Wachezaji wa timu ya soka ya Tanzania ‘taifa stars’ wakiwasili katika Uwanja wa Ndege wa Kimataifa wa Julius Nyerere jijini Dar es Salaam leo wakitokea N’Djamena ambapo waliifunga timu ya taifa ya Chad kwa mabao 2-1. Timu hizo zinarudiana kesho katika Uwanja wa Taifa jijini Dar es Salaam. (Picha na Francis Dande).
Kocha Mkuu wa Taifa Stars,Jan Paulsen akiongea na waandishi wa habari katika  Uwanja wa Ndege wa Kimataifa wa Julius Nyerere jijini Dar es Salaam leo.Taifa Stars wamewasili leo wakitokea N’Djamena nchini Chad kushiriki mchezo wa kimataifa ambapo waliifunga timu ya taifa ya Chad kwa mabao 2-1.
Wachezaji wa Timu ya Taifa wakiwa ndani ya Basi lao.
Washabiki wa wakiwa wameizunguka Basi iliyokuwa imewabeba wachezaji wa Timu ya Taifa.

Michuzi Blog

Tanzanian blog operating since 2005, covering International news and Local News, including Politics, Fashion, Social Scenes, Interviews, Movies, Events, personalities and anything positive happening worldwide. Written in Swahili and English targeting both Swahili and English readers.

Toa Maoni Yako:

Kuna Maoni 17 mpaka sasa

  1. Headphones nini, ushamba flani hivi, acheni.

    ReplyDelete
  2. kidogo tim haina sura ngumu inaonyesha angalau kuna vijana

    ReplyDelete
  3. Msibweteke vijana, kazi bado ipo si utani kukolifai wc. Fanyeni mazoezi ati! Chad ni nchi ndogo sana kisoka wala sidhani kama ipo kwenye list ya fifa. Ila tunawapongeza.

    ReplyDelete
  4. Hebu wacheni ma big head kwa ushindi mmoja jamani!

    ReplyDelete
  5. washamba asili zao zinaonekana waziwazi

    ReplyDelete
  6. acha wajidai nazo kwani wamekuomba pesa ya kununulia acha wivu wa kizamani

    ReplyDelete
  7. Acha ushamba wewe mdau kwani kula muziki wakati wa sakari ni ushamba, ahh watuwengine bwana... kula muziki wakati upo ndani ya ndege hata husaidia masikio yasitesekke sana na altitude na kelele za ndege....

    ReplyDelete
  8. acha ubwege wewe kwani headphones matumizi yake nini au nani anastahili kuvaa, au unafikiri wana vaa ma Dj tuu

    ReplyDelete
  9. hilo basi lilivyo-park linawakilisha uchizi na kutofuata sheria kwa madereva wetu maana huyo dereva amepanda sttripped barrier kuweka basi lake ndio maana ajali haziishi

    ReplyDelete
  10. nimependa sana basi la timu ya taifa lilivyopaki...!
    ushamba mbona ndio zetu,
    usishangae wakaenda bungeni Dodoma ! bongo bana! sijui tuna nini sisi ..kah!

    ReplyDelete
  11. Waswahili bwana!Hata mkiwa nje za nchi kujifunza tamaduni za wenzeti hambadiliki kamwe mnanikera sana watanzania,kwani kusikiliza mziki ni ushamba nyie nyang'au??????????alafu mnashangaa kwa Timu yetu kwenda Bungeni mbona Timu za wenzetu NBA huwa wanaenda White House wakipata ushindi?mbona huwa amsemi ushamba wewe kuku?Acha upuuzi elimika mbwa weeee.

    ReplyDelete
  12. achen ushamba wa kukosa uzalendo!km nch ndogo lkn si tumeshinda?safi sn taifa stars,vjn ur free kuenjoy headphones are ok,au mpk umuone drogba na hizo hd fones ndo utakubali?achen upumbavu na wivu wenu wa kijinga.

    ReplyDelete
  13. Mengine yote semeni, lakini hili la parking linatutia aibu. Inaelekea huyu dereva hajui kabisa maana ya alama za barabara. Anafikiri udereva ni kuingiza gia, kukanyaga ekselerata na breki pekee!!! Ndiyo maana barabara zetu hazidumu, madereva wanapanda misingi ya vizuizi vya barabara mpaka basi. Wabongo bwani!! Lakini wepesi wa kulalamika.
    Wanausalama wa barabarani mpo hapo?

    ReplyDelete
  14. Kwenye MPIRA hakuna cha timu ndogo.Timu imeshinda..habari ndiyo hiyo.Hongera vijana.Parking dereva atakuwa amepata ujumbe.
    Tukiwatoa hao jamaa kundi letu wee!!.Morocco,Gambia,Cote d'ivoir.Siyo kundi baya.Nchi ya kuogopa sana hapo ni Gambia(ndiyo Gambia)..Morocco tulishacheza nayo(Hakuna kubabaika tena),Akina Drogba tulishacheza nao(Hakuna kubabaika tena).

    David V

    ReplyDelete
  15. kumekucha na sisi sasa tumecharuka!,,,kazi bado ipo mbele, Chad wapewe tena kichapo kesho mzunguko wa pili warudi kwao.

    ReplyDelete
  16. watanzania na wadau wa michezo na sereksli ndo wa kuinua tim yetu na tusichoke kuipa moyo kwani safar bado ni ndefu na kimpira bado tupo nyuma (RAJABU ALLY MNDEWA)

    ReplyDelete
  17. Watu wengine si hawajui matumizi ya headphones ni nini msishangae binadamu tunatofautiana, Wanajua ni kwa ajiri ya Dj'z tuu kwi kwi kwi kwi kwi,hongera stars kwa ushindi na leo lazima tuwachape nyumbani!

    ReplyDelete

Hii ni Blog ya Watanzania popote walipo duniani kwa ajili ya kuhabarisha, kutoa/kupokea taarifa na kuelimisha mambo yote yaliyo chanya kwa Taifa letu. Tafadhali sana unapotoa maoni usichafue hali ya hewa wala usijeruhi hisia za mtu/watu. Kuwa mstaarabu...