Mkuu wa Mkoa wa Tanga, Luteni (Mstaafu) Chiku Gallawa akizungumza katika Maadhimisho ya sherehe za miaka 50 ya Uhuru katika uwanja wa Jitegemee wilayani Muheza, sherehe ambazo kimkoa zitafanyika wilayani Korogwe Desemba 9. Mkuu huyo wa mkoa alisisitiza umuhimu wa wananchi mkoani Tanga katika kusherehekea miaka 50 ya uhuru kubadili mtazamo wa kutumia fursa na rasilimali zilizopo mkoani humo kujiletea maendeleo. Alisema mkoa huo umekuwa ukikabiliwa na changamoto nyingi lakini kubwa wananchi watumie ardhi yenye rutuba kulima na kujitosheleza kwa chakula ikiwemo kuongeza ushindani katika mazao ya biashara. Wengine kaika picha ni Mkuu wa wilaya ya Muheza, Bw. Methew Nasei (Kushoto), Mwenyekiti wa CCM wilaya hiyo, Bw. Peter Jambele na Katibu Tawala mkoa wa Tanga, Bw. Benedict Ole Kuyan.
baadhi ya viongozi waliofuatana na Mkuu wa mkoa wa Tanga, wakisikiliza hotuba mbalimbali za kiongozi huyo wakiwemo waasisi wa Uhuru wa Tanganyika. kutoka kushoto ni Mbunge wa Muheza CCM Bw. Herbert Mntangi, Msaidizi wa Mkuu wa mkoa wa Tanga Bw. Joseph Sura, Mwenyekiti wa halmashauri ya wilaya ya Muheza Bw. Amir Kiroboto na Mkurugenzi Mtendaji wa halmashauri ya wilaya hiyo Bw. Tem Goliati.Picha na Mdau Mashaka Mhando, Mzee wa Bonde.

Michuzi Blog

Tanzanian blog operating since 2005, covering International news and Local News, including Politics, Fashion, Social Scenes, Interviews, Movies, Events, personalities and anything positive happening worldwide. Written in Swahili and English targeting both Swahili and English readers.

Toa Maoni Yako:

Kuna Maoni 2 mpaka sasa

  1. Ni kwa nini ktk Tanzania Maafisa Tawala ngazi za juu wengi wanakuwa X Soldiers? (Wastaafu wa Jeshi na Idara za Usalama).

    Hawa maafisa wastaafu Wakuu wa Mikoa na Wilaya ina maana ktk uendeshaji wetu hakuna mahala pengine pa kuwaweka kama ktk Idara za utendaji kwa uzalishaji na usimamizi huduma za jamii ngazi za chini,,,kama mahospitali,mashule,ustawi wa jamii na kwingineko...inakuwa kama wamezaliwa Kutawala ngazi za juu tu?...!!!.

    ReplyDelete
  2. wastaafu jeshini kuanzia Captain kwenda juu ndiyo wenye ruhusa ya kutumia rank zao hata wanapokuwa wamestaafu. kwa msingi huo unafanya makosa kutumia cheo 'luteni mstaafu', sheria zetu haziruhusu hilo.

    iko siku utakutana na afande lt.gen.abdulrahmani shimbo atakupa somo zuri kuhusu suala hili.mwisho tutakuwa na private, lance corporal, au corporal mstaafu

    ReplyDelete

Hii ni Blog ya Watanzania popote walipo duniani kwa ajili ya kuhabarisha, kutoa/kupokea taarifa na kuelimisha mambo yote yaliyo chanya kwa Taifa letu. Tafadhali sana unapotoa maoni usichafue hali ya hewa wala usijeruhi hisia za mtu/watu. Kuwa mstaarabu...