NA MAGRETH KI NABO – MAELEZO

SERIKALI imesema kwamba msongamano wa ndege zinazosubiri kutua au kuruka katika Kiwanja cha Ndege cha Kimataifa cha Julius Nyerere umepungua baada ya kufanyika kwa ukarabati mkubwa ambao umeongeza uwezo wa kuhudumia ndege 30 kwa saa badala ya nane.

Kauli hiyo ilitolewa leo na Waziri wa Uchukuzi, Omari Nundu katika sherehe ya kuadhimisha siku ya kimataifa ya usafiri wa anga duniani zilizofanyika kwenye viwanja vya Mamlaka ya Usafiri wa Anga Tanzania(TAA) jijini Dares Salaam.

Ambapo kauli mbiu yake ni ‘Kusaidiana na Kushirikiana kwa ajili ya Usafiri Endelevu wa Anga Duniani’.

“Wizara kupitia Mamlaka ya Viwanja vya Ndege Tanzania imekamilisha matengenezo makubwa ya miundombinu na uboreshaji wa mitambo… Mategenezo haya yamejumuisha ukarabati mkubwa wa njia ya kurukia ndege, viungio vyake na maegesho ya ndege,”alisema Waziri Nundu.

Waziri Nundu aliongeza kuwa serikali itaendeleza juhudi za kuboresha miundombinu na ubora wa huduma za usafiri wa anga katika viwanja vya ndege nchini hadi viwepo vya kutosha vya kuweza kuhudumia nchi nzima. Hivyo kwa kuanzia serikali imepanga kushughulikia viwanja 17.

Aliongeza kuwa ili usafiri huo uwe endelevu,uwepo wa wataalam wa usafiri wa anga ni muhimu. Serikali itashirikiana na mamlaka hiyo na wadau wengine kuhakikisha kuwa Watanzania wengi wanapata mafunzo hayo.

Aidha Waziri Nundu alisema hatua za haraka zinapaswa kuchukuliwa katika suala hilo kwa kuwa marubani na wahandisi wengi wazalendo wana umri wa miaka zaidi ya 50, ambapo aliishauri mamlaka hiyo na wadau kuanza taratibu za kuimarisha mfuko wa mafunzo huku akiutaka uwe endelevu.

Naye Mkurugenzi Mkuu wa mamlaka hiyo, Fadhili Manongi alisema idadi ya abiria wanaotumia usafiri huo imeongezeka kutoka 1,206,821 mwaka 2000, hadi abiria 3,027,512 mwaka 2010 ambapo ni sawa na ongezeko la asilimia 151.

Alisema safari za ndege pia zimeongezeka kutoka 112,821 hadi 181,240 katika kipindi hicho kwa asilimia 61 na kuhusu utalii nchi ilipokea 782,699 kwa mwaka 2010 ukilinganisha na watalii 501,669 mwaka 2000.

Manongi aliongeza kuwa asilimia 50 au 60 ya watalii hutumia usafirihuo na iliyobakia wa barabara hawa wanaotoka nchini Kenya baada ya kuwasili kwa ndege nchini humo.

Michuzi Blog

Tanzanian blog operating since 2005, covering International news and Local News, including Politics, Fashion, Social Scenes, Interviews, Movies, Events, personalities and anything positive happening worldwide. Written in Swahili and English targeting both Swahili and English readers.

Toa Maoni Yako:

Kuna Maoni 5 mpaka sasa

  1. Mmekarabati na ndani? Vyoo vipi ile harufu na joto linavotutesa wakati wote, aircondition vipi tayari?

    ReplyDelete
  2. nilitaka kusema haya haya ya anon wa 11:23.ndani ni kuchafu sana.pia mkianza ya ndani msisahau na fenicha za wafanyakazi wenu jamani inakera mno.Hivi hamuendagi hata Jomo Kenyatta International Airport kwenye study tour manake nadhani mi nikipewa vyeo vyenu nitafanya hizo kazi

    ReplyDelete
  3. Uwanja wa ndege wa kimataifa bado kabisaaa!!!!.

    Tunayo azma ya kukuza Utalii na Uwekezaji nchini vitu ambavyo vinahitaji zaidi hadhi na uwezo wa sio uwanja mmoja sema viwanja kadhaa vya kimataifa vya ndege nchini kwa uakisi huu hapa chini:

    1.Mzunguko wetu wa kiuchumi bado upo chini inabidi kuongeza zaidi viwanja vya ndege vya kimataifa sio tu hii Julius Nyerere Dar na Kilimanjaro Airport, inatakiwa hadi sehemu kama Geita ambapo pana mwamko na mhimili wa kiuchumi na sehemu zingine kama karibu na maeneo ya Utalii ili wageni waweze kufika direct huko,

    2.Tunaingia ktk Ushindani wa eneo la Afrika ya Mashariki tusije pigwa bao na wenzetu kuwa na viwanja zaidi vya ndege vya kimataifa ni muhimu ili kuvuta Utalii na Uwekezaji nchini.

    ReplyDelete
  4. Huo uwanja ambao hata ku-replace light bulbs mmeshindwa? Yaani uwanja wa kimataifa bulbs zinamulika mulika kama radi kwavile zimeungua na nyingine zimekufa. Halafu some ceiling boards zinaanguka na nyingine zimening'inia unaona nyaya kila mahali...!!

    ReplyDelete
  5. Jamani haya mabilioni ya Ufisadi kuwaachia watu na familia zao wakala, na kuwafunga kwa vifungo vya miaka miwili si bora tunge
    yazamisha ktk vitu kama viwanja vya ndege vya kimataifa?

    ReplyDelete

Hii ni Blog ya Watanzania popote walipo duniani kwa ajili ya kuhabarisha, kutoa/kupokea taarifa na kuelimisha mambo yote yaliyo chanya kwa Taifa letu. Tafadhali sana unapotoa maoni usichafue hali ya hewa wala usijeruhi hisia za mtu/watu. Kuwa mstaarabu...