Meneja wa Mwanamuziki Charles Baba,Benard Msekwa akiongea na waandishi wa habari (hawapo pichani) leo jijini Dar es Salaam kuhusiana na mwanamuziki wake huyo kujiunga rasmi na Bendi ya Mashujaa.Kushoto ni Mkurugenzi wa Utawala wa Bendi ya Mashujaa,Yohana Mlawa.
Meneja wa Mwanamuziki Charles Baba,Benard Msekwa akionyesha bahasha kwa waandishi wa habari (hawapo pichani) yenye mkataba uliosainiwa na Mwanamuziki huyo ambao ameutuma kwa njia ya DHL.

MWANAMUZIKI wa zamani wa bendi ya African Stars wana Twanga Pepeta, Mbwana Gabriel Cyprian maarufu kwa jina la Charles Baba ametunga wimbo maalum wa kuanzia kazi katika bendi yake mpya ya Mashujaa kama sehemu ya utambulisho wake rasmi.

Meneja wa bendi hiyo, Benard Msekwa alisema kuwa wimbo huo utatambulishwa rasmi kesho Ijumaa katika onyesho maalum litakalofanyika kwenye ukumbu wa Business Park kwa kushurikiana na wanamuziki wa bendi hiyo pamoja na bendi nyingine mbili, Mapacha Watatu na Extra Bongo.

Msekwa alisema kuwa wimbo huo ni ‘suprize’ kwa mashabiki wa muziki wa dansi hapa nchini baada ya kusaini mkataba mnono wa miaka miwili.

Alisema kuwa hatua ya kutunga wimbo huo ni kuthamini kile alichokipata kutoka kwa uongozi wa Mshujaa na hasa wanatarajia kuona mambo makubwa siku ya onyesho lake. Kuhusiana na maamuzi ya kujiunga na Mashujaa, Msekwa alisema kuwa jumla ya bendi tano zilikuwepo katika mchakato wa kumwania mwanamuziki huyo katika bendi hiyo.

“Kulikuwa na bendi nyingi sana ambazo zilimtaka mwanamuziki wangu, lakini tulishindana kuhusiana na dau ambazo walizotoa,” alisema Msekwa.

Alifafanua kuwa Charles kwa sasa yupo nchini Dubai kwa mapumiziko na mkataba aliusaini akiwa huko na kuutuma kwa njia ya DHL. Aliongeza kuwa Charles anatarajiwa kuwasili nchini kesho saa 9.00 alasiri kwa ndege ya shirika la Emirates akitokea Dubai.

Mmoja wa Wakurugenzi wa bendi ya Mashujaa, Yohana Mlawa alisema kuwa wamefarijika kushinda mbio za kumchukua mwanamuziki huyo na sasa milango ya usajili wao imefungwa.

“Kama mnavyofahamu, tayari tumemchukua Charles na mwimbaji wa zamani wa bendi ya FM Academia maarufu kwa jina la Thalathin Tatu na tayari amekwenda sambamba na wanamuziki wanzake wa bendi hiyo,” alisema Mlawa.

Alisema kuwa hakuna mwanamuziki yoyote wa bendi ya Mashujaa ambaye ataondolewa katika bendi yao baada ya kuingia wanamuziki hao wawili. 

Michuzi Blog

Tanzanian blog operating since 2005, covering International news and Local News, including Politics, Fashion, Social Scenes, Interviews, Movies, Events, personalities and anything positive happening worldwide. Written in Swahili and English targeting both Swahili and English readers.

Toa Maoni Yako:

Kuna Maoni 12 mpaka sasa

  1. huko ulikokwenda siko afadhali ungeenda sikinde au msondo ndio unapotea kwenye anga ya muziki hurumaaaaaaaaaaaaa

    ReplyDelete
  2. hata km ni dau mtu unaweza ukaruka mkojo akakanyaga mavi ile bendi ni ya wazaire watupu lazima watakufunika charles huwezi kufurukuta pale

    ReplyDelete
  3. TATIZO LA WANAMUZIKA WA TANZANIA WANASUMBULIWA NA SIFA NA USHAMBA NAUNGA MKONO MCHANGIAJI WA HAPO JUU NINI ATAFANYA PALE HAYA YETU MACHO

    ReplyDelete
  4. HAYA KWENYE VICHAA UNAJINGIZA BILA KUOGOPA SI WATAKUMALIZA

    ReplyDelete
  5. ulikataa na kujitoa mapacha wa 3 bila sababu ya msingi angalia sasa hakuna mwanamuziki wa dance anawakamata mapacha 3 kwa kipato!!

    ReplyDelete
  6. Kwa level uliofikia better kuanzisha Bendi yako mwenyewe!mbona wengi wameweza wewee!...ukoje lakini grgrrrrrr!!

    ReplyDelete
  7. HIVI WEWE UNA LUKWALE?KAA!..mashujaa?kwani vita hivyo?

    ReplyDelete
  8. Mashujaa ni bendi feki kama vile Akudo impact, yaani kelele nyingi na kutaja majina ya watu wakati ujumbe ni mistari miwili tu. Charles kama utapewa uongozi ua muziki wa namna hii, watu tunataka ujumbe katika muziki wa TZ sio kutaja tu majina ya watu huu ni ukosaji maadali na si utunzi kwani mtunzi anatoa ujumbe si kuataja tu majina bila sababu.

    ReplyDelete
  9. Maskini kweli la kuvunda halina ubani. Yaani kwa akili yako kabisa ya form II, umeamua kujiunga na Wazaire ili ukapigie muziki viti???? Dogo umechemsha mbaya, tunajua utarudi tu, Twanga Kisima cha Burudani.

    Mdau HK

    ReplyDelete
  10. Chalz muweke mungu kwa kila jambo,usiogope wazaire,kazi ni popote pale,mkono uende kinywani...kama hajaona maendeleo alikokuwa mwanzo anaweza badili sehemu nyingine..riziki anapanga mungu sio binadamu..hongera sana chals baba

    ReplyDelete
  11. nenda tu ukishindwa rudi mkosa fadhila

    ReplyDelete
  12. sasa jamani mnataka anganganie sehemu moja kwani kafunga ndoa na twanga?anatafuta maslai,kwani nyie huwa hambadili kazi??ajira gani ya tanzania mnayopigia kelele hivyo??mbona watu wengi tuu wanabadili kazi??

    ReplyDelete

Hii ni Blog ya Watanzania popote walipo duniani kwa ajili ya kuhabarisha, kutoa/kupokea taarifa na kuelimisha mambo yote yaliyo chanya kwa Taifa letu. Tafadhali sana unapotoa maoni usichafue hali ya hewa wala usijeruhi hisia za mtu/watu. Kuwa mstaarabu...