Mdau Mwalimu Kipanga akiwa katika pozi la picha mara baada ya kulamba nondozz yale ya Bachelor Of Business Administration katika Chuo Kikuu cha Dodoma baada ya kutunukiwa katika mahafali ya pili ya chuo hicho.
Mdau Mwalimu Kipanga akipokea kitabu cha Qur'aan kutoka kwa Mama yake Mzazi,Bi. Mwanakombo Jumaa mara baada ya kulamba nondozz yake ya Bachelor Of Business Administration katika Chuo Kikuu cha Dodoma mwishoni mwa wiki.ambapo Mama alimsihi kijana wake pamoja na kufuzu elimu ya dunia asisahau imani yake, pamoja na kujiendeleza zaidi. Mgeni rasmi katika mahafali ya 2 ya Chuo hicho alikuwa Rais Mstaafu awamu ya tatu,Mh. Benjamin Mkapa ,(hayupo pichani)
wahitmu wakipozi kwa picha mara baada ya kulamba Nondozz zao mwishoni mwa wiki katika mahafali ya pili ya Chuo Kikuu cha Dodoma , (kutoka Kulia) Juma Setumbi –Shahada ya Biashara katika Rasilimali Fedha, yaani Bachelor of Commerce in Finance, Khadija Kitambulio (katikati) Shahada ya Elimu ya Jamii katika Sosholojia- na Mwalimu Kipanga (kushoto) Shahada ya Uongozi katika Biashara yaani Bachelor of Business Administration).
Mdau Mwalimu Kipanga akielekea kwenye mahafali ya pili ya Chuo Kikuu Cha Dodoma ambapo ametutukiwa Shahada ya kwanza ya Uongozi katika Biashara (Bachelor of Business Administration).

Michuzi Blog

Tanzanian blog operating since 2005, covering International news and Local News, including Politics, Fashion, Social Scenes, Interviews, Movies, Events, personalities and anything positive happening worldwide. Written in Swahili and English targeting both Swahili and English readers.

Toa Maoni Yako:

Kuna Maoni 4 mpaka sasa

  1. Yaani mama Bi Mwanakombo hongera sana kwa kumuasa vyema mtoto wako mpendwa.

    Nakupongeza sana kwani siyo wazazi wengi wanaokumbuka zawadi kama hiyo adhimu.

    ReplyDelete
  2. Mwalimu Kipanga!Mama kakupa zawadi nzuri mno ya Qur'an!usiiweke ndani isome na uifuate atakusaidia hapa Duniani na kukuokoa Akhera!
    Ahlam UK

    ReplyDelete
  3. Maashaallah!!!!
    Nakuomba umuenzi mama yako kama anavokuenzi.

    ReplyDelete
  4. mashallah,hongera sana,na usije ukamsahau mama yako,maana ameonesha jinsi anavyokujali na kukuthamini,na usimsahau muumba wako

    ReplyDelete

Hii ni Blog ya Watanzania popote walipo duniani kwa ajili ya kuhabarisha, kutoa/kupokea taarifa na kuelimisha mambo yote yaliyo chanya kwa Taifa letu. Tafadhali sana unapotoa maoni usichafue hali ya hewa wala usijeruhi hisia za mtu/watu. Kuwa mstaarabu...