katibu Mkuu wa Wizara ya Kazi na Ajira,Bw.Eric Shitindi alipokuwa akizungumza na wanahabari katika ukumbi wa Mikutano wa Wizara ya Kazi na Ajira.Katibu Mkuu aliwajuza wanahabari kuwa Wizara hiyo itakuwa na maonyesho ya utendaji wake mbalimbali katika kipindi cha miaka 50 ya Uhuru.Maonyesho hayo yataambana na Wiki ya Hifadhi ya Jamii ambayo itahusisha Mamlaka ya Usimamizi na udhibiti wa Sekta ya Hifadhi ya jamii na Mifuko yote ya Hifadhi na jamii Tanzania Bara (GEPF, LAPF,NSSF,PPF,NHIF,PSPF).
Wiki ya Hifadhi ya Jamii ambayo ni mara ya kwanza nchini Tanzania, itazinduliwa rasmi na Waziri wa kazi na ajira Mh.Gaudentia Kabaka siku ya tarehe 08/11/2011 katika viwanja vya maonyesho vya Mnazi Mmoja. Kusudi kubwa la wiki hii ijayo kuanzia tarehe 08/11 mpaka 13/11/2011 katika viwanja vya Mnazi mmoja.Kusudi kubwa la wiki ya Hifadhi ya Jamii ni kuulelimisha Umma juu ya Sekta ya Hifadhi ya Jamii na umuhimu wa kila mwananchi kuwa mwanachama na kuendeleza uanachama katika sekta hiyo.




Wakuu Wa Mifuko ya PPF,PSPF,GEPF wakifuatilia kwa makini maelezo ya katibu mkuu


Mkurugenzi wa mamlaka ya Usimamizi na Udhibiti wa Sekta ya HIfadhi ya jamii (SSRA) Bi. Irene Isaka- katikati, na Mkurugenzi mkuu wa LAPF,Bw. Eliudi Sanga wakifuatilia maelezo ya Katibu Mkuu 

Katibu Mkuu,Naibu katibu Mkuu,Kamishna Wa kazi na ajira,Mkurugenzi mkuu wa SSRA katika picha ya pamopja na wakuu wa mifuko ya Hifadhi ya Jamii Tanzania Bara.

Michuzi Blog

Tanzanian blog operating since 2005, covering International news and Local News, including Politics, Fashion, Social Scenes, Interviews, Movies, Events, personalities and anything positive happening worldwide. Written in Swahili and English targeting both Swahili and English readers.

Toa Maoni Yako:

Kuna Maoni 3 mpaka sasa

  1. Kijana wa mzee poti umependeza. Irene hujambo!!
    Mdau N.America

    ReplyDelete
  2. Eric is the best. Listen to this interview while he was a Deputy PS at president's office.
    http://www.princeton.edu/successfulsocieties/content/focusareas/CS/oralhistories/view.xml?id=264

    Mdau, Canada

    ReplyDelete
  3. TUKIJIPANGA, SUALA LA KUJITEGEMEA INAWEZEKANA!...mifuko kama hii inaweza kutukomboa kutoka ktk makucha na masharti magumu ya MISAADA ya WAINGEREZA na Bwana DONALD CAMERON wao!

    ReplyDelete

Hii ni Blog ya Watanzania popote walipo duniani kwa ajili ya kuhabarisha, kutoa/kupokea taarifa na kuelimisha mambo yote yaliyo chanya kwa Taifa letu. Tafadhali sana unapotoa maoni usichafue hali ya hewa wala usijeruhi hisia za mtu/watu. Kuwa mstaarabu...