Na Mohammed Mhina, wa Jeshi la Polisi Handeni
Mahakama ya Wilaya ya Handeni mkoani Tanga imewahukumu Raia 103 wa Somalia, kwenda Jela mwaka mmoja baada ya kukiri kosa la kuingia nchini kinyume cha sheria.
Mbele ya Hakimu Mkazi wa Mahakama ya Handeni Jonathan Mgongolwa, mwendesha mashitaka wa Idara ya uhamiaji wilayani humo ASP Charles Kasambula, alidai kuwa wasomali hao walikamatwa na Polisi katika maeneo mawili tofati wilayani humo wakiwa njiani kuelekea nchini Malawi bila ya kufuta taratibu za kiuhamiaji.
Watuhumiwa wote walikiri shitaka hilo na Hakimu Mgongolwa akaamru kuwahukumu kwenda Jela mwaka mmoja na kwamba mara wamalizapo kifungo chao, wasomali hao wasafirishwe kurudishwa makwao katika nchi waliotoka.
Wakati wa hukumu hiyo, Hakim Mgongolwa amesema amelazimika kutoa adhab hiyo ili iwe fundisho kwa wageni wengine wanaotaka kuingia hapa nchini kufuata taratibu na sheria zikiwemo zile za kimataifa zinazomlazimu kila mgeni kuheshimimu mipaka na taratib za nchi anayopanga kuingie ama kupitia akiwa njiani kuelekea katika taifa lingine.
Wasomali hao hao ambao wote ni waname wenye umri kati ya miaka 20 na 30, walikamatwa na Polisi wilayani Handeni mwishoni mwa wiki iliopita wakati wa operesheni maalum ijulikanayo kama funga mwaka bila uhalifu inayoendeshwa katika wilaya mbalimbali za mkoa wa Tanga tangu mwanzoni mwa mwezi Novemba mwaka huu.
Katika hata nyingine Jeshi la Polisi mkaoni Tanga limesema linafuatilia nyendo za mawakala wanaopokea wahamiaji haram na kwasafirishwa kwa magendo kwenda katika mataifa mengine.
Kamanda wa Polisi mkoani humo ACP Costantino Masawe, amesema kuwa pamoja na mawakala hao, pia Polisi inayafuatilia magri ya mizigo na madereva wanaotumika kuwasafirisha wasomali hao ili wakamata na kuwafikisha mahakamani.
Kamanda Masawe amewaomba wananchi kuendelea kutoa ushirikiano kwa Polisi ili kuwafichua wale wote wanaojihusisha na vitendo viovu vikiwemo vile vya usafirishaji haramu wa binadam.



Wasomali Wafungwa, hawa jamaa wapewe DONA NA MAHARAGE, siku ya Sikukuu wapewe Ugali na Hombo la tura (NDULELE)chakula asilia cha kabila la Kizigua la hapo Handeni hadi watoke!
ReplyDeleteWASOMALI waelewe kuwa hapa Tanzania kuna Polisi na Serikali, siyo msitu kama kwao Somalia ambako hakuna Serikali na iliyokuwa jiji la Mogadishu imekuwa kijiji huku mbung'o wakiruka huku na huko ,ngo'ombe na ngamia hadi katikati ya jiji!!!.
ReplyDeleteMungu kwa kweli anaadhibu, Wasomali na nyodo yao wamekuwa ktk dunia Watumwa?,,,(Mungu hugeuza mambo) ndio maana Wamakabila wanasema MULUNGU CHIBIDU!!!
ReplyDeleteMie ningewabana hao wanaowasaidia na kuwatoza faini kubwa sana inayoweza kulipia deportation zao. Yanini kuwaweka jela ambapo kumejaa na kuna magonjwa na tutumie kodi zetu kuwalisha mwaka mzima?
ReplyDeleteBlackmpingo
Tumefika wapi sasa tukifurahia watu wafungwe jela miaka kwa ajili ya immigration. Chuki mnayo ionesha thidi ya wasomali haitawafikisha popote.
ReplyDeleteMme sahau nyie wenyewe mnakimbilia nchi zingine kama south africa na ulaya na mna ingia kimagendo.
Hao wasomali walikuwa waki enda saouth africa kama vile nyie wabongo mnavofanya.
Chuki na wasomali haita watajirisha ..nyie bado maskin na mtaendela kuwa maskini kama kawaida tu.
Ingelikuwa rahisi na kugharimu kidogo sana kama serikali ingeliwatia katika lori na kuwarudisha somali mara moja kuliko kuwaweka jela kwa mwaka.
ReplyDeleteGharama za kuwaweka jela halafu kuwaondosha nchini ni kubwa mno, bora watimuliwe mara moja.
HAWA JAMAA WALITAKA WAKAMATWE MAKUSUDI KISHA WAFUNGWE KAMA ILIVYOTOKEA,NI RAHISI KU BLEND IN OTHER CULTURE THAT WAY, KISHA WAKITOKA INAKUWA RAHISI KWANI WATAKUWA WAMEIMPROVE KISWAHILI WAKIWA JELA,KISHA WATAKUWA WAMEMAKE FRIENDS WAKIWA JELA,BAADA YAHAPO HTAWAKIRUDISHWA WAKARUDI TENA INAKUWA RAHISI KUTOKAMAMTWA NAKUISHI KAMA WATANZANIA WENGINE NA KUFANIKISHA NJAMA ZAO ZA KIJASUSI,NYIE MNAFURAHI KUWAFUNGA.Angalia uone,sikiliza na usikie,siku moja hutomjua msomali kama ni msomali baada ya kuwa fluent in swahili na kuelewa culture zetu.
ReplyDeleteMimi naona ndugu zangu bado mko nyuma sana mnashabikia kuhusu wasomali lakini mko kimya kuhusu wachina ambao wanakuja na ndege na uhamuaji haifanyi chochote kuwazuia.Wanawauzia vitu bomu kisha watafungu viwanda na kuharibu mazingira kwa kumwaga kemikali ovyo kila mahali.Hata sasa hivi angalieni hao samaki tunaoringia watatoweka wote halafu mtaanza kuagiza toka china ambao wameathiriwa na kemikali za chlorine na zinc. Mimi naona bora wasomali kuliko wachina kwani ni watu hatari sana.
ReplyDeleteHUKU NI KUKIUKA HAKI ZA BINAADAMU TANZANIA IMESAINI MKATABA WA HAKI ZA BINAADAMU , SHERIA I NASEMA RAIA YEYETO ANAYETOKA NCHI YENYE VITA NA AKIKUBALI KAMA YEYE ANASHIDA BASI LAZIMA APEWE HIFADHI YA UKIMBIZI NA KWA KUWA SISI SERIKALI HAITAKI KUHIFADHI ASINDIKIZWE HADI NCHI ALIYOTOKA AU TUMHURUMIE AENDE MBELE , NAONA SUALA LA KUMFUNGA MWAKA 1 WAKATI MFUNGWA WA BONGO SERIKALI INAMGHARAMIA SH 7000 KWA SIKU X 365 TSH 2,555,000 KWA KILA MFUNGWA MARA 103 NI TSH 263,165,000 HAKIMU KACHEMSHA IMEKULA KWETU WALIPA KODI
ReplyDeleteMm
ReplyDeletehapo ndio utagundua kuwa viongozi wa bongo kuanzia chini mpaka juu vichwa maji
ReplyDeletekuwafunga mwaka mzima na kuongeza ghalama huko jela wanaona ni ujanja
ni bora kama mdau alietangulia hapo juu kuwa wapakiwe kwenye usafiri warudishwe somalia
jambo jengine watanzania mnafurahia kukamatwa kwa wasomali mbona warundi wamejaa na serikali ipo kimya
huyo kamanda anashindwa kushirikiana na raia kupambana na majambazi anaona kukamata wakimbizi na kuwafunga ndio jambo la maana
ulisikia wapi wakimbizi wanafungwa?
shame on u masawe una matatizo ya udini unatakiwa kupewa adabu na hao jamaa wamekusoma subiri ndugu zao wakutie adabu
mkimbizi anakimbia nchi yake anafikia kukamatwa na kufungwa roho mbovu sana hata huyo yesu wako hakubali roho kama yako
Mimi nikiwa mtanzania mwenye asili ya kisomali.kwanza kabisa napenda kutoa shukrani zangu za thati kwa serikali ya tanzania.,kwani nimepata elimu ya msingi mpaka kidatu cha sita biła malipo. Pili nakumbuka kabisa ya kwamba bibi yangu mza mama aligombea uhuru wa tanzania.aliuunga mkono azimio la arusha mwaka wa 1967, kwa kutembea kwa miguu akiwemo,hayati baba wa taifa,kutoka arusha mpaka USA river .pili kulikuwemo na watanzania wenye asili ya kisomali ambao walishika wathifa tefauti serikalini, kwa mfano, ndugu kinana,hayati hassan diria,na wengineo wengi tu. Lazima tukubaliane yakwamba, wasomali ni homogin society kama vile wahindi na waarabu,ni society za wenyewe kwa wenyewe katika nchi zao.sisi watanzania tumekua na matabaka tofauti . Ujamaa na kujitegemea yalitufunza mambo mengi sana.Tanzania ni nchi ambayo inayo
ReplyDeleteheshimika sana Hapa Afrika na duniani kwa ujumla,tumewapokea wakimbizi wengi tu,kutoka ,Rwanda,burundi,msumbiji,Afrika ya kusini,somalia. watanzania kwa ujumla ni watu wakarimu,wanajali sana utu na ubinadamu.Basi sio vizuri kuweka uhasama na chuki,na kutukana taifa zima, na ndani yake kuna wazuri na wabaya
GHARAMA YA KUWAHUDUMIA WAFUNGWA 103 WA KISOMALI:::::TSHS. MILLIONI 263,165,000/=
ReplyDeleteMdau Mtoa Maoni Anonymous wa Thu Dec 29, 02:20:00PM 2011
SASA ANGALIA MCHANGO WAKO WA KUTATHIMINI GHARAMA NI MKUBWA NA KAMA NINGEKUWA WAZIRI WA MAMBO YA NDANI NINGEKUPA KAZI KUWA MCHUMI WA MAHAKAMA!
HATA HIVYO HILI INABIDI KWA NGUVU ZOTE LIFIKE NGAZI ZA JUU KUNAKO HUSIKA ILI LISHUGHULIKIWE, KWA KUWA HATUWEZI KUWAGHARIMU WALIPA KODI KWA HILO!.
KWA KUWA MAGEREZA NI SEHEMU YA UZALISHAJI NA SIO KUWALISHA WATU BURE, KAMA TATHIMINI YA GHARAMA IMEFANYIKA ,,,TATHMINI YA PILI INATAKIWA YA ''HUMAN RESOURCE'' KUTAMBUA HAWA WASOMALI WANA TAALUMA GANI ILI WAPEWE MZIGO WA KAZI (WORK LOAD) KULINGANA NA TAALUMA ZAO HUKU TUKIZINGATIA GHARAMA HIYO TSHS. 263.1 MILLIONI ILIPWE KWA KAZI ZAO NA FAIDA JUU!
KAMA ITAKOSEKANA HAWANA TAALUMA, WASIWE WAFUNGWA WA KULA BURE HANDENI,WAPELEKWE MAGEREZA YA UZALISHAJI, INABIDI TUWABEBESHE ZEGE KTK UJENZI WAJENGE MIRADI YA BARABARA,MABWAWA NA RELI,WAFYATUE MATOFALI AU WAKACHANE MBAO TABORA MPAKA WALIPE GHARAMA HIYO NA FAIDA JUU!
TANZANIA KAMWE HATUWEZI ENDESHA MAMBO KWA UCHUMI WA HASARA!
Mdau wa 12 Mzalendo mwenye asili ya Kisomali.
ReplyDeleteAhsante kwa maoni na pole kwa maumivu ya kusononeshwa kutokana na ndugu zako katika asili kwa yaliyowakuta.
Anonymous wa Thu Dec 29, 01:40:00 PM 2011
TAFADHALI JIHESABU WEWE KUWA MWANANCHI KAMILI MTANZANIA MZALENDO CHUKULIA ADHABU YA KIFUNGO CHA WASOMALI 103 WASAFIRI HARAMU ILIYOTOLEWA NA MAHAKAMA TANZANIA KUWA NI SEHEMU YA UTENDAJI HALALI NA SIO UKANDAMIZAJI!
AHSANTE!
Kwanza tangu lini uhamiaji haramu ikawa ni kosa la jinai (felony)? Mtu hawezi kufungwa Tanzania kwa kosa hili, isipokuwa kama hatopewa mwanasheria wa kumtetea.
ReplyDeleteMdau Anonymous Thu Dec 29,05:41:00 PM 2011
ReplyDeleteSasa Sheria hiyo unaitoa wapi Mbona sasa wamefungwa?
Sheria hizo unazosema ni zile zile zinazoenda na Misingi ya Haki za Binaadam huko Ulaya na Marekani, lakini kwa watu wengine lakini wao wenyewe US na EUROPE wanazikiuka!
Wewe zamia US AU UK au EURO yeyote kihasara hasara uone kama hutafungwa na ukitoka RE PATRIATION HUKU BONGO UNAFIKIA GEREZANI TENA!
Hapa BONGO NI KAMA HIVYO PILATO ANAKUKUNGÚTA ''NYUNDO'' ZA NGUVU KICHWANI!
katika haki za binaadamu raia yoyote yule ukimkamata kwenye nchi yako akiwa kama mzamiaji na akidai ukimbizi nchi yatulazima imsikilize na kumhudumia hadi maamuzi yakapatikana , hapa kuna watu ambao hawajuwi haki za binaadamu , hairuhusiwi hata kuoneshwa kwenye TV hawa ni wakimbizi nchi yao inavita haikaliki ,mimi kinachoniuma ni hizi gharama tunazobebeshwa sh million 270 za kuwahudumia wananchi hawa ni nyingi sana kwa taifa langu , itakuwa ni rahisi kuwapeleka na karandinga hadi somalia kuliko kuwafunga na kuitia serikali hasara , mahakimu wanatakiwa wasomeshwe uchumi , leo ati mwanmke kamtukana shoga yake anapelekwa jela miezi 6 , mpeleke hospital akasafishe vyoo miezi 3 atapata adabu na taifa litapata faida
ReplyDelete