Kama ningechaguliwa Rais wa Jamhuri ya Muungano wa Tanzania ningefanya mambo yafuatayo:
o Wizara ya Nyumba, Ardhi na Ustawi wa Jamii
o Wizara ya Miji na Maendeleo ya Miji
o Wizara ya Ajira na Pension
o Wizara ya Uchukuzi na Miundo Mbinu
o Wizara ya Biashara na viwanda
o Wizara ya Uchumi na Mipango
o Wizara ya Mambo ya Nje, Ushirikiano wa Kimataifa Baina ya Tanzania na Nchi za Kigeni na Diaspora
o Wizara ya Mambo ya Umoja wa Mataifa na Mashirika ya Kimataifa
o Wizara ya Serikali za Mitaa na Uongozi bora
o Wizara ya Mambo ya Ndani, raia, mipaka na Usalama wa Taifa
o Wizara ya Ulinzi
o Wizara ya Ushuru na Uhakiki wa Mahesabu ya Serikali
o Wizara ya Sheria, Haki na Katiba
o Wizara ya Jumuiya ya Afrika Mashariki na SADC
o Wizara ya Elimu na ufundi(itajumuisha elimu ya juu na chini)
o Wizara ya Masuala ya watoto, kinamama, vijana na wazee
o Wizara ya Afya
o Wizara ya Madini na Nishati
o Wizara ya Chakula, Kilimo, Uvuvi na Vyama vya Ushirika
o Wizara ya Sayansi na Teknolojia
o Wizara ya Habari, Siasa na Propaganda za serikali
o Wizara Maalumu kwa Masuala ya Wananchi, Bunge, Serikali na Vyombo vya kutetea Haki.
Sababu ya kutoa mpangilio huu wa wizara ni kuwa, wizara za sasa zinabidi kubadilika kwa kuwa zinaacha mambo mengi ya msingi nje.
By Anonymous


Hivi wewe, una akili timamu kweli! Wizara 22 za nini? Kweli hufai kuwa rais hata kwa dakika 1
ReplyDeleteMHE. RAISI WA KUFIKIRIKA:
ReplyDeleteBado Serikali yako ina Wizara nyingi mno!.
1.Itambulike kuwa wingi wa wizara ndio uakisi wa matumizi ya Serikali licha ya ufanisi.
2.Pia kwa vile nchi nyingi zilizoendelea zina jitahidi siku hadi siku kubana matumizi zaidi mfano kuwa na idadi ndogo ya Balozi zake nje.
3.Wizara ya FEDHA ni Wizara nyeti sana kwa Serikali na ndio Mhimili mkuu wa uendeshaji wewe hujaiweka kwa vile ADMINISTRATION inaenda sambamba na FINANCE.
4.Nchi nyingi zilizoendelea au zisizoendelea zinazotaka ufanisi unakuta zinakuwa na Wizara kama 14 tu mfano MAREKANI na RWANDA.
wewe ndio bureee kabisa, mawizara yote hayo ya nini na nchi yetu ya kimasikini,Nilijua tunazungumzia kupunguza matumizi wewe bado unatujazia tena ma wizara!!!!! agrrrrrrrrrrrrrrrrrrrrrrrrrrr!!!
ReplyDeleteumejitahidi mdau lakini sioni tofauti na ukubwa wa wizara zililopo sasa. ila kimsingi naona umelenga mambo machache tuu ambayo yanakukera binafsi na ukahisi uyaweke kiwizara. wizara 22 sio mchezo wakati wenzako wanafikiria kuwa na jumala ya wizara zisizozidi 15 wewe uko 22 duuuuuh, wake up blazaaa
ReplyDeleteNa wewe naona hutatufaa kwa sababu wizara zako bado ni utitiri hiyo hela ya kuendesha wizara zote hizo utazitoa wapi.
ReplyDeleteHongera kwa wazo lako la kuanzisha mjadala huu kusudi ifike mahali tukubaliane ni wizara ngapi tuwe nazo na zifanye nini badala ya wizara kuanzishwa ili watu fulani wapate uwaziri yaani wizara inaanzishwa kumlenga mtu? Hii ni hatari.
Kwa hiyo wewe Michezo na utamaduni hautaki ?
ReplyDeleteUngeongeza wizara ya fedha kwenye wizara ya mipango na uchumi ni hilo tuu
ReplyDeleteHahhahahahahah I need a laugh early in the morning and this helped.
ReplyDeleteThey say you are a slave to the words you say and master to the ones you don't say. In this case the Utopian President is a slave to his keyboard. Happy New Year all and may God save us from such potential presidents.
hahahahahahaha
Mi mdau namuelewa. Inabidi kweli wizara zilizopo ziangaliwe upya. Uwingi au uchache wa wizara si jambo la kusumbua kwa sababu, si kweli kwamba upungufu wa wizara ni ubanaji wa matumizi kwa sababu ukipunguza wizara unaunda institutions za kuendeleza kile ulichokipunguza katika wizara. Hivyo si kweli kwamba matumizi yanapungua maradufu ukipunguza wizara. Halafu, si haki kuilinganisha Tanzania na Rwanda au Tanzania na Marekani kwa sababu Rwanda ni ndogo hivyo haitahitaji wizara nyingi. Marekani ni Kubwa sana na ina serikali kuu yaani Federal na serikali ndogo Hamsini. Hivyo si kweli kwamba Marekani ina wizara chache kwa sababu kila state bado ina wizara zake. Halafu sisi mikoa yetu haina wizara au mabunge kama ilivyo Marekani. Tujifunze kutengeneza mambo yetu bila kuiga. Angalia Serikali mpya iliyoundwa kufufua uchumi wa Italy, Ina wizara nyingi. Na Italy ni nchi ndogo kieneo kuliko Tanzania.
ReplyDeletehizi ni dalili za kushiba McDonald...sisi tuliopo nje tunadhani na kujifanya tuna akili kuliko na wale wote waliopo Tanzania kwa sasa ni mahayawani...nilipo ona Diaspora nikajua huyu ni mpiga BOX kashiba...hahahahaha jamani tulio nje tusifikiri Watanzania waliopo nyumbani ni mahayawani...sasa Wizara zote hizo za nini na title nyingine hata hazieleweki!
ReplyDeleteduuuu!!!??? unatania au upo serious.
ReplyDeleteBajeti yako itakuwa kuudumia wizara tu, wengine wajijue. Ndo maana unatakiwa kuwa na washauri ila marais wengi wakiafrika wanakataa ushauri. ila wewe unaweza kukubali ndio maana ukalileta hapa lijadiliwe. Basi tangeneza wizara si zaidi ya 15.
Mdau kajitahidi. Inabidi tuangalie wizara zetu zinakaaje. Kubana matumizi kuzuli lakini tuangalie wapi na lini? Mapato ya serikali yameongezeka sana. Je tunahitaji wizara ngapi? Mdau hongera kwa kutoa hoja.
ReplyDeletemichezo na utamaduni wewe aaahh
ReplyDeleteNa wewe sijui umewalenga kina nani ili wapate uwaziri? Wizara zote hizo za nini, hata kama kuna wizara nyeti umeacha.
ReplyDeleteRais wa kufikirika hongera kwa mawazo hayo ila unakazi sana ya kuziendesha wizara. Uwingi wa wizara namna hii ndipo pale unapolazimika kuwapa jamaa, ndugu au washikaji zako ili wakuendeshe puta.
Kama ni kwa fikra hizo, usijaribu hata kuomba huo URAHISI maana siyo Urais, hautufai kabisaaaaaaaaaa.
wewe hutufai, huo ni uchafu ni bora wizara za JK
ReplyDeleteMdau wa tisa Mi mdau namuelewa:
ReplyDeleteAnonymous wa Wed Dec 28,09:10:00 AM 2011
Kuwa na ngo'mbe wengi sio kigezo cha utajiri!
Unaweza kuwa na ngómbe 100 wasio bora ukapata lita 30 za maziwa kwa siku, mwingine akawa na ngómbe 10 bora akapata lita 60 za maziwa kwa siku!.
BARAZA KUBWA LA MAWAZIRI ,NI MWENENDO WA KISIASA KWA KUTOA AJIRA NGAZI ZA JUU ZAIDI KWA WADAU(SIO NGAZI ZA CHINI).
Uendeshaji wa Serikali ni ule ule bila kujali ukubwa wa nchi!
Mfano uendeshaji wa Benki Kuu kwa nchi hautofautiani kwa kanuni kati ya Rwanda,Tanzania,Marekani na nchi zinginezo.
Je kuna tofauti kati ya Upasuaji wa Panya na Upasuaji wa Binaadamu?,,,mbona Madaktari Wanafunzi wanajifinzia kwa panya kwanza?
Kanuni za kuu za Msingi za kuendesha genge la Dagaa ni tofauti na kanuni za kuendesha Benki au Kiwanda?
Angalia Uteuzi wa Katibu Mkuu mpya wa Jumuia ya Afrika ya Mashariki (EAC) umemweka aliyekuwa Waziri wa Afya wa Rwanda Dr. Patrick Sezibera, sasa kama alikuwa Waziri wa Nchi ndogo kama Rwanda atawezaje kuongoza eneo la nchi 5 ikiwemo Rwanda yenyewe, Burundi,Uganda,Kenya na Tanzania?
Mimi nikiwa rais nitaunda wizara moja muhimu. Wizara ya kuchapa viboko watu wanaoota ndoto za mchana.
ReplyDeleteKuna wizara ambazo zingeweza kuunganishwa na kupunguza uwingi wa wizara hizo kwa mfano Wizara ya Ulinzi kuunganishwa na Wizara ya mambo ya ndani, wizara ya ushuru na uhakiki wa mahesabu ya serikali kuunganishwa na wizara ya uchumi na mipango n.k. Hii ingepunguza utitiri wa wizara zako Rais wetu wa kufikirika.
ReplyDeleteSafi sana.
ReplyDeleteyou would have been the first anonymous president bro !
ReplyDeleteyale yale mdau ametoa mawazo lakini watu wanajibu kwajazaba bila ya kutoa point za maana. Tubadilike watanzania..
ReplyDeletekitu ambacho kinaua ni financial kungekua na wizara 1 tu inayodili na pesa za wizara zote
ReplyDeleteHaya, tuseme sawa kwa kuwa ni mawazo yako! Tangaza na mawaziri tuone!
ReplyDeleteNingekuwa raisi wa kufikirika ningeunda wizara KUMI tu. Nazo ni hizi:
ReplyDelete(1) Wizara ya Mambo ya ndani
(2) Wizara ya mambo ya nje na ushikiano wa majirani na nchi za kimataifa (EAST AFRICA etc inaondoka)
(3) Wizara ya Ulinzi na JKT
(4) Wizara ya Fedha, Uchumi na Mipango
(5) Wizara ya Mambo ya Jamii (disasters; bunge; michezo; utamaduni; etc)
(6)Wizara ya Science, Technology Education (kindergatten, middle, secondary and hgher education)
(7) Department of Agriculture, Fisheries and Natural Resources
(8) Wizara ya Nishati, Maji
(9) Wizara ya Maswala Mazito Ya Kijamii (disasters; environment; Ajira ya vijana; Retirement za wazee
(10) Wizara ya Afya
No deputy ministers, but PS's (watumishi tuuu)!!
Rais Mtarajiawa, 2016
Wewe unafikiri kila matatizo yanaundiwa wizara kalaga bao
ReplyDeletemimi ningeweka wizara chache tu na nyingine zitakuwa ndani ya serikali za mitaa serikali kuu kutakuwa na wizara ya fedha,wizara ya ulinzi ,wizara ya mambo ya ndani na wizara ya mambo ya nje lakini wizara nyingine zitakuwa katika kila mkoa chini ya serikali za mikoa zitakuwa sawa na maofisa wa serikali za mikoa
ReplyDeletepumba tupu....hamna kitu kabisa wewe...hun tofaut na waliounda wizara ya sasa....hata hivyo let me stress something that...kupunguza wizara sio njia peke ya kucontrol matumizi...Kama tukiweza kuzui upoteu wa pesa na matumizi mabaya ya pesa kwenye wizara tulizonazo ni jambo la mbolea zaidi ya kupunguza wizara...lets work on reducing matumizi mabaya ya wizara kabla ya kufkiria mengine.....
ReplyDeleteMbona umesahau wizard ya kinababa
ReplyDeleteukiwa rais itabidi kwanza ukatibiwe...hatuendi hivi
ReplyDeleteYAANI WEWE MICHEZO KWAKO OUT,HAKI ZA BINADAMU OUT,UTALII,SANAA,. NENDA TENA SHULE
ReplyDeleteMdau hongera. Ni kweli Wizara zilizotajwa kama ni nyingi zitaongeza ajira kwa Watanzania. Watanzania wanalia hawana ajira. Hazitaongeza tu ajira bali itabidi serikali itumie intelligence kubuni miradi ya kuziendesha wizara hizi. Mi namuelewa mdau na wale wote walioguswa na kutoa matusi katika comments zao. Wengi wao wako serikalini ndio maana hata lugha yao ni ya matusi ili kumuaibisha mdau. Lakini ukweli uko pale pale kwamba Tanzania bado hatujajenga utamaduni wa kupokea mawazo na kujadili mawazo kiutaalamu bila matusi. Hili ni jambo la aibu kwa watoa maoni yenye kuchafua lugha. Hongera mdau, umeleta mada tutaijadili. Naelewa kabisa kuwa Mdau hana matatizo na Serikali ya JK ila anatoa tu mawazo akiangalia mbali. Hii si shida bali ni kupanuana kimawazo.
ReplyDeleteSuala la nipotism yaani kuwapa rafiki au watu unaowafahamu uwaziri lipo kila nchi. Hivyo nadhani Mdau anaweza kabisa akafanya hivyo akitaka. Mdau uliyetoa komenti ya "slave" hapo juu hata wewe ni "slave" kwa sababu wote hapa wametumia lugha ya Taifa ila wewe peke yako umetumia lugha ya kimombo. Wewe ndio slave haswa kwa sababu hata unaona aibu kuchangia mada katika lugha yako ya taifa! Hahahaha!
ReplyDeleteAshukuriwe mola wewe si raisi wetu. Na itafaa zaidi kama tukijua jina lako ili tuhakikishe huji kugombani uraisi huko mbeleni. Wizara 22 za nini?
ReplyDeleteWizara ya Michezo yaweza kwenda kwenye Wizara ya Habari. Ila Wizara ya Michezo imekuwa kero kwa Wananchi kwa sababu, kwenye Michezo tupo nyuma siku nenda, siku rudi. Watanzania wengi wamekerwa ndio maana wanazomea hata timu yao ya taifa. Mambo ya Fedha yatashughulikiwa na Wizara ya Uchumi.
ReplyDeleteAsante sana wadau waliotoa mawazo ya kujenga. Niliandika hii article ili kuona Wananchi wana mawazo gani. Nimegunfdua kuwa hawataki wizara nyingi.
Nimegundua vilevile wachangiaji wengi wa maoni hutoa matusi tu badala ya kutoa hoja mbadala au hoja za kustimulate akili kwa midahalo inayojenga ubunifu na hali ya kutaka kutoa maoni ya kujenga nchi. Ni asilimia chache ya wachangiaji hoja hutoa hoja zisizo za kashfa na matusi.
Niliandika hoja hii kutaka kupata maoni tu. Lakini naona lugha za kejeli na kebeli zimejaa. Nawashukuru wote ila kwa wale wasio na lugha nzuri, ni bora usome habari na husitoe hoja. Matusi yanamaanisha uwezo wa kufikiri umefika kikomo hivyo lazima mtu atukane.
Nawapongeza vile vile wale wasiotukana kwani wanaonyesha uelewa fika wa masuala mbalimbali. Hawa ndio wanatusaidia katika kupanuana mawazo. Asanteni.
Fikiria kwamba mimi ni rais mteule wa 2016 ninasubiri tu kuapishwa. Kabla sijaunda wizara yoyote nitajiuliza kwanza ni nani kanifikisha hapa?
ReplyDelete(1) Baba alinisomesha kwa pesa yake mwenyewe - nitamuundia wizara (awe waziri au anichagulie atakaendeleza mipango yako)
(2) Mama alinisaidia sana - na yeye wizara yake kama (1) hapo juu
++++++++++++++++++++++++++++++++
Jumla 1+2 Baba na mama wizara mbili....
(3) Shangazi, njomba, wakwe na wapwe zangu - kila mmoja wizara yake
+++++++++++++++++++++++++++++++++
Jumla 1+2+3 - Hapa tumefikia wizara kama 21 hivi
(4) Rafiki zangu wakubwa nilioenda nao shule - wanilinde katika mchanganuo na utekelezaji wa ajenda zangu. Nitachugua ishirini tu....kila mmoja na wizara yake
+++++++++++++++++++++++++++++
Jumla 1+2+3+4 Hapa zimefika wizara 34 na upuuzi...
(5) Nyumba ndogo zangu zote lazima wanufaike bwana weeeee.....(hivi nilikuwa nazo ngapi tena??)
+++++++++++++++++++++++++++++++
Jumla 1+2+3+4+5 - Hapa zimefikia wizara kama 77 hivi
(6) Walionichangishia pesa za kuendesha mnada nji nzima......
Jumla 1+2+3+4+5+6 - Hapa zinafikia kama wizara 99 na upuuzi...hivi...
(7) Wizara maalumu kwa wengineo
Jumla 1+2+3+4+5+6 Hapa zinafikia wizara 111 (na hapa bado mabalozi...)
(8) Hivi shangazi, mjomba, shemeji zangu na wifi za mke wangu nimewakumbuka au bado? - Basi ngoja niongeze wizara nyeti tatu za kuangalia majengo ya sirikali yangu
Jumla 1+2+3+4+5+6+7 Hapa jumla ni wizara 129
(9) Nimebakiza mabalozi...mke mkubwa naomba uniangalizie taratibu za kufanya uteuzi huu....
9.1 Kule kwa Obama tumweke nani? Atuangalizie marichimondi watakaosaidia tatizo la umeme?
9.2. Kule kwa malkia aende nani? Hapa karibu na nitahitaji suti kibao za kubadili? Nani anaweza kunitafutia haraka ikibidi?
9.3. Kule Jepu vipi....Nafikiri tumweke jamaa ambae anaweza kutusaidia mikataba ya magari...
9.4. Na Kanada je? Basi tufikirie gas na madini...tutakula wapi kama hatumweki mwenzetu pale?
9.5. Na kule sauzi je? Mzee mwenzangu huachii kituuu...waachie na wengine sasa...
9.6. Haya tuwapeleke nji za africa. Lakini Singapore bwana nataka mtu atakaengalia yule bwana alifika je pale.- Nitaendesha hii nji kama yule bwana nihakikishe ninafika lakini niwe na retirement yangu nzuri kule Ngorongorowood (holywood?). Na pia pale Lushotowoord. Hata ikiwezakana niweke kiota changu pale Chalinzewood!
(10) Nimemsahau nani - mtumee wale wanangu wanatakiwa wawe kwenye utumishi wa umma...lakini ngoja.Mkuu wa mkoa, wilaya au kijiji? Mmmmh....Nitalala leo nikiamka kesho niutangazie umma.
(10) Narudi nyumbani
Ni mimi raisi mteule (niliyepata asilimia 33% ya kura zote za watanzania)! Lakini si unaona nilivyo jipendelea!!
Mungu tubariki nji yetu ijae upendo na neema. Hamjui kwamba hapa kwetu ni kisiwa cha AMANI AMANI AMANI....AMANI...
Mdau wa 35 Anonymous Wed Dec 28, 09:26:00 PM 2011
ReplyDeleteWewe RAISI MTARAJIWA WA 2016 wa IDADI KUBWA YA NAMBA 1+2+3+4+5+6+7
SERIKALI YAKO ITAKUWA NI DHALIMU NA YA KIDIKTETA!
KWA SABABU UNAAHIDI KUTOA MADARAKA KWA KUWAPENDELA WAZAZI WAKO BABA, MAMA NA JAMAA ZAKO BILA KUFUATA MISINGI INAYOKUBALIKA YA KIDEMOKRASIA, UTAFIKIRI WATU WENGINE HAWAN AKILI VILE!
DUNIANI KWA SASA NCHI ZINAZOWEZA KUKUBALI UDHALIMU WA AINA HIYO ZINAPUNGUA NA INAKARIBIA KUWA HAKUNA KABISA!
ANGALIA LIKICHOMUUA KANALI GADDAFI LIBYA MOJA YA SABABU NI UPENDELEO WA MADARAKA KWA WATOTO WAKE NA JAMAA ZAKE WA KARIBU!
ONA KOREA YA KASKAZINI DIKTETA KIM IL JONG AMEANGUKA NA AMEZIKWA JANA NA TAYARI MWANAYE AMESIMIKWA URAISI!
KWA TAARIFA YAKO HII KOREA YA KASKAZINI NDIO ''FINAL REGIME'' IN THIS EARTH! SIKU ZAO ZINAHESABIKA!
(KOREA YA KASKAZINI NI DHALIMU YA MWISHO KUFUTIKA KTK USO WA DUNIA!-siku zao zinahesabika!)
HUWEZI ENDESHA NCHI KAMA MRADI BINAFSI!
NAKUSIKITIKIA EWE RAISI MTARAJIWA WA 2016 UNAOTA NDOTO ZA MWENDAWAZIMU!