Mwenyekiti wa kamati ya maandalizi ya Mkesha Mkubwa – Dua maalum kwa Taifa askofu Godfrey Emmmanuel Malasi (katikati) akizungumza na waandishi wa habari leo jijini Dar es salaam kuhusu mkesha mkubwa wa kuliombea taifa utakaofanyika katika uwanja wa taifa Desemba 31,2011 ambapo mgeni rasmi atakuwa rais wa Jamhuri ya Muungano wa Tanzania Dkt.Jakaya Kikwete. Wengine ni Viongozi wa kamati hiyo kutoka Umoja wa makanisa ya Kikiristo Tanzania (Tanzania Christian Fellowship of Churches).
Viongozi wa mkesha mkubwa wa kuliombea taifa (waliosimama mbele) wakifanya maombi maalum kwa waandishi wa habari ili waweze kutekeleza majukumu yao ya kuitumikia jamii kwa uadilifu kutokana na changamoto mbalimbali wanazokumbana nazo.Maombi hayo yamefanyika leo jijini Dar es salaam.
Na. Aron Msigwa – MAELEZO.
Umoja wa makanisa ya Kikiristo Tanzania (Tanzania ChristianFellowship of Churches) umeandaa mkesha mkubwa kwa ajili ya dua maalum kwa taifa kwa lengo la kumshukuru Mungu kwa kulivusha taifa katika kipindi cha miaka 50 ya uhuru na kuanza kipindi kingine ambapo mgeni rasmi katika mkesha huo atakuwa rais wa Jamhuri ya Muungano wa Tanzania.
Akizungumza na waandishi wa habari leo jijini Dar es salaam, mwenyekiti wa kamati ya maandalizi ya Mkesha mkuu kutoka Tanzania Christian Fellowship of Chrches Askofu Godfrey Emmmanuel Malasi amesema watanzania wanapaswa kujua Mungu anakusudi gani na taifa la Tanzania katika kipindi hiki ambacho Taifa limetimiza miaka 50 ya uhuru na kuanza kipindi kingine na kutoa wito kwa kila mtanzania kufanya kazi kwa bidii na kushiriki katika uchumi wa taifa.
Amesema serikali inazo sera nzuri za kuweza kuwamilikisha wananchi rasilimali ziliizopo nchini ili waweze kuishi maisha bora na kuongeza kuwa wananchi wanapaswa kutambua majira na wakati uliopo sasa wakati taifa linapoanza miaka 50 mingine ya uhuru kwa kuzitumia fursa zilizopo kujiletea maendeleo.
“Kila mmoja anapaswa kushiriki na kushirikishwa kikamilifu katika uchumi wa taifa letu ambalo sasa limemaliza miaka 50 ya uhuru, kila mtu anapaswa kutambua nafasi yake, tusikae kwa kubweteka, tusikae kwa kulalamika kila mtu ajue ni wakati wa kumiki na kurithishwa rasilimali zilizopo katika taifa hili”
Amesema mwaka huu dua maalum kwa taifa litafanyika katika mikoa 14 ya Tanzania ikiwemo Dar es salaam, Arusha, Mwanza,Kilimanjaro, Singida Iringa, Mbeya ,Iringa, Kagera, Dodoma, Ruvuma, Tabora,Tanga na visiwa vya Zanzbar na Pemba.
Amefafanua kuwa katika mkesha huo viongozi mbalimbali wa taifa ,vyama vya siasa na balozi mbalimbali zipatazo 37 zilizopo nchini zimearikwa kushiriki mkesha huo na kuongeza kuwa tayari baadhi ya balozi zimethibitisha kushiriki mkesha huo.
Kuhusu maadalizi ya mkesha huo askofu Godfrey Malasi amesema yanaendelea vizuri na kutoa wito kwa wananchi kujitokeza kwa wingi katika dua hiyo maalum na kuongeza kuwa mkesha huo utaambatana na tukio maalum la watoto 50 kusimama uwanjani na kutamka maneno ya kupokea miaka 50 ijayo ikiwa ni ishara ya kupokea kizazi huru cha watanzania.
Kwa upande wake makamu mwenyekiti wa kamati ya mkesha mkuu wa Taifa Askofu Keneth Damas ameipongeza serikali kwa kuwa na msimamo wa kupinga suala la ndoa za jinsia moja (ushoga) katika mikutano ya kimataifa iliyofanyika hivi karibuni na kuuita uamuzi huo kuwa ni ushindi mkubwa kwa taifa la Tanzania na watu wake katika kuheshimu utu na utamaduni wa taifa na uukataaji wa vitendo vya udhalilishaji na kuongeza kuwa wao kama viongozi wa dini wataendelea kuonya na kufundisha watu wajue athari za dhambi hiyo.
“Sisi kama viongozi wa makanisa katika nchi hii tunapinga kwa nguzu zote vitendo vya ushoga ndani ya taifa letu, vitendo vya ushoga ndivyo vilivyosababisha Sodoma na Gomora kuchomwa moto kwa kuwa vilimchukiza sana Mungu, Sisi kama viongozi wa dini katika kizazi chetu na vizazi vijavyo hatutaki kufikia hapo na kuona taifa letu likichomwa moto”




Kama mnamuomba Mungu muumba wa Mbingu na ardhi na kila kilichomo baina yake tuko pamoja. Lakini kumuomba aliyeumbwa na Mungu i.e. Jesus hatuko pamoja, lakini tutaendelea kuheshimiana. Ni hayo tu.
ReplyDeleteNdugu zangu Waislam, nina wasihi msihudhurie mkutano huu, dua hii anaombewa nani? Tanzania si haina dini! Huu nimuendelezo tu wa wakristo kutaka kui-christianize Tanzania na hususan Pwani, tusikubali.
ReplyDeleteUSHOGA KWA IMANI ZETU ZOTE TANZANIA, HADI MAPAGANI NA DINI ZA JADI...TUNAUKATAA KATA KATA!!!, Afadhali turudi kule kuleeee kwenye SIASA YA UJAMAA NA KUJITEGEMEA KULIKO KUMTEGEMEA TAAHIRA MWINGEREZA NA MASHARTI YAKE YA KIMSUKULE YA MISAADA!
ReplyDeleteNyie anonymous sisi tulio wengi tutaenda na tutaomba katika jina la Yesu. Sisi twaongozwa na Roho mtakatifu na kweli. Nyie mnaotegeme mwili na sheria hayo ni yenu. Msituletee udini hapa
ReplyDeletekwani wimbo wa taifa hautoshi? na kwanini iwe usiku?
ReplyDeleteAnony Wed Dec 28, 07:17:00 PM 2011, kama unadai unaongozwa na Roho mtakatifu. Kama kweli wewe ni muumini Yesu/Jesus kashakupa mtihani huu hapa:
ReplyDeleteMark 16
15 He said to them, “Go into all the world and preach the gospel to all creation. 16 Whoever believes and is baptized will be saved, but whoever does not believe will be condemned. 17 And these signs will accompany those who believe: In my name they will drive out demons; they will speak in new tongues; 18 they will pick up snakes with their hands; and when they drink deadly poison, it will not hurt them at all; they will place their hands on sick people, and they will get well.”
Swahili
15Akawaambia, ``Nendeni ulimwenguni kote, mkawahubirie watu wote Habari Njema. 16Ye yote atakayeamini na kubatizwa ataoko lewa. Lakini ye yote ambaye atakataa kuamini, atahukumiwa.
17``Na hizi ndizo ishara zitakazoandamana na wale wata kaoamini: Kwa kutumia jina langu watafukuza pepo; watasema kwa lugha mpya;
18wataweza hata kuwakamata nyoka na kunywa sumu lakini wasidhurike; watawawekea wagonjwa mikono, nao watapona.''
Je waweza kunywa sumu?
Suala la kuliombea Taifa na kujiombea sisi wenyewe ni zuri na endapo nia ya kuwasiliana na Mungu wa dhati na kwa dhati itakuwepo.Lakini kwa mtizamo mwingine ibada za usiku na zenye kushirikisha wahumini wenye imani tofauti,huwa shetani anajipenyeza kati na kuwateka walio wake na kuanza kumsurubisha Bwana Yesu Msalabani usiku huo[X].Kama hiyo haitoshi,sina uhakika kama watumishi walioandaa mkesha huu hawapo kwenye orodha ya wale wanaoshiriki biashara ya dawa za kulevya na waliokwisha nyooshewa vidole.Nawaomba kama mpo na mtasoma oni hili,ni bora msishiriki mkesha huo la sivyo mtaumbuliwa siku siyo nyingi.Mungu awabariki kwa kazi hii.Amina.
ReplyDeleteWe anonymous. Usipotoshe maandiko. Unataka ninywe sumu ili nimjaribu Muumba wangu? Imeandikwa Usimjaribu Mungu wako? Na nyie kwa nini mnaambiwa peponi mtapewa masuria walio bikra na wanawake pia watapewa masuria? Usagaji huo! Na hapa duniani mnawanyanyasa sana wanawake kwa kuwaoa na kuwataliki kiasi watoto wenu wanakosa malezi mema.
ReplyDeleteAcheni utapeli ninyi! Maombi yanatakiwa kila mara na wala si matamasha ya kuuza sura kwa kisingizio cha kuliombea taifa.
ReplyDeleteKwa nini mkesha tena wa kuombea Taifa uwe usiku????????????????????.
ReplyDeleteKuna niniiiiiiiii, watoto watabaki na nani nyumbani usiku????? na dada wa nyumbani Je yeye hafai kuombea Taifa lake au kwa sababu hana uwezo haina haja ya kumuomba Mungu?????????? ina maana watoto wasishiriki katika Ibada hiyo, hawafai au????????? kwa nini iwe uwanjani hamna nyumba za ibada???????? kama mna nia njema tuombeeni kama maswala ya siasa mtaumbuka vibaya. Je waandaji wa mkwsha hou sio wale wauzao madawa ya kulevya??????? mtaibua vingine nyie walokole mnavyojiita msukule haitakuwepo kweli.....
WAISLAMU IWE MARUFUKU KUHUDHURU VITU KAMA HIVI NAWAOMBA SANAAAAAAAAAAAAAAAA HAWAAMINIKI HAWA NUKSIIIIIIIIIIIIII
huenda na haya mafuriko yametokana na laaaaaaaana zenu za viongozi wa dini kuhusika na madawa ya kulevyaaaa
ReplyDeleteSie tunatoa sadaka kibao hamfanyi ya maana mnajirajirisha tuuuuuuuu mnaona haitoshi mnaanza kuuza madawa ya kulevyaaaaaaaaaa laaaaaaaaaaakum
Anony Thu Dec 29, 12:24:00 AM EAT Mr Ex Muslim: Haya ndo matatizo mlokuwa nayo watu kama wewe, unashindwa na hoja unaanza matusi. Kwa mtazamo wangu unaonekana unaishi USA wewe au la utakuwa unasikiliza sana propanada za watawala wako. Mimi nimechukua maandiko kama yalivyo kwenye bibilia na kukuonyesha.
ReplyDeleteUkweli ni kwamba husomi kitabu chako unachokiamini, kwa hiyo hii imekua kama mshtuko kwako, maana hukutegemea kuona vitu kama hivi ndo maana unaanza matusi.
Kwa taarifa yako,hii tactic ya kusema waislaam wanatesa wanawake inatumiwa sana na hao wanaotaka kuwaletea ushoga Bongo. Kama wanawake wa kiislaam wanateswa basi ingekua wote wanawakimbia waume zao, lakini sijaona hilo. Ni mengi ya kukuelimisha lakini humu si mahala pake. Ushauri wa bure, fungua macho umepigwa changa la macho huoni wewe kwa sasa, ukishtuka muda umekwisha.
ACHENI MAWAZO POTOFU KUMBUKENI HAKI ZA BINADAMU HAO MASHOGA NI BINADAMU KAMA WENGINE KWANINI WASIPIGANIE HAKI ZAO ?SISI TUKUMBUKE NI WATU WA KUSAIDIWA KWA KILA KITU KAMA HATUTAKI KUFUATA SHERIA NA HAKI ZA WENGINE TUTAKIONA ! TUSIKAE TU KUSEMASEMA WAKATI HATUJUI LOLOTE WALA ELIMU HATUNA BADO YA KUTUFANYA TUJIKOMBOE WENYEWE BILA MSAADA WA HAO WETU AMBAO WALITUTAWALA NA BADO WANATUTAWALA NA WATAENDELEA KUTUTAWALA MPAKA KARNE TANO ZIJAZO.
ReplyDeleteHIO SALA HAISAIDII CHOCHOTE KWANI HUMO HUMO MAKANISANI USHOGA NDIO UNATAWALA.MAPADRE WA ROMAN CATHOLIC WAMESABABISHA MPKA DINI IANZE KUSAMBARATIKA KWA SABABU ZA VITUKO VYA USHOGA NA KULAWITI WAVULANA WADOGO WADOGO NA SIO SIRI HIO DUNIA NZIMA INAJUA SASA MIMI BINAFSI SIELEWI KWA NINI HUO USHOGA USIWEKWE HADHARANI. NIMEONA KWA MACHO YANGU MCHUNGAJI WA KANISA ROME AKINIBEMBELEZA NIKAMTIE NYUMA NA YEYE NDIO MTU WA KANISA HUSIKA NA AKANAMBIA HI DHAMBI KWA BINADAMU KAMA HAWEZI KUPATA HAJA YAKE ETI NI DHAMBI, HUO USHOGA NI MAUMBILE YA BINADAMU ALIVYOZALIWA WALA HAWEZI KUBADILIKA NA UKITUMIA NGUVU ZA ,HIO WEWE SASA NDIO UNADHAMBI.
KWANI KIPI BORA KUJIFICHA AU KUWEKA HADHARANI ILI KILA MTU AJULIKANE HISIA ZAKE NI ZIPI?
HALAFU TUKUMBUKE SISI WAAFRIKA HATUNA DINI, KWANI KWENYE HISTORI YA DINI HATUJAWAHI SIKIA KAMA KULIKUWEPO MTUME MWEUSI WOTE WATUME WALIKUWA WATU WEUPE AU WA RANGI KAMA WAARABU . MTUME MOHAMMAD ALIKUWA MUARABU , YESU ALIKUWA MZUNGU AU MJEWISH NA NDIO HAO SISI TUNAFUATA NYAYO ZAO. SIJASIKIA MTU MWEUSI HUSUSAN MUAFRIKA ATI ALIKUWEPO KWENYE UTAWALA WA DINI SISI TULIKUWA NI WATUMWA NA TUTAENDELEA KUWA WATUMWA
TANZANIA HAITOKUWA NA DEMOCRAY KAMA HAKI ZA BINADAMU HAZITOPATA NAFASI KATIKA JAMII. TUSIWE WABAGUZI KWA KUKIONA KITU SIO CHA SAWA WAKATI WANAOLETA MAENDELEO YA DUNIA KARIBIA ASILI ,MIA40 NI MASHOGA. AMBAO NI MADAKTARI, MAINJINIA,VIONGOZI WALIOKUWA NA SIFA. WAKIKASIRIKA TUTAUMIA NA WANAUWEZO WA KUTUUMIZA. LAZIMA TUANGALIE WATU WENGINE WANAISHI VIPI TUSIJIANGALIE TU SISI NA MAISHA YETU YA KITANZANIA TUKAJIONA KANA KWAMBA TUNAWEZA KILA KITU NA TUNA NGUVU YA KUKATAA MAMBO MUHIMU YA DUNIA,
NAMALIZIA KWA KUSEMA KUWA NCHI ZA KIISLAAM KAMA VILE SAUDIA, PAKISTAN, AFGANISTAN NA DUBAI NINAVYOIFAHAMU MIMI NDIO VINARA WA SHUGHULI HIZI ZA USHOGA AMBCHO NI KITU KILA MTU ANAKIJUA LAKINI HAWATAKI KUKIDISCUSS KATIKA BUNGE LAO KWANI KARIBIA KILA KIJANA WA 4 WA UARABUNI KISHA MFANYA MSENGE TENA KWA KUNUNUA.WANAWALETA MASHOGA KUTOKA UFILIPINO NA THAILAND NA PAKISTAN IJLI WAJE WAWARIDHISHE HAJA ZAO NA WAKO NJE NJE BILA KUFICHA KITU . KWA NINI SISI NDIO TUONE NI KITU CHA AJABU MPAKA KIOMBEWE SALA?
Mungu amemuita kila mtu kwa ubinafsi, kama Mungu wake aliyemuita kamuelekeza kufanya hivyo, wewe inakukera nini? kusudi la maombi ni jema, na mimi naamini Mungu mpenda amani hachukii kusudi lilo jema. Wewe kama huendi,ni wewe, wako watakaoenda. Watz tutaacha kulalamika kwny kila jambo, lini? hata mambo yanayojenga umoja na amani???? kama mtu anafanya jambo kwa kusudio jema hata kama wewe hulipendi anasitahili kutiwa moyo kwa kusudi hilo lilo jema.
ReplyDeleteTumwombe Mwenyezi Mungu atupe hekima na busara katika swala hili, kama wewe unaona alikuhusu na ulipendi ni bora ukae kimya kuliko kutoa lugha mbaya, hakuna binadamua ndani ya hii dunia anamadaraka ya kumhukumu binadamu mwenzake ni Mungu peke yake; mbele za Mungu hakuna dini ila sisi binadamu kwa tamaa zetu ndio tumepanga dini, sote tu wamoja mbele za Mungu na ndo manaa hakuna naeishi akhera wote tupo tunakanyaga kwenye udongo wa dunia.
ReplyDeleteBwana Esu si alikufa vile, atasikia kweli maombi ya nchi isiyo na dini?
ReplyDeleteSasa mnawajuwa viongozi walafi, walioandika na wanaondika mikataba mibovu, mnawajua kabisa viongozi waliojilimbikizia mali kwa njia ya wizi, rushwa na ufisadi, mnawajua kabisa viongozi wa miradi ya kila aina waliofuja hela kushindwa kutimiza miradi, mmnawajua kabisa viongozi wasiotii na kufuata sheria za nchi, sasa huyu mungu mnayetaka kumuomba, mnataka afanye nini? Matatizo yote nchini, kuanzia maafa baharini, mitoni, maziwani, barabarani na n.k. yametokana na kutowajibika kwetu, hakuna hata kiongozi wa maana aliepewa miaka kadhaa jela wala kushughulikiwa kwa ufasaha, hata huyo mungu anawatazama, anawakejeli, anajiuliza, hawa mbona sheria wanazo, askari wanao, majaji wanao, sasa kwanini hakuna cha maana kinachofanyika pale kuona kweli nao wanajisaidia.
ReplyDeleteAcheni kupoteza muda, nguvu na wakati wetu.
Matatizo yote nchini yamesababishwa na ufisadi wetu au wa viongozi wetu.
Mungu hausiki, na hata hizo sala haziwezi kufika!
TUNAOMBA SERIKALI KUSITISHA AU KUSIMAMISHA HAYA MAOMBI MAANA KWA UPEO WANGU NAONA KABISA DALILI ZA UDINI ZINAKARIBIA TUMKUMBUKE BABA WA FAIFA KWA KUFATA MANENO YAKE LAA SIVYO TUTAPOTEZA TAIFA.
ReplyDeleteMUNGU IBARIKI TANZANIA
Dini hamsaidii mwanadamu chochote, mtatoana roho mnabishania hewa...! Mungu peke yake ndiye Mungu wa kuabudiwa. na kama mkesha huu ni kumuomba Mungu kwa taifa, mimi nasema na waombe kwa bidii...! taifa hili linamuhitaji sana Mungu wakati huu. Mungu bariki Afrika, Mungu ibariki Tanzania.
ReplyDeletehttp://www.mkeshamkubwa.org
ReplyDeleteTunamshukuru Mungu kwamba Mkesha ulifanikiwa sana kwani watu wengi wanaomtii Mungu na wanaolipenda Taifa na viongozi wa Tanzania waliitikia na walikuja kwa wingi na tuliomba kwa ajili ya Taifa letu kuanzia jioni saa kumi na mbili hadi asubuhi saa kumi na mbili asubuhi.Mheshimiwa Samwel Sitta ,Waziri wa Ushirikiano Afrika Mashariki alikuwa ndiye mgeni rasmi akimwakilisha Rais wetu Mpendwa Jakaya Kikwete ambaye ndiye alikuwa amealikwa kuwa mgeni rasmi lakini kutokana na majukumu aliyonayo hakuweza kuhudhuria.
ReplyDeletePia alikuwepo Dk Mwakyembe ambaye ni waziri wa uchukuzi na aliweza kushiriki nasi mpaka saa tisa usiku.Pamoja nao walikuwepo wawakilishi wa mabalozi kutoka kwa Majirani zetu wazuri wa Rwanda na Burundi na Zambia na tuliomba kwa ajili ya nchi zao.Majirani zetu kutoka Kenya nao walikuwepo na tuliomba pamoja.
Pamoja nao alikuwepo Dr.Mary Mwanjelwa Mbunge wa kuteuliwa kutoka Mbeya na viongozi wengine wengi tu kutoka serikalini.
Katika Mkesha huo watu wengi waliokolewa baada ya kuamua kuziacha njia zao mbaya na wakampa Yesu maisha yao baada ya mahubiri mazuri kutoka kwa Mtoto wa Mobuto Seseseko aliyekuwa Kiongozi na Rais wa iliyokuwa Zaire.Huu ulikuwa ni mkesha wa 16 tangu kuanza kwa maono haya.Ni mkesha wa Watanzania wote bila kuchagua rangi wala dini zao na huhudhuriwa na watu wote na hata miongoni wa waliokoka siku ile ni waislamu na watu wa madhehebu mengine.Watanzania sisi ni kitu kimoja tusibaguane kwa misingi ya dini, ukabila, rangi na chochote kile.
Pia kumwomba Mungu ni wakati woweote,mahali popote hata kama ingekuwa ni chini ya mti au uwanja wa taifa.Mungu wetu anapatikana kila mahali na husikia maombi na hujibu maombi kwa wakati wake.Maandalizi ya mkesha wa 17 tayari yameshaanza na karibuni sana kwa ajili ya maandalizi hayo kwani mkesha huu huandaliwa na Watanzania wote kupitia michango yao wanayotoa.Mungu atubariki sana Watanzania na tuzidi kupendana na kuwa na mshikamano kama tulivyokuwa tangu mwanzo-Sam