIE, APUMZIKE KWA AMANI, 

-AMINA!

Michuzi Blog

Tanzanian blog operating since 2005, covering International news and Local News, including Politics, Fashion, Social Scenes, Interviews, Movies, Events, personalities and anything positive happening worldwide. Written in Swahili and English targeting both Swahili and English readers.

Toa Maoni Yako:

0 comments so far,add yours

Hii ni Blog ya Watanzania popote walipo duniani kwa ajili ya kuhabarisha, kutoa/kupokea taarifa na kuelimisha mambo yote yaliyo chanya kwa Taifa letu. Tafadhali sana unapotoa maoni usichafue hali ya hewa wala usijeruhi hisia za mtu/watu. Kuwa mstaarabu...