YAP KUELEKEA JUMAMOSI MAMBO YOOTE YAMESHAJIPAA NGUO ZIMESHARUDISHWA TOKA DRYCLEANER , NA HAPA NDIO ZILIKUWA ZINAPANGWA KWA KUWEKWA  TAG ZA BEI. KILA NGUO ZISHAPANGIWA BEI YAKE....VIATU NAVYO VISHAANDALIWA ...TAYARI KWA KUKUUZIA...KUNA NGUO ZA KILA AINA OFISI, MTOKO ,B2A HADI ABAYA. NIWEWE TU NA CHOICE YAKO.
 NASISITIZA 
HII NI CHARITY:: NJOO UTUCHANGIE KIVYOVYOTE VILE KWA KUTUPATIA PESA CASH ,KUMNUNULIA DADA,MDOGO WAKO AU HATA RAFIKI YAKO 


MAHALI::KIKIS FASHION ,MIKOCHENI,PEMBENI YA BARCLAYS BANK NA ENGEN PETROL STATION,MIKOCHENI 
MUDA::SAA 4 ASUBUHI HADI SAA MOJA USIKU
SIKU::JUMAMOSI

                                                  VIKO TAYARI SASA
                                           NGUO TOKA DRY CLEANER
                                              VIATU VIKO TAYARI KABISA

                              HADI B2A NYENGINE HAZIJAVALIWA KABISAAA
                                             ABAYA NAZO ZIPO
                                                VIVAZI VYA MTOKO



Michuzi Blog

Tanzanian blog operating since 2005, covering International news and Local News, including Politics, Fashion, Social Scenes, Interviews, Movies, Events, personalities and anything positive happening worldwide. Written in Swahili and English targeting both Swahili and English readers.

Toa Maoni Yako:

Kuna Maoni 28 mpaka sasa

  1. Ni mitumba? Au alikuwa anazivaa Mwamvita, mbona zinatoka kwa dry cleaner?

    ReplyDelete
  2. Kwa ajili ya kuchangia nn?

    ReplyDelete
  3. eti mitumba kutoka kwa mwamvita.
    hahahhahaaaa...... wabongo bana.
    hivi huko tanzania kumbe watu washaanza kujiona ma-star namna hiyo
    yani avae halafu awauzie tena wabongo wenzane?
    diiiiiiiiiii hii kali bwana mithupu

    ReplyDelete
  4. CELEBRITY EXCESSES.

    ReplyDelete
  5. Uwe unasoma juu kwanza ni Charity inamaanisha itakuwa alikuwa anazivaa yeye anaona kwake basi ila kwa wengine zitawafaa nakuwafaa wengine hizo pesa yeye atapeleka kwenye misaada ni mfano mzuri nafikiri kwa wengine mdau UK.

    ReplyDelete
  6. naomba nikujibu mdau hapo juu kuwa hizo nguo sio kusema ni mitumba kwa mujibu wa Mwamvita mwenywe mwamvita makamba amejitolea nguo zake mwenyewe alizokuwa anazifaa ndio anaziuza na pesa itakayopatikana ni kwa ajili ya kuchangia watoto Yatima....Hongera sana Mwamvita kwa hili UMEWEZA SANA na mungu atakubariki

    ReplyDelete
  7. Ni nguo za mwamvita Alia kuwa anazivaa, nw ameamua kuuza hela isaidie charity

    ReplyDelete
  8. hivi nyinyi wanawake wa kiafrica kwanini mnapenda sana kuvaa nywele za bandia ? mimi ni mwarabu ila hupenda sana wanawake wa kiafrica wenye kuacha nywele zao za kiasili huwa nawaheshimu pia zaidi ...

    please acheni hayo mambo

    ReplyDelete
  9. Wewe vp hapo juu..hufahamu..uliza nini binadamu anafanya kwa kuwasaidia wenzake..Hizo ni nguo za bei ya juu, kwa kizungu ni designer..nyengine zimevaliwa Mara moja, zinauzwa ili atoe mchango kwa jamii..hata ulaya na India ni jambo la kawaida..atapata fedha nzuri tu hapo..well done Mwamvita..

    ReplyDelete
  10. usijali kama ni mitumba au la, wanawake kuvaliana nguo kwa kuazimana ni kitu cha kawaida, bali hapo watakuwa wanaazimana kwa pesa sio bure, la maana nenda kawaunge mkono ila kama sio jinsia ile samahani ila muhamasishe na muwezeshe wako akawaunge mkono.

    ReplyDelete
  11. Kitu kikipita dry cleaner (washing machine & detergents+ironing & heating) sayansi inatuambia hakuna bactearia anaweza stahimili atakufa tu!

    ReplyDelete
  12. Dada from Dk.January 13, 2012

    Nawapenda nyie wadada kwa moyo wenu wa upendo wa kuwafikilia wengine hiyo ni zawadi kubwa sana kuwa na moyo kama uwo.Wengi inabidi tuige mfano huu mzuri. Nawatakia shughuli amani kwa siku ya kesho.

    ReplyDelete
  13. mmh nguo ni nzuri i wish ningekuwa bongo niziwahi hongera mwamvita kwa moyo wa kujitolea

    ReplyDelete
  14. Zikivaliwa na mwamvita hawazitaki. Lakini zingekuwa zimevaliwa na wanawake wa kizungu wa paris au london wangezigombea.

    ReplyDelete
  15. my dear sisters,
    KITU MNACHO KIFANYA KAMA NI KWELI HELA ZITAWAFIKIA WALENGWA NI KIZURI SANA NA KIFANYWE MFANO WA KUIGWA NA MTU MWINGINE MWENYE VIWALO VIKALI VINAVYO UZIKA BASI NAE APELEKE MUNGU AKUBARIKI NEXT ELECTION UCHAGULIWE MBUNGE WA VITI MAALUM.BIG UP XXX

    ReplyDelete
  16. Hata late Pricess Diana alifanya hivyo!!

    ReplyDelete
  17. amefanya vizuri sana ninampenda na kumsifia sana anauelewa wa hali ya juu huyu dada hata hivyo zingine zitamkumbusha walipokua pamoja na mumewe kabla hawajatengana, bora aziuze tu.

    ReplyDelete
  18. Hongera sana Mwamviata Makamba!

    WATANZANIA ACHENI UJINGA WENU, INA MAANA MMEKUWA JUU SANA SIKU HIZI HAMVAI MITUMBA?

    Hawa wanaojikweza wana matatizo sana ukiona mtu wa mamna hiyo ni yule anayebakisha makombo ya chakula nyumbani kwake mjini wakati jirani hali yake duni anatupa jalalani kesho yake!...huku kijijini kwao nduguze wanakufa njaa!

    ReplyDelete
  19. Mwamvita Makamba ni mzuri wa sura na roho pia, Mwenyezi Mungu amzidishie!

    ReplyDelete
  20. MUNGU anapendezwa na watu wenye moyo wa kujitoa na kufikiria wengine kama Mwamvita.Kama unataka kujitolea na wewe unga mkono zoezi hili kwa kununua nguo hizo.

    ReplyDelete
  21. hayo manywele yanawafanya muonekane na mavichwa kama mijusi ya mapangoni.

    ReplyDelete
  22. Hongera Mwamvita Makamba kwa Uzuri wa Sura na Moyo na Roho!

    Mwamvita amekwisha jaaliwa na Mungu!

    Wenye wivu wajinyonge mkafie mbele na Roho mbaya zenu,,,Mwamvita ana mwanya wa juu hamjui hiyo ni siri ya uzuri?

    Pana Mwana falsafa mmoja alishawahi kuniambia kuwa alivyo mtu ni kile kilichopo ndani ya moyo wake ambacho kinaakisiwa na SURA, RAGHBA-LILE JICHO LAKE MBELE YA WENGINE, na mara nyingi mtu mwenye sura ya mvuto huwa na roho nzuri!

    Sasa ninyi waosha vinywa mnaokosoa mmetoa nguo zenu kama Mwamvita?

    Tena unaweza kukuta mwanamke anajifanya kutoa maoni ya kukosoa wakati yeye mwenyewe anashinda katika Migahawa akinywa juisi mjini hata kazi hana!

    Kalaga baho mwenzenu anafanya kazi Vodacom na ndio hivi anawajali wengine ninyi je?

    NDIO NINYI WANAWAKE MAGUBERI WA MJINI WACHEZA TAARABU MAGOMENI!

    Nyie wenye roho mbaya kazi ni kukosoa tu inawezekana hata ma house girl wenu mnawaweka maisha mabaya kuwavalisha magunia na matambara ya deki kwa roho zenu mbaya!

    ReplyDelete
  23. Madada wengi kwa kuwa na roho mbaya ndio maana mna kwama kimaisha hamfanikiwi!

    Wengi ndoa zenu na mahusiano yanaota mbawa mara kwa mara mnaishi kwa tabu, hamdumu na wanaume!

    Mjaribu kuwa na roho za huruma na imani kwa kutoa!

    Kazi yenu ni kudharau mambo ya wengine na kusema wenzenu vibaya!

    KHAAA, ANGALIENI MFANO HUU WENZENU FLAVIANA MATATA NA MWANVITA MAKAMBA HAOOO WANAFANYA VITU VYAO,,,MUNGU MJOMBA WENU AFANYE MNACHOTAKA NINYI WANAFIKI?

    MNAFIKIRI MUNGU ATAKOSA KUWABARIKI MWAMVITA NA FLAVIANA?

    ReplyDelete
  24. Wenzenu wanatoa kazi zenu mmebakia kuponda ohhh mitumba, ohhh kavaa Mwamvita!

    Kazi mmebaki kusafisha kucha, kuosha miguu na kutegemea wanaume!

    ReplyDelete
  25. eh, kumbe walishatengana na mumewe?

    ReplyDelete
  26. another trip to Dubai paid

    ReplyDelete
  27. Tuejenge utamaduni wa kuthamini jitihada za wenzetu hata kama ni ndogo kiasi gani!.

    Mwamvita Makamba na Flaviana Matata wameanza na wengine tujitahidi tujikakamue na sisi!

    Sio kutumia muda mwingi kumuanika mtu na kumpekua kimaisha hadi juu ya mahusiano na mwenza wake na mambo kadha wa kadha ambayo ,hata kama ni hivyo je wewe msemaji yanakuhusu nini?

    Mfano hapo juu Pana mtoto Mlemavu wa ngozi, ngalia watu walivyo wabaya wapo watu wanaweza angamiza maelfu ya shilingi, malaki ya shilingi hadi mamilioni kwa starehe za ajabu kabisa, je wangetoa chochote kwa watu kama huyu mtoto Albino mgonjwa kweli Mungu angekosa kuwabariki?

    ReplyDelete
  28. Tusikalie majungu na kupekuana tu kimaisha!

    Ohh analipiwa nauli ya ndege ya Dubai,,,ohhh ametengana na mwenzie!

    Ninyi mmefanya nini kitu cha angalau wema kwa jamii?

    Huku tukiiachia Serikali kufanya kila kitu!

    Mpaka angapau mchango wa chupi za watoto waliokumbwa na mafuriko Disemba 2011 tusubiri Serikali?

    ReplyDelete

Hii ni Blog ya Watanzania popote walipo duniani kwa ajili ya kuhabarisha, kutoa/kupokea taarifa na kuelimisha mambo yote yaliyo chanya kwa Taifa letu. Tafadhali sana unapotoa maoni usichafue hali ya hewa wala usijeruhi hisia za mtu/watu. Kuwa mstaarabu...