KUNDI la viboko katika mto Sitalike uliopo katika Hifadhi ya Taifa ya Katavi katika wilaya ya Mpanda mkoani Rukwa wakiburudika mtoni baada ya msimu wa mvua kuanza wiki hii, hali ilikuwa mbaya kufuatia mto huo kukauka maji wiki chache zilizopita kama walivyokutwa na mpiga picha hivi karibuni (Picha na Peti Siyame).
Home
Unlabelled
kundi la viboko wakiburudika ndani ya mto sitalike baada ya msimu wa mvua kuanza.
Subscribe to:
Post Comments (Atom)
Hee hee asante sana Peti..umenikumbusha Mpanda..Mto Sitalike..unavuka daraja na kuna kona kali...kuna 'barrier" ya askari pori.si ndiyo hapo??.Nilikosa uhondo sikuiona hii midude.
ReplyDeleteKuna viboko kama hawa tena mitaa ya Seronera kwenye kidaraja fulani hivi.
David V
wow that is so cool!!
ReplyDeleteWoow!!hizo ndizo rasilimali za kutupatia mapato kwa kutembelewa na watalii badala ya kutegemea misaada ya masharti.
ReplyDeleteCJM
Wawe wakivunwa japo kidogo na wananchi kupata kitoweo badala ya kuachwa wafe kwa ukame.
ReplyDeleteIli kusaidia kuwahifadhi Tanapa waangalie uwezekano wa kuchimba lambo la uhakika Katavi la kusaidia kutunza maji wakati wa kiangazi. South Africa hufanya hivyo.
Nadhani boko ni wanyama walio katika hatari ya kutoweka duniani. Kuwe na mpango mkakati wa kuwatunza wawepo miaka 500 ijayo wataleta pesa nyingi kwa vizazi vijavyo.
Halafu tuambiwe eti mabwawa na mito imekauka ndio maana umeme umekuwa wa mgao.
ReplyDeleteSASA HIVI TANESCO WATATANGAZA
Ingekuwa raha iliyoje viongozi wa chadema tukawatumbukiza humo wafanye fujo, si wanapenda fujo?
ReplyDeleteWe anonym 17,01;55pm 2011, uache roho mbaya utatumbukizwa wewe ukawafanyie fujo peke yako. Bora viongozi wa chadema wakifanya fujo hawajifichi ila wewe unajificha maana wee muoga.
ReplyDeleteTuwe makini na rasilimali zetu kama hawa Viboko mtoni wamekaa mkao wa hasara.....unaweza kukuta siku moja wamepandishwa ndege wanatoroshwa nje!
ReplyDelete