Mwenyekiti Mstaafu wa CCM na  Rais Mstaafu Mh. Benjamin Mkapa akilakiwa na Katibu Mkuu wa CCM, Mh. Wilson Mukama alipowasili leo Uwanja wa Ndege wa Julius Nyerere jijini Dar es Salaam, akitoka Afrika Kusini ambako alimuwakilisha Rais Jakaya Kikwete katika maadhimisho ya miaka 100 ya chama cha ANC. Kati niu Mama Anna Mkapa.

Michuzi Blog

Tanzanian blog operating since 2005, covering International news and Local News, including Politics, Fashion, Social Scenes, Interviews, Movies, Events, personalities and anything positive happening worldwide. Written in Swahili and English targeting both Swahili and English readers.

Toa Maoni Yako:

Kuna Maoni 11 mpaka sasa

  1. Tanzania bwana! Mungu aendelee kuibariki. Unaona Rais Kikwete hana shida na waliomtangulia. I hope this tradition continues. Jamuhuri yetu inaendelea kukomaa!

    ReplyDelete
  2. Kweli kabisa. Huwezi kuona zambia au malawi wakifanya hivyo. Hata kenya hawafanyi hayo. We are unique bwana

    ReplyDelete
  3. Ni kweli mdau wa kwanza hivyo ndo inavyotakiwa. ukianza kusumbua waliokutangulia labda ubadili katiba ubakie madarakani vinginevyo ukishuka tu na anayekuatia anakushughulikia ipasavyo. tuliona mfano wa Chiluba alivyojaribu kumuadhibu Mhasisi wa Taifa la zambia na yeye mwisho wake ulikuwa mbaya kwani alishughulikiwa vilivyo na aliyemfwata. utamaduni huu uendelee vinginevyo itakuwa kasheshe

    ReplyDelete
  4. Aah wapi jamaa alienda kukagua miradi yake huko!!

    ReplyDelete
  5. na waendelee kutumia ndege ya Rais kusafiri nayo amen....

    ReplyDelete
  6. Unamaanisha nini we mdau wa kwanza???
    Kwamba kuogopana na kulindana ndio utamaduni unaouunga mkono??
    Kweli tunakazi kubwa kufikia maendeleo kama kuna watu wanaoweza kudhubutu kufikiri namna hiyo.
    Ni aibu kubwa na hasara kubwa!

    ReplyDelete
  7. tunakukumbuka sana mheshimiwa Mkapa kwa mengi mazuri uliyoyafanya especially uchumi,i wish katiba ingekuwa inakuruhusu ugombee tena uraisi kura yangu ungepata.Mungu azidi kukulinda na kukupa afya njema

    ReplyDelete
  8. We miss u baba, u did a lot, and still the nation is relying on you in so many things. Take us to the right direction and right choice. We remember u for so many things. Eduction, the capital city status, government employee status and the status of the people. We miss u so so much. Live longer, and be blessed.

    ReplyDelete
  9. Yaani kama kungekuwa na uwezekano wa huyu bwana kugombea tena urais tungemrudisha - uchumi ni mbaya kuliko kinoma na hatuoni katika hawa wenye hatihati za kugombea urais ambaye ataweza kurudisha hali bora ya uchumi wote ni mafisadi na waroho wa kujinufaisha bila kukumbuka wananchi wakawaida na nchi yenyewe. JK nchi ameifikisha pabaya kiasi kwamba huyo anatakae chukua hii nchi inabidi awe makini kweli kweli kama alivyo kuwa Mzee Mkapa.

    ReplyDelete
  10. I like this man very executive

    ReplyDelete
  11. hayo ni mambo mazuri ya mheshimiwa kikwete na hakuna mwingine maana mkisema kuwa walio madarakani kuheshimu au kuwapa nafasi waliopita hayo hayakuwa kwa mkapa

    mkapa hakumpa nafasi kabisa mzee wetu mwinyi na kipindi mkapa yupo madarakani mzee wetu ruksa tulimsahau kwenye media zote

    maana alikuwa hahusishwi na chochote na hata kulikuwa na habari za kutendewa ubaya na huyo ben

    big up mh.kikwete mtakaokuja igeni

    ReplyDelete

Hii ni Blog ya Watanzania popote walipo duniani kwa ajili ya kuhabarisha, kutoa/kupokea taarifa na kuelimisha mambo yote yaliyo chanya kwa Taifa letu. Tafadhali sana unapotoa maoni usichafue hali ya hewa wala usijeruhi hisia za mtu/watu. Kuwa mstaarabu...