Mabasi ya abiria yafanyayo safari zake kati ya Dar - Mbeya yakiyapita magari mengine huku yakiwa yameongozana katika kona za milima ya Iyovi,huku wakiwa hawana wasiwasi wowote.hivi kwa mfano,wakati wanaenda namna hii halafu mbele kunatokea gari nyingine,ni nini kitatokea hapo??
Hili nalo mambo yalikuwa ni hivyo hivyo.sijui kifanyike kitu gani ili kuhakikisha uzembe kama huu unatokomezwa kabisa?
cha msingi peleka hizo picha police zikiwa kama ushahidi na hakikisha vyombo vya habari zinapata picha hizi,naamini GP Said mwema atachukua hatua kwa hayo mabasi.Jambo la pili sione waandishi wa habari ambao wanajiita wapiganaji wakipigania wananchi wa tanzania,wao pia wanachangia tanzania kuwa na ajali hizi
ReplyDeleteKwanza alama za barabarani kama zilivyochorwa hapo chini (solid white lines at the middle of the road) zinaonesha kabisa kwamba HAIRUHUSIWI au kwa lugha nyingine ya kidemokrasia (msiseme jamaa dikteta) SI SALAMA kuipita gari iliyombele yako. Sababu ni simple tu...huna full control kwa sababu huoni wala hujui utakachokutana nacho baada ya kona. Kwa maana hiyo gari mbili zinazoelekea upande mmoja zimetumia full length ya barabara bila kujali watumiaji wengine wa barabara na hii ni kinyume cha sheria. Lakini hii ni bongo. Serikali ina ushahidi hapa wana uwezo wa kuwafungulia kesi madereva wa mabasi haya ili kutoa onyo but these guys will get away with it. How sad
ReplyDeleteHao wanao overtake hapo wanavunja sheria. Alama za mistari kamili miwili inaonyesha kuwa hapo hairuhusiwi kupita gari lingine. Hata hivyo dereva wa gari la mafuta ana overtake pamoja na wa bus pia. Ikitokea ajali hapo maafa yake ni makubwa kwa vile katika mabasi hayo yote kuna idadi kubwa ya abiria. Madereva, pamoja na kujua sheria za barabarani, inabidi vilevile tuwe na nidhamu.
ReplyDeleteNadhani ni vizuri kama serikali itaweza kuweka masomo ya kujikumbusha kila baada ya muda fulani kwa kila dereva hususan madereva wa mabasi ambao wanapakia abiria.Kwasababu nchi yetu madereva wengi wamepata leseni kwa mlango wa nyuma kuliko waliofanya mtihani wa udereva kiuhalali.Hii ni hatari sana na watu wengi watateketea na ajali za kipumbafu.Wanao miliki mabasi au magari makubwa wanatakiwa wasajiliwe na walipe malipo madogo kwa serikali ili wapewe masomo kila mwaka na kuwakumbusha madereva sheria za barabara pamoja na kuepukana mwendo wa kasi ili kuepusha hizo ajali.Ikiwezekana hata mitihani midogo wapewe ili kuwapima ujuzi wao kama upo salama kwa manufaa ya wananchi.
ReplyDeleteDawa ni polisi kuwafuatilia, anapo vunja sheria namna hii, apate adhabu kubwa dereva ikiwemo ya kufungiwa leseni, na alipe pesa nyingi kwamfano alipe tsh. millioni kumi kwa kosa hili hana jela miaka kumi.
ReplyDeleteHuo ni uzembe wa hali ya juu, na wa kulaumiwa ni serikali. Polisi wapo hawasimamii sheria inavyotakiwa. Sheria ya matumizi ya barabara ulimwenguni inasema hutakiwi kuvuka msitari mweupe ulionyooka,kwa hiyo picha hao wote wameshavunja sheria hata kabla ya ajali kutokea.
ReplyDeleteamakweli ajali Tanzania hazitakwisha,hapo nadhani huyo dereva haelewi kabisa matumizi ya hiyo mistari miwili katikati ya barabara,kwa ninavyo fahamu ukiona mistari miwili kama hiyo(solid lines)hauruhusiwi kupita gari lingine .inawezekana mbele kuna mlima,kona au mteremko unaosababisha dereva asione gari linalokuja upande wa pili
ReplyDeletePolisi hawafanyi lolote hapo wakiwakamata wanapewa kitu kidogo wanawaachia huru! Ila ikitokea ajali ndo watafanya uchunguzi na wakipata matokeo ya uchunguzi wanaweka kapuni matokeo hayo life goes on! Hii ndo Tanzania yetu usalama wa raia ni midomoni tu unapokuja kwenye vitendo ni sifuri!
ReplyDeleteHawa madereva formula1 wanaiweza duhhh! Wana roho za plastic. Mdau toka bujumbura
ReplyDeleteMdau wa hapo juu siyo kwamba madereva hawaelewi kuhusu hiyo mistari meupe iliyonyooka, lakini hiyo ni dharau tu.
ReplyDeleteWenye mabasi jamani wajulisheni madereva wenu juu ya nidhamu ya uendeshaji ili tupunguze ajali.
Ajali nyengine zina kinga.
nadhani kama walivyochangia baadhi ya wadau hapo juu swala ni kupitisha sheria itakayowezesha kuwafikisha madereva kwenye sehemu husika kwa kitendo cha kubainika kuhatarisha maisha ya raia wema kupitia picha kama hivyo.
ReplyDeleteHakuna ajabu kuona vitu kama hivyo huko nyumbani. Hivi karibuni nilikuwa huko kwa likizo gari yangu ikagongwa na daladala makusudi.Walipokuja traffic police katika mazungumzo yaliyotokea askari huyo alisema driver anaweza ku-overtake hata magari matano no matter aina gani ya magari. Je umbali wa magari matato yanayotembea driver anaweza kuepuka kinachotokea huko mbele yake??????,
ReplyDeletemimi nafikiri dividers zingesaidia sana kupunguza ajali kwa sababu madreva wanaondesha namna hii ni kwamba hawajali maisha ya watu na kwa vile hatuwezi kuweka polisi kila corner ni bora kujikinga kabla ya maafa.
ReplyDeletesiyo nini kifanyike,hapo ni faini tu 700,000,tuone kama atarudia tena.Tumechoka na ajali,tuwe wakali kama mbogo,kwenye uhai wa mtu.
ReplyDeletemimi natakakuona hawa walo vunja sheria ushahidi upo huo wachukuliwe hatua ikiwa kifungo miezisita hivyo itakua fundisho kwa sote hamna cha mwana sheria kusimamia kesi hizo kutokana na maafa mengi taifa imeisha yapata
ReplyDeleteImefika mahali inabidi sisi kama abiria tukiona dereva anafanya upuuzi kama huo ambao unahatarisha maisha yetu tusikae kimya,papo hapo dereva tumpe onyo.
ReplyDeleteCHAPA VIBOKO HAO MADEREVA NONSENSE
ReplyDeletemsilaumu mabasi kweli ni hatari na makosa ila chamsingi kungekuwa na utaratibu kama ulaya mfano BASI LA SAA 7AM LINAFIKA SAA 2PM MKOA KADHAA BASI LA SA 8PM LINAFIKA SAA KADHAA HAPO KUNGEKUA NAUSHINDANI MZURI WA KIBIASHARA na ajali zingeepukwa asilimia 78% kutokana bila utaratibu huo watu watashindana kila mtu atataka kufika mwanzo ili apate sifa,haya ni mawazo yangu hata kama abiria watalazimisha usafiri wa kutosha - pia kuwepo na speed limit na pia speed camera njiani na adhabu either kunyang'anywa leseni kwa mwaka na kadhaa tena kwa dereva na company,
ReplyDeletemimi nadhani hapa dawa ni kuwaambia madereva wachukue tena test au mitihani ya udereva na alama zote za barabari ziwekwe. Halafu watie sahihi kwamba nikivunja sheria ya alama hizi za barabarani nitakaa jela miaka mitano kwanza. Viboko kumi wakati naingia na viboko kumi wakati natoka jela .
ReplyDeletemkulima
Hii Inaonyesha Hata Abiria Hawayajali Maisha Yao!! Hakuna Hata Mtu Mmoja aliyekuwa na Busara Na Kupiga kwenye Namba zinazogawiwa Na Polisi? Eeh Mungu Liombee Taifa Hili!!!
ReplyDeleteLakini hata abiria inakuwaje waruhusu dreva afanye hivyo bila kumpigia kelele? Abiria pia wanachangia hali hii kwa kuacha kutoa taarifa polisi.
ReplyDeleteMaeneo yote yanayohitaji kuendesha kwa tahadhari kama haya yawekewe Police check posts, hata kama hizo cp zitawekwa katika interval ya km 5 ili iwe rahisi kwa polisi kufanya Patrol.Serikali ifanye vituo hivi permanent, viwekewe cameras na vifaa ambavyo vina uwezo wa kufuatilia magari yanayopita sehemu hizo. Pili, akikamatwa mtu akiendesha vibaya apelekwe mahakamani, na ahukumiwe kifungo cha kufaa.(Miaka si chini ya 10) au faini ya kufaa(si chini ya 10M. watakoma.
ReplyDeletehao jamaa uendeshaji wao sio kabisa,ila tatizo jeshi la polisi nalo linafanya kazi manually zaidi inabidi wabadili namna ya kukabiliana na hawa wahalifu wa barabarani,hawa jamaa wakifika hizo kona za iyovi ni kama wapo vitani,wanaendesha magari bila kujali roho za watu waliowachua kwenye mabasi
ReplyDeleteHuo ni uzembe wa mwaka overtaking ktk kona ..ebo!!!
ReplyDeleteTatizo madereva kwa Tanzania sheria sio kali ...issue kama hii akipata ajali analazwa ndani skiu 2 tu halafu anatozwa kiduchu kama faini Tsh. 20,000/=
Ngoja ajali itokee ndio utajua na kusikia vitendo vyetu; Hivi abiria waliokuwemo kwenye mabasi hayo walikua wamelala? Ile mikogo ya kwenye matangazo kwamba piga simu endapo dereva ataendesha vibaya ilishindwa kutumika? Mpaka dakika hii nini kimefanyika dhidi ya wazembe kama hawa wakati ushahidi wa wazi upo? Ndugu zangu kelele tutapiga nyingi lakini kama nia hasa ya kutaka kuondoa ajali za maramara haipo matokeo ya ajali yatakuwa sehemu ya maisha yetu.
ReplyDeleteTusubiri tuone kama kuna polisi atathubutu kufuatilia haya mabasi, hakuna mwenye ubavu huo wote either wamewekwa mfukoni na matajiri ama wao watapewa kitu kidogo na mambo yanaisha.
ReplyDeleteSisi ni watu wa kitu kidogo na hakuna nayefuata sheria hapa TZ hata na sisi tunaoandika hapa.
Ama kweli mabasi yatatumaliza
Kila mtu anaangalia atafaidi nini akifuatilia mambo kama haya, vinginevyo atahamishiwa Namtumbo akafe njaa na kuishia kukagua baiskeli.
kwikwikwi kwekwekwe hahaha hohoho mdau hapo juu kanichesha kweli kweli eti serekali iweke speed camera njiani hivi huyu jamaa sijui iko dunia gani? hivi kwanini watu wanapenda kuionea serekali mimi naamini hizo camera zikiwekwa kesho saa nne asubuhi basi kubali au ukatae saa nne na robo itakuwa ni story ya hapa kuliwahi kuwa speed camera yani kesi kuliko zipungue basi ndo zitazidi bora kubaki bila hizo speed camera. mdau toka bujumbura
ReplyDeleteMamlaka ya kodi TRA imefanikiwa kwa kiasi kikubwa kuwashika wakwepa kodi kwa kuwa na vifaa na muundo wa kisasa...je kwa nini na muundo wa mwenendo wa vyombo vya usafiri usipatiwe uangalizi wa mitambo maalumu?
ReplyDelete