KUNDI la  viboko   katika  mto  Sitalike  uliopo  katika  Hifadhi ya  Taifa  ya  Katavi  katika   wilaya  ya Mpanda mkoani  Rukwa  wakiburudika   mtoni  baada  ya  msimu  wa   mvua  kuanza  wiki  hii,  hali ilikuwa  mbaya   kufuatia  mto  huo  kukauka  maji  wiki  chache  zilizopita  kama  walivyokutwa  na  mpiga  picha  hivi karibuni (Picha  na Peti Siyame).

Michuzi Blog

Tanzanian blog operating since 2005, covering International news and Local News, including Politics, Fashion, Social Scenes, Interviews, Movies, Events, personalities and anything positive happening worldwide. Written in Swahili and English targeting both Swahili and English readers.

Toa Maoni Yako:

Kuna Maoni 8 mpaka sasa

  1. Hee hee asante sana Peti..umenikumbusha Mpanda..Mto Sitalike..unavuka daraja na kuna kona kali...kuna 'barrier" ya askari pori.si ndiyo hapo??.Nilikosa uhondo sikuiona hii midude.

    Kuna viboko kama hawa tena mitaa ya Seronera kwenye kidaraja fulani hivi.

    David V

    ReplyDelete
  2. wow that is so cool!!

    ReplyDelete
  3. Woow!!hizo ndizo rasilimali za kutupatia mapato kwa kutembelewa na watalii badala ya kutegemea misaada ya masharti.

    CJM

    ReplyDelete
  4. Wawe wakivunwa japo kidogo na wananchi kupata kitoweo badala ya kuachwa wafe kwa ukame.
    Ili kusaidia kuwahifadhi Tanapa waangalie uwezekano wa kuchimba lambo la uhakika Katavi la kusaidia kutunza maji wakati wa kiangazi. South Africa hufanya hivyo.
    Nadhani boko ni wanyama walio katika hatari ya kutoweka duniani. Kuwe na mpango mkakati wa kuwatunza wawepo miaka 500 ijayo wataleta pesa nyingi kwa vizazi vijavyo.

    ReplyDelete
  5. Halafu tuambiwe eti mabwawa na mito imekauka ndio maana umeme umekuwa wa mgao.

    SASA HIVI TANESCO WATATANGAZA

    ReplyDelete
  6. Ingekuwa raha iliyoje viongozi wa chadema tukawatumbukiza humo wafanye fujo, si wanapenda fujo?

    ReplyDelete
  7. We anonym 17,01;55pm 2011, uache roho mbaya utatumbukizwa wewe ukawafanyie fujo peke yako. Bora viongozi wa chadema wakifanya fujo hawajifichi ila wewe unajificha maana wee muoga.

    ReplyDelete
  8. Tuwe makini na rasilimali zetu kama hawa Viboko mtoni wamekaa mkao wa hasara.....unaweza kukuta siku moja wamepandishwa ndege wanatoroshwa nje!

    ReplyDelete

Hii ni Blog ya Watanzania popote walipo duniani kwa ajili ya kuhabarisha, kutoa/kupokea taarifa na kuelimisha mambo yote yaliyo chanya kwa Taifa letu. Tafadhali sana unapotoa maoni usichafue hali ya hewa wala usijeruhi hisia za mtu/watu. Kuwa mstaarabu...