Mkurugenzi Mtendaji wa Benki ya NBC, Lawrence Mafuru (kushoto) akishiriki kusakata dansi lililokuwa likiporomoshwa na bendi ya FM Academia ‘Wazee wa Ngwasuma’ wakati wa sherehe za Siku ya wanafamilia wa benki hiyo katika Hoteli ya South Beach, Dar es Salaam.
Baadhi ya wafanyakazi na wanafamilia wa benki ya NBC wakishindana katika mbio za magunia katika Siku ya Wanafamilia ya benki hiyo katika Hoteli ya South Beach, Dar es Salaam jana. Robert Kusekwa (wa pili
kulia) alibuka kidedea.
Baadhi ya wafanyakazi na wanafamilia wa benki ya NBC wakishindana katika kuvuta kamba ili kumpata mshindi katika Siku ya wanafamilia ya benki hiyo katika Hoteli ya South Beach, Dar es Salaam.
Baadhi ya watoto wa wafanyakazi wa benki ya NBC wakifurahi katika bwawa la kuogelea ikiwa ni baadhi ya burudani kuadhimisha Siku ya Wanafamilia ya benki hiyo katika Hoteli ya South Beach, Dar es Salaam.
Ofisa Uhusiano wa NBC, Eddie Mhina akigawa zawadi kwa baadhi ya watoto wa wafanyakazi wa benki hiyo wakati wa sherehe za Siku ya Wanafamilia wa benki hiyo jijini Dar es Salaam.

Michuzi Blog

Tanzanian blog operating since 2005, covering International news and Local News, including Politics, Fashion, Social Scenes, Interviews, Movies, Events, personalities and anything positive happening worldwide. Written in Swahili and English targeting both Swahili and English readers.

Toa Maoni Yako:

Kuna Maoni 5 mpaka sasa

  1. kama kawa wabongo tutaishia kuvuta kamba na kukimbizana na magunia!!

    ReplyDelete
  2. Mdau wa kwanza, it's true :-) Hakuna creativity, kampuni inayobuni haya mambo ni moja tu na imeishiwa ubunifu.

    BTW, hivi Mafuru ni mzee au kijana? Nauliza kwa mara ya pili leo, jamaa huwa ananichanganya changanya sana taswira yake, itabidi siku moja nimvizie mitaa ya ofisini kwake nimcheki.

    ReplyDelete
  3. Acha hizo wewe mdau hapo juu wivu nini? NBC hongereni sana kwa matunda yenu mko juu!!

    ReplyDelete
  4. Nice event, well done NBC

    ReplyDelete
  5. Ubunifu ni muhimu sana kwa maendeleo ya jamii,,,ili tusichoke na mitindo ile ile inabibi waandalizi wetu wa mipango wawe wana jaribu ku akisi kutoka vyanzo tofauti ili kubuni vitu vipya vinavyoendana na jamii yetu ktk sekta zote za maisha, utendaji,simamizi wa jamii,sanaa na utamaduni,siasa, na vingine vingi!

    ReplyDelete

Hii ni Blog ya Watanzania popote walipo duniani kwa ajili ya kuhabarisha, kutoa/kupokea taarifa na kuelimisha mambo yote yaliyo chanya kwa Taifa letu. Tafadhali sana unapotoa maoni usichafue hali ya hewa wala usijeruhi hisia za mtu/watu. Kuwa mstaarabu...