Mkurugenzi Mkuu wa Shirika la Taifa la Hifadhi ya Jamii (NSSF), Dk. Ramadhan Dau (kushoto), akibadilishana hati za makubaliano na Mkurugenzi Mtendaji wa Kampuni ya Ujenzi ya  China Railway Engineering Group Co. Limited, Shi Yuan baada ya kutiliana saini mkataba wa ujenzi wa Daraja la Kigamboni, Dar es Salaam . Wanaoshuhudia ni Waziri wa Ujenzi, Dk. John Magufuli (wa pili kushoto), Mkuu wa Mkoa wa Dar es Salaam, Said Sadick (katikati) na Waziri wa Kazi na Ajira, Gaudentia Kabaka. (PICHA NA RICHARD MWAIKENDA

Dk. Dau akitiliana saini na Mkurugenzi Mtendaji wa Kampuni itakayojenga daraja la Kigamboni, Dar es Salaam, Shi Yuan

Wakibadilishana hati za mkataba huo

Waziri wa Kazi na Ajira, Kabaka akihutubia wakati wa hafla hiyo

Mwenyekiti wa Bodi ya NSSF, Abubakar Rajab, akitoa shukrani kwa Serikali

Wakiwa katika picha ya pamoja baada kusaini mktaba


 Dk. Dau akipongezwa na Mkuu wa Mkoa wa Dar es Salalaa, Said Sadick
 Waziri wa Ujenzi akijadiliana jambo na Mtangazaji wa Radio Clouds, Ephrahim  Kibonde 'Mnyambala' aliyekuwa MC wa hafla hiyo
                                     Magufuli akiwa katika picha ya moja na baadhi ya wapigapicha za habari. Picha na Kamanda wa Matukio

Michuzi Blog

Tanzanian blog operating since 2005, covering International news and Local News, including Politics, Fashion, Social Scenes, Interviews, Movies, Events, personalities and anything positive happening worldwide. Written in Swahili and English targeting both Swahili and English readers.

Toa Maoni Yako:

Kuna Maoni 43 mpaka sasa

  1. mh magufuli ni jembe wachane tu hao wanasiasa sisi hatutaki siasa ukweli zinaumiza sana taifa wanakuja na hoja zao zisizo na suluhisho kulumbana tu kila siku ukweli wana tu boa piga kazi mzee wa kazi achana nao hao

    ReplyDelete
  2. hii project ikimalika itatujengea sifa Tanzania kua na daraja kama hili..wachina walijenga daraja la manzese watu wanafanyia biashara na kupiga picha sasa sijui hili likikamilika wabongo tutajisikia vipi...najua wachina hawana longo longo wao ni kazi tu ila sasa wasije wakalipua kama wanavyolipua barabara ikawa balaa..

    ReplyDelete
  3. huyu ndiye mtu tunayemhitaji,hongera mh, magurufu,tupo tayari kwa kampeni ya urais wewe ndiye mtu unayemfuata mh, kikwete mtu muhimu sana ,hongera sana tupo na wewe hatukuachi nyuma mzee wetu,bega kwa bega

    ReplyDelete
  4. mimi ningeshangaa sana kama kampuni nyingine zaidi ya hii ya CREG ya kichina, ukweli kihalali ni ngumu kushindana na kampuni za kichina kwa gharama. lakini angalizo serikali na mteja (NSSF)wawe makini sana na wahakikishe wanamlipa vizuri consultant engineer wa kuwasimamia viwango vinginevyo yaweza kuwa kitimutimu. hawa jamaa wako vizuri kwenye kujenga kufuatana na muda ila wakati mwingine ni walipuaji wazuri tu haswa tukilala usingizi. lakini kwa kuwa tutakuwa na jembe maghufuli bila shaka atafanya kazi vizuri na wenye mradi (NSSF) kuhakikisha hayafanyiki yale ya barabara ya kilwa

    ReplyDelete
  5. KAZI YA DR DAU SIO MAGUFURI KAKAAA PONGEZI NI KWA DR DAU..HIYO PROJECT MAGUFURI ALIIKUTA MEZANI KABLA HAJAWA WAZARI..

    ReplyDelete
  6. Hawa ndo viongozi tunaowataka ahsante sanaa mheshimiwa Dau ndiyo shirika pekee la tz ambalo linasukuma maendeleo ya taifa. Yani kila nikitazama kila kona ya maendeleo nchini ni NSSF tuu

    MDAU MKELEKETWA na MZALENDO

    ReplyDelete
  7. Bigup NSSF kwa kudhamini hii project itatujengea jina sana Tanzania yani napenda sana uongozi wa Mheshimiwa Dau ndani ya NSSF mana jamaa wanajihusisha na mambo mengi saana katika maendeleo km nyumba,majengo n.k. Ni changamoto kwa taasisi nyingine kuchangia maendeleo ya nchi

    MDAU UGHAIBUNI

    ReplyDelete
  8. Hongera kamanda Dr.Dau kwa utumishi wako uliotukuka.Umefanya kazi kubwa sana ndani ya Nssf.Daraja hili ni ukombozi wa Watanzania wote halina tofauti na Daraja kubwa la hapa UK la Dartford Bridge.Ni fahari kwa Tanzania yetu.

    Mwenyezi Mungu akulinde na kila shari pamoja na maadui wasiokutakia mema.

    Mdau Baba K.
    London.UK

    ReplyDelete
  9. Magufuli, kama ni kushambuliwa ashambuliwe na asasi za wanaharakati. Vyama vya siasa vinavyomshambulia vinajitia kitanzi, kikiwemo cha kwake mwenyewe.

    ReplyDelete
  10. Aisee mnamchelewesha Dr. Magufuli, picha kwake za nini???

    ReplyDelete
  11. Hongera Dr. Dau ama kweli wewe ni mtu wa Vitendo si maneno.Nashangaa leo ni siku ya furaha kama hii wenzetu kule Jamii Forum ndio imekuwa siku ya kuishambulia Nssf.

    Watu hawa ni sawa na yule bwana aliyeambiwa ukiomba kitu kizuri kwa mwenzio basi nawe Mwenyezi Mungu anakuzidishia mara mbili,yuko jamaa badala ya kuomba heri akaomba yeye atolewe jicho moja ili macho mawili ya jirani yake yatoke.masikini hakujua kuwa dua ile utatakiwa kuomba heri tu na si shari.huo ndio mwenendo wa Jf kijiwe cha kijicho na roho mbaya.

    Mdau 17.
    Mayfair-England.

    ReplyDelete
  12. Dr.Dau mpango Mzima.kula tano mpiganaji wetu.
    Chichi.
    Lewisham-Uk.

    ReplyDelete
  13. Bab kubwa kwa NSSF chini ya Dr.Ramadhan Dau.
    S.Kiliza
    Bromley.Uk.

    ReplyDelete
  14. Pongezi kwa Dk Dau na NSSF...tumeona kazi yako katika kuinvest katika sekta nyingi tanzania..watz tujivunie na mchapa kazi huyu

    Jack
    Mdau Glasgow

    ReplyDelete
  15. Ganda la muwa la jana.................

    ReplyDelete
  16. concept nisiyoielewa kwenye ukamilifu wa daraja hili, ni pale watu watakapokuwa wanatakiwa kulipia ili kupita!

    ReplyDelete
  17. Dr. Ramadhani K. Dau kweli kazi umeifanya!

    HONGERA SAAAANA, ilikuwa ni ndoto kuwa na wazo kama la kupata Daraja la kuunganisha Kigamboni!

    Lakini sasa yametimia!

    ReplyDelete
  18. Wandugu Mnyonge Mnyongeni Haki yake Mpeni,

    Haya Mashirika na Mipango inayosuasua kwa nini tusiunde Timu ya Wachapa kazi, TIMU YA MAPAMBANO /KIKOSI CHA KUFA NA KUPONA kama watu majembe 5 au 10 wakishirikiana na WAANGALIZI halafu wakapewa jukumu?
    -----------------------------------
    MASHIRIKA NA MIPANGO:
    -----------------------------------
    1.MRADI WA MABASI YAENDAYO KASI (DART)
    2.SHIRIKA LA RELI-TRL
    3.TANESCO
    4.MIRADI TATA YA UJENZI WA BARABARA
    5.TICTS-MIZIGO BANDARINI
    6.KAMATI YA MAAFA NA MAJANGA
    7.ATCL-SHIRIKA LA NDEGE
    8.MIGODI YOTE YA MADINI
    9.MALIASLI
    10.BENKI KUU
    -----------------------------------
    TIMU YA KUFA NA KUPONA/ KIKOSI CHA VITA:
    -----------------------------------
    1.JOHN P. MAGUFULI
    2.DR.RAMADHANI K. DAU
    3.LAZARO NYALANDU
    4.PROF. MARK MWANDOSYA
    5.PROF.ANNA TIBAIJUKA
    6.IGP. SAIDI MWEMA
    7.DR.HARRISON MWAKYEMBE
    8.SAMWEL SITTA
    9.NAPE NNAUYE
    10.BALOZI OMBENI SEFUE
    -----------------------------------
    WAANGALIZI:
    -----------------------------------
    1.RAISI JAKAYA M. KIKWETE
    2.UTAWALA WA UJERUMANI KUTIPIA UBALOZI WAKE NCHINI (KWA UANGALIZI NA UFIKIAJI MALENGO NA SIO UTAWALA)
    3.UBALOZI WA USWISI
    4.UBALOZI WA NORWAY
    5.WANANCHI WOTE WA TANZANIA WALIO NDANI NA NJE YA NCHI KUSHIRIKISHWA KUPITIA MIDAHALO YA NJIA YA HABARI REDIO NA TELEVISHENI YA TAIFA (LIVE). KUHUSU MCHAKATO WA MATEKELEZO.

    NAFIKIRI KWA MPANGILIO HUU NA TIMU HII NCHINI TANZANIA BAADA YA MIAKA MITATU MAMBO YATAKUWA MAMBO!

    ReplyDelete
  19. Mnampongeza Ramadhani Dau kwa kutumia pesa za wastaafu kujenga daraja wakati wastaafu wanasota pale ofisini kwake bila kupata pensheni zao kwa wakati unaostahili? Je hii ni investment kama inavyotakiwa kwa michango ya wafanyakazi kuwa invested ili wanapostaafu walipwe mafao mazuri bila usumbufu?

    Pamoja na kwamba ujenzi wa hili daraja ni muhimu sana na utatusaidia sana kuepuka kero za usafiri kigamboni lakini jamani matumizi ya pesa za wastaafu siyo haya.
    Hii nadhani inasababishwa na mapungufu ya fund managers kutojua majukumu yao vizuri au kutafuta umaarufu wa kisiasa tu. Nadhani anafanya maandalizi ya kuingia kwenye siasa kwa gharama ya michango ya wafanyakazi/wastaafu.

    ReplyDelete
  20. Kaika Orodha ya Majembe ya Tanzania KIKOSI CHA VITA/ KUFA NA KUPONA pana wengine wengi tu na hawa pia ni MUHIMU:

    1.Balozi PETER KALAGHE-UINGEREZA
    2.NEHEMIA MCHECHU-NHC/ TANZANIA

    ReplyDelete
  21. Kikosi cha vita/kufa na kupona aongezwe Bi ANANILEA NKYA atatia changamoto.

    ReplyDelete
  22. MNANICHEKESHA MNAOMPA HONGERA MAGUFULI KWA LIPI KBWA ALILOFANYA, HII PROJECT ILIKUWEPO TOKEA ENZI NA ENZI ILIKUWA INASUBIRIWA TU KUPATIKANA KWA MFADHILI! HII NI PROJECT ALIOIIBUA DOKTA DAU NA SI MAGUFULI NARUDIA SIIIII MAGUFULI !!!! msimpake kilemba ,, kuna mtu amesema GANDA LA MUA LA JANA ! NI KWELI ! HII NI KAZI YA KUSIFIWA DK DAU

    HONGERA SANA DOKTA DAU !

    ReplyDelete
  23. hongera Dr dau kwa kazi yako nzuri sana. utakuwa umesaidia sana watanzania kwa kutengeneza ajira na kuondoa usumbufu na kuokoa muda wa kusubiria pantoni

    stev- London

    ReplyDelete
  24. MICHUZI BLOG MKO BIASED, MAONI MENGI SANA YENYE UKWELI MNAYABANIA MNAOGOPA NINI? KAMA UPIGANAJI HAMUUWEZI HII KAZI ACHIENI WENGINE. KAMA NYERERE ANGEKUWA MWOGA BABA ZENU WANGEISHIA WAPI? ACHENI WOGA!!!!!

    ReplyDelete
  25. Bora waharakishe daraja hilo watu tuache kupiga mbizi wakati wa kwenda Kigamboni

    ReplyDelete
  26. BILA SHAKA HUU UTAKUWA MRADI WA MUHIMU,HASA TUKIZINGATIA MIPANGO YA KUFANYA KIGAMBONI KUWA DUBAI NDOGO.

    HIYO PICHA YA PAMOJA NIMEIPENDA. WENZETU WAWILI WAWILI SIE KIBAO. NGOJA GHARAMA ZA HII SHEREHE YA UTIAJI SAINI ZITAKAVYOKUWA KUBWA. KWANI DK MAGUFULI ANGEAMBATANA NA MAOFISA WAWILI NA DK DAU VILE VILE WAWILI HAINGENOGA?

    ReplyDelete
  27. sasa wewe usuielwa dhana ya kulipia daraja ni ipi wakati hata ughaibuni wanaotumia madaraja hulipia?

    ReplyDelete
  28. JEMBE LINGINE LA TANZANIA NI MWANAMAMA ENG.STELLA MANYANYA.

    NITARUDI BAADAYE NA ORODHA YA MAPENDEKEZO YA BARAZA LA MAWAZIRI LA WAKINA MAMA TU. MAANA WAO HAWANA LONGOLONGO MRADI WASIINGILIWE KATIKA UTENDAJI WAO NA MIDUME YENYE UCHU.

    ReplyDelete
  29. Nawapongeza kwa maadalizi ya ujenzi wa daraja , kuna wakati wakazi wa kigamboni walikuwa wanaulizwa kwamba daraja likijengwa wapo tayari kulipia wakati wa kupita katika daraja hilo? nami nauliza je katika nchi yetu hii kuna daraja linalipiwa? au wakazi wa kigamboni siyo watanzania?, wanapesa nyingi?,au ndo warudi kijijini kama walivyoambiwa kwenye kupanda pantoni? haki sawa kwa wote ipo wapi?

    ReplyDelete
  30. JAMANI TUMECHOKA MBONA MAJINA MNAYOTOA NI WALEWALE WALIOPO MADARKANI TUNATAKA MAGEUZI.

    TUNATAKA ORODHA ANGALAU YENYE MCHANGANYIKO NA MAJINA MAPYA LAKINI UTENDAJI WAO UNAELEWEKA HATA KAMA NA WACHACHE MAANA WAPO WENGI SANA KWENYE TAASISI ZETU WANAFANYA KAZI NZURI SANA HASA WANAWAKE MNAOWAJUA TUPENI MAJINA YAO JAMANI HII NI CHANGAMOTO TU LABDA ITASAIDIA.

    ReplyDelete
  31. wewe ni phd holder wa kweli kweli.hongera sana DR. dau kwa kazi hiyo na nyignine nyingi ulifanya kwa manufaa ya watanzania na tanzania. kwa kweli umesaidia kila sector muhimu. Big up DR.

    max- shephard bush-London

    ReplyDelete
  32. Taarifa ya ujenzi wa daraja la Kigamboni imekuja muda muafaka. Daraja hili litasaidia kuleta maendeleo ya haraka kwa wakazi wa Kigamboni. Hongera kwa wahusika wote.
    Faustine Ndugulile-Mbunge Kigamboni

    ReplyDelete
  33. Na mimi vile vile wa Iringa kusomea dua mradi huo ufanikishe

    ReplyDelete
  34. Mdau hapo juu,kutokulipwa pensheni kwa wastaafu au mafao yao kwa wakati si kwamba mfuko unakuwa hauna pesa, ila wastaafu ndo wanakuwa na mapungufu katika ukamilishaji wa nyaraka,hususan za ajira au uzembe wa mwajiri kwa kutokuchangia michango ya watumishi wake,uliza wadau wa mifuko ya pensheni watakwambia,sio unaongea tu,suala la investment katika mifuko huwa ni muhimu.

    ReplyDelete
  35. Hongera kaka Dau
    Justina Brian
    Kent-UK

    ReplyDelete
  36. I am thankful to the Almighty to witness this great moment in the History of my great Country ,Tanzania . I can almost see the future History books 100yrs from now..."The first major bridge in Tanzania was built by NSSF under the leadership of Dr. Dau" ....NSSF continues to be a catalyst in changing ,developing and shaping the way forward for a brighter Tanzania through its commitment to social& Country development in various projects. This is indeed another example of a great patriotic Organisation that NSSF is to Tanzania & Tanzanians ..Well done NSSF under your leadership, and God Bless.

    ReplyDelete
  37. Kweli Nssf wameamua kufanya kweli.

    ReplyDelete
  38. BIG UP R. K. DAU.
    JUHUDI ZAKO TUNAZIONA.KAMA SI WEWE THIS IDEA INGETOKA WAPI?ISSUE NI KUWA CREATIVE KWANZA THEN UFUATILIAJI.NAUNGANA NA WENGINE SI MAGUFULI WA KUPAISHWA NI JEMEDARI R.K. DAU.
    NSSF ENDELEENI KUKAMUA.

    ReplyDelete
  39. KAMANDA DAU UNAFANYA TUNAONA.HATUNA LA KUKULIPA ILA TUNATAMBUA SAAAAAAAANAAA UMUHIMU WAKO NDANI YA JAMII YA KITANZANIA.
    TUNAMSHUKURU MUNGU KWA KUJAALIA WEWE KUZALIWA NDANI YA TANZANIA NA KUWA MTANZANIA MAANA UNAYOTUFANYIA NI MAKUBWA.HIVI UNGEKUWA MKENYA MAFANIKIO HAYA WANGEYAPATA WENZETU.LAKINI TUNASHUKURU KWA WEWE KUWA MTANZANIA NA KUFANYA KAZI KWA MAENDELEO YA TAIFA LAKO.MUNGU AKULINDE MILELE.

    ReplyDelete
  40. HONGERA SAAAAANAAAA MZEE DAU.SINA LA KUSEMA ILA MUNGU BABA AKUZIDISHIE UHAI MREFU UZIDI KUTUFANYIA MENGI.
    VIONGOZI ACHENI MAKELELE YA KUTAFUTA KURA TUNATAKA WATU KAMA R. K.. DAU.
    BIG UP KWA Dr. DAU NA MAISHA MEMA YENYE BARAKA.
    MDAU JOHNSON.
    IRINGA.

    ReplyDelete
  41. Asante DR. DAU.

    Nadhani anony wa tano toka juu umefurahi.

    ReplyDelete
  42. Kule kigamboni ndiko kwenye ardhi ya Mh. Kichaka, kwa hiyo daraja hilo sio kwa ajili yetu wabongo. Hata hivyo tutanufaika kwa kupita na baiskeli zetu.
    Huu ndiyo ukweli ninaoomba bloger usiubanie.

    ReplyDelete
  43. Wabongo bwana. Kitu hakijakamilika wala hakijaanza kutengenezwa mnakenua mijino juuu. Hizi hadithi za kibongo nimeshazizoea, mtakuja sikia yale yale ya New Dar kigamboni na serikali kuhamia dodomya. Subirini muona vitu vimekamilika ndo mkenue meno.

    ReplyDelete

Hii ni Blog ya Watanzania popote walipo duniani kwa ajili ya kuhabarisha, kutoa/kupokea taarifa na kuelimisha mambo yote yaliyo chanya kwa Taifa letu. Tafadhali sana unapotoa maoni usichafue hali ya hewa wala usijeruhi hisia za mtu/watu. Kuwa mstaarabu...