Mwenyekiti wa halmashauri ya wilaya ya Namtumbo mkoani Ruvuma,Steven Nana akizungumza wakati wa kikao cha baraza la madiwani wa halmashauri hiyo jana (hawapo pichani) ambapo kwa pamoja waliadhimia kuwafukuza watumishi watatu wa halmashauri hiyo.
Mkuu wa wilaya ya Songea mkoani Ruvuma,Savery Maketta akifungua kikao cha baraza la madiwani wa halmashauri hiyo jana mjini namtumbo.
Diwani wa kata ya Mkongo,Bw Danny Nyambo akitoa taarifa juu ya matatizo ya watumishi watatu wa halmashauri hiyo na kushindwa kwao kuwajibika ipasavyo ambapo pia alipendekeza watumishi hao kufukuzwa kazi kwa manufaa ya halmashauri yao.
Mkurugenzi wa halmashauri ya wilaya ya Namtumbo mkoani Ruvuma Bw Mussa Zungiza akitoa taarifa mbalimbali ya halmashauri hiyo kwa wajumbe wa baraza la madiwani mjini Natumbo jana.
Mwanasheria wa halmashauri ya wilaya ya namtumbo Ruvuma Davis Mbembela akifafanua sheria mbalimbali kwa madiwani wa halmashauri hiyo wakati wa kikao cha baraza la madiwani kilichofanyika jana mjini humo.
Baadhi ya madiwani wa halmshauri ya wilaya ya namtumbo wakiteta jambo kabla ya kuwafukuza watumishi watatu wa halmashauri hiyo kutokana na kushindwa kuwajibika ipasavyo.Picha na Muhidin Amri.

Michuzi Blog

Tanzanian blog operating since 2005, covering International news and Local News, including Politics, Fashion, Social Scenes, Interviews, Movies, Events, personalities and anything positive happening worldwide. Written in Swahili and English targeting both Swahili and English readers.

Toa Maoni Yako:

Kuna Maoni 5 mpaka sasa

  1. kama mavazi yenyewe ndio haya basi hata Udiwani wakupewa sitaki. Nilikuwa nataka kugombania udiwani Kata yangu but I changed my mind. Yaani joto lote ukanivalishe hayo madubwasha halafu hata mshahara sipewi!!!

    ReplyDelete
  2. sasa hilo ndio vazi la taifanganyika au vipi duu si mchezo

    ReplyDelete
  3. Madiwani wana majukumu gani katika jamii? Hawatuwakilishi wananchi sehemu yoyote zaidi ya vikaoni kwao. Matatizo ya kijamii huwa tunayafikisha kwa wabunge ambao wanayawakilisha bungeni sasa hawa watu wana kazi gani? Hivi vyeo vingine bwana.
    Naomba jibu.

    ReplyDelete
  4. Hivi hawa madiwani kuna ulazima gani wa kuvaa hivi viremba viremba vyao?............USELESS KABISA

    ReplyDelete
  5. HAWA MADIWANI WAMESOMEA WAPI SHERIA ZA USALAMA KAZINI HADI WAKAE VIKAO VYA KUJADILI KUFUKUZA WATUMISHI?(STANDING ORDERS)

    ReplyDelete

Hii ni Blog ya Watanzania popote walipo duniani kwa ajili ya kuhabarisha, kutoa/kupokea taarifa na kuelimisha mambo yote yaliyo chanya kwa Taifa letu. Tafadhali sana unapotoa maoni usichafue hali ya hewa wala usijeruhi hisia za mtu/watu. Kuwa mstaarabu...