Habari uncle

Naomba uiweke hii habari kwa blog yako kwa faida ya watanzania wote!

Mimi nashangaa sana utawala wetu wa Jeshi la Polisi sijui una matatizo gani, nipo katika manispaa ya Songea kwa wiki ya tatu sasa kibiashara hali ya huku si shwari kabisa…! Kila siku ni mauaji ya watu kuchinjwa na kunyofolewa nyeti zao, jana ameuawa Shekhe akitoka msikitini, leo dereva wa boda boda nae amechinjwa lakini RPC Michael Kamhanda alipoulizwa anadai eti hana ushahidi wa mauaji hayo na eti mauaji yamebase katika mambo ya wivu wa mapenzi!

 Sasa wivu wa mapenzi hadi kwa shekhe jamani? Karibu kila siku mtu mmoja anauawa hii ni hatari na jeshi lipo kimya sana! Sasa leo asubuhi watu wameamua kuandamana kwenda polisi na ofisi za mkuu wa mkoa kuupeleka mwili wa mmoja wa watu waliouawa leo ili waamini but nashangaa polisi wanatumia nguvu sana kuzima maandamano na hadi hapa naandika taarifa hii ya kwenda kwenye Globu ya Jamii hii nimeshuhudia watu watano wakiwa wameanguka chini kwa kupigwa risasi na haijafahamika kama wamekufa au wako katika hali gani. 

Polisi wanatumia nguvu sana mabomu ya machozi yanapigwa mji mzima na risasi za moto hakuna shughuli inayofanyika katika manispaa ya Songea kwa sasa maduka benki yamefungwa! Lakini hii inatokana na uzembe wa Jeshi la Polisi Mkoani humo wakudharau matatizo ya wananchi! 

Na sasa wanafunzi wa shule za sekondari na msingi nao wanaandamana, kweli Tanzania imebadilika, hali hii sijawahi kuiona katika maisha yangu yote!

Me nahoji nguvu ya polisi iko wapi? Polisi sio tena msaada kwa wananchi bali ni wapenda rushwa! IGP jeshi lako limeoza sana, najua hizi habari za mauaji hazita repotiwa na TBC but picha na video tunazo na zitarushwa tu kwa mtandao muda si mrefu!

Nawasilisha!

Mdau wa libeneke Songea!

Michuzi Blog

Tanzanian blog operating since 2005, covering International news and Local News, including Politics, Fashion, Social Scenes, Interviews, Movies, Events, personalities and anything positive happening worldwide. Written in Swahili and English targeting both Swahili and English readers.

Toa Maoni Yako:

Kuna Maoni 5 mpaka sasa

  1. Chonde chonde, kwa heshima na taadhima shime kwa kila mwenye Mamlaka, Tanzania ya leo sio ya jana na wala haitakuwa ya kesho,

    Tutekeleze wajibu na majukumu yetu, kwa nini Mamlaka nyeti kama Jeshi la Polisi linakubali kupoteza imani yake kwa wananchi kirahisi na kuacha mambo hobelahobela kana kwamba watanzania ni wajinga ama MAJUHA,

    Uwapi Mkuu wa nchi, safari ngapi ZIMEBAKI KWA MWEZI HUU ILI MRADI TUJUE LABDA LINI UTAKUWA MAPUMZIKONI MAANA NAONA CHEO CHA MAMLAKA YA NCHI HAKIJAKUTOKA BADO, KILA LA KHERI

    ReplyDelete
  2. Aibu sana hii coz kama maandamano kama hayo Polisi wanatumia Nguvu kuficha maovu au?

    ReplyDelete
  3. mdau tafadhali rusha picha hizo na pole kwa matatizo.

    ReplyDelete
  4. watu wa songea wamezungukwa na umaskini mkubwa wa kipato tangu kiwanda pekee cha kukausha tumbaku kilipofungwa mnamo mwanzoni mwa mwaka 2000.kiwanda kile kilikuwa kinaajili watu wsio pungua 15000 vijana kwa wazee na hasa wanawake.Serikali haijafanya juhudi zozote kuinua maisha ya watu wa songea zaidi ya kuwaongezea shida na taabu kwa kuzuia biashara huria ya mahindi,njia nyingine pekee inayowapatia watu wa songea kipato mara moja kwa mwaka kila msimu wa mavuno.Sijashangaa leo kusikia wala kuona kinachotokea songea kwani haya yamechelewa sana kutokea.Kitu kikubwa na kilichobaki kwa watu wa songea ni maisha yao tu ambayo wa,meonyesha wapo tayari kuyalinda hata kwa kuyatoa wenyew pale wanapopata nafasi. sina budi kuungana na wana libeneke wengine kulaani na kulaumu kwa nguvu zote kitendo cha jeshi la polisi kutumia nguvu nyingi kuwanyamazisha wadai haki ya kuishi na kuwaacha wauuaji wakijipanga kuongea idadi ya waanga wasio na hatia.Matusi ya RPC na Mkuu wa kituo cha polisi songea kwa wananchi kupitia vyombo vya habari yaliyoriushwa mfululizi tokea juzi 19/2/2012 hadi jana 21/2/2012 ndio chanzo cha umwagaji damu mkubwa uliotokea tokea leo asubuhi mpaka muda huu.Jumla ya raia watano na askari wawili wanasadikiwa kupoteza maisha.Tuwasiliane jioni kwa taarifa zaidi.Makabiliano makali kati ya polisi na wananchi yanaendele maeneo ya matarawe na lizaboni pale mwembechai.
    Babu yetu mpendwa amekwenda na Tanzania yake,wamebakia macowboy wachache wanaichezea nchi kwa jinsi wanavyojisikia!

    Nduna Zimanimoto
    Songea mfaranyaki

    ReplyDelete
  5. sioni kama kuna ulazima wa mapolisi kurusha risasi hewani hadi kumfyatulia binadamu na kusababisha vifo.kuna nyenzo za kuwatawanyisha hawa waandamanaji lkn si risasi, kuwadunda, kuburuza mtu hadi anakufa jameni!. mabomu ya machozi maji yao yanayowasha nakadhalika vyatosha kabisa kutuliza ghasia za waandamanaji. Polisi kuweni makini msifanye mambo ambayo yanaweza kuvuruga utendaji wa kazi na mipangilio ndani ya jeshi la polisi kama vile jela, kuachishwa kazi na marishafo ya hapa na pale. Mungu atubariki, tulipende Taifa letu la Tanzania amani itawale.

    ReplyDelete

Hii ni Blog ya Watanzania popote walipo duniani kwa ajili ya kuhabarisha, kutoa/kupokea taarifa na kuelimisha mambo yote yaliyo chanya kwa Taifa letu. Tafadhali sana unapotoa maoni usichafue hali ya hewa wala usijeruhi hisia za mtu/watu. Kuwa mstaarabu...