Waungwana,kwa heshima na taadhima naleta hii mada inayohusiana na mambo ya utaalamu kuhusu tasnia ya muziki ambayo,ni kazi kama zilivyo kazi zingine zote.Nia hapa ni kumega kidogo nilichonacho/ninachokijua katika taaluma hii ili,wenye nia ya kujifunza moja au mawili,waweze kufanya hivyo.

MUZIKI NI NINI?!.
Hili ndilo swali la kwanza la kujiuliza kwa yeyote anayetaka kuigusa nyanja hii japo kwa kusoma kama historia na si kuingia katika mazoezi ya vitendo na hatimaye kuonesha kipaji chake mbele ya kadamnasi.

Hapa kila mtu anaweza kulijibu swali hili kulingana na utashi wake na uelewa alionao katika fani hii, kutokana na aliyoyaona na kuyasikia kuhusu muziki.Ikumbukwe kwamba,"sikio" ni kiungo muhimu katika mwili kinachoupokea mdundo wa ngoma kwa namna ya kipekee, na kumfanya mlengwa aanze kutikisa viungo vya mwili wake wakati mwingine pasipo mwenyewe kujijua.

Lakini kwangu mimi, kwa kutumia neno moja, nitasema.... muziki ni "SOUND"(MLIO). SOUND ndiyo inayotengeneza muziki,endapo sound hizo zitapangwa katika ufundi na umaridadi unaovutia masikioni mwa m/(wa)-lengwa.SOUND hiyo hiyo,inaweza kuwa mbaya au "kelele" masikioni endapo mtumiaji hakufanya kazi ya ziada kuzioanisha sauti ili ziwe burudani masikioni.

SOUND inaweza kutumika pia kama kiashirio cha tukio linalotegemea kutokea au
lililokwisha tokea.Mfano ni kama kengele zinazoashiria tukio la Ibada makanisani, matumizi ya ngoma vijijini tangu karne nyingi zilizopita,kama njia ya mawasiliano katika matukio muhimu yanayowajumuisha wanakijiji wote.SOUND imekuwa ikitumika katika mataifa mbalimbali tangu enzi na enzi kama kiashirio.

Michuzi Blog

Tanzanian blog operating since 2005, covering International news and Local News, including Politics, Fashion, Social Scenes, Interviews, Movies, Events, personalities and anything positive happening worldwide. Written in Swahili and English targeting both Swahili and English readers.

Toa Maoni Yako:

Kuna Maoni 1 mpaka sasa

  1. nimeshindwa kuchangia. Sijaelewa maana ya neno SOUND. Tafadhari nifahamishe.

    ReplyDelete

Hii ni Blog ya Watanzania popote walipo duniani kwa ajili ya kuhabarisha, kutoa/kupokea taarifa na kuelimisha mambo yote yaliyo chanya kwa Taifa letu. Tafadhali sana unapotoa maoni usichafue hali ya hewa wala usijeruhi hisia za mtu/watu. Kuwa mstaarabu...