HABARI ILIYOTUFIKIA HIVI PUNDE TOKA MKOANI KILIMANJARO,INAELEZA KUWA MWANAFUNZI ALIEKUWA MAJERUHI KWENYE AJALI YA GARI ILIYOTOKEA KATIKA SHULE YA SEKONDARI YA KOROGWE GIRLS MKOANI TANGA HIVI KARIBUNI,AITWAYE ZAHRA JUMANNE AMEFARIKI DUNIA MCHANA HUU KATIKA HOSPITALI YA KCMC MJINI MOSHI.

MWANAFUNZI HUYO AMBAYE ALIUMIA VIBAYA SANA NA MPAKA KUPELEKEA KIFO CHAKE BAADA YA KUGONGWA NA GARI LILILOKUWA LIKIENDESHWA NA MMOJA WA WANAFUNZI WA SHULE HIYO.

TUTAENDELEA KUPEANA TAARIFA KADRI ZITAKAVYOKUWA ZINATUFIKIA HAPA GLOBUNI.

Michuzi Blog

Tanzanian blog operating since 2005, covering International news and Local News, including Politics, Fashion, Social Scenes, Interviews, Movies, Events, personalities and anything positive happening worldwide. Written in Swahili and English targeting both Swahili and English readers.

Toa Maoni Yako:

Kuna Maoni 26 mpaka sasa

  1. jamani Zahra!lala pema mama..inauma na kuumiza sana,mwenyezi mungu awape nguvu na faraja wazazi na ndugu za marehemu

    ReplyDelete
  2. Mama yangu wee!!!! Hiki kizahazaha kimekuwa hivi tena.
    Poleni sana Ndugu na jamaa wote kwa msiba huu.

    ReplyDelete
  3. janeth k dms
    jamani Mungu amuweke mahala pema peponi, nawapa pole wafiwa ,tushukuru Mungu kwa kila jambo.

    ReplyDelete
  4. inna lilah waina ilaih rajiuni...mipango ya Allah, lakn inaumiza sana ukizingatia sababu iliyosababisha ajali...kibibi kama ana akili atalia sana tu, sana...ila asije akakufuru tu

    ReplyDelete
  5. what a bad ending to this already sad story.

    ReplyDelete
  6. Daaa! Mungu ailaze roho ya marehemu mahali pema peponi!

    ReplyDelete
  7. Hakuna mipango ya Mungu hapa. Tujifunze kuwa responsible na actions zetu. Hiyo ni negligent homicide na ni lazima mhusika awajibishwe. Hata kama haitamrudisha marehemu iwe fundisho kwa wengine wenye tabia ya kushow off vitu wasivyoweza. Nna hasira kweli basi tu. Mungu watie nguvu jamaa namarafiki wa binti huyu.

    ReplyDelete
  8. Nikweli kabisa, nakubaliana na wewe....wakati mwingine hatuwi makini na mambo hatari kama haya hasa ya vyombo vya moto....ikitokea, utasikia ni mipango ya Mungu....huyu msichana alitaka kuonyesha wenzake kuwa yeye ndo sana, hana leseni ya kuendesha gari (sidhani kama anayo) halafu tunasema bahati mbaya, kama ana akili timamu hapa hakuna bahati mbaya.

    ReplyDelete
  9. Kwanza kabisa huyu jamaa aliye mgonga binti huyu ahukumie na apewe adhabu kali sana kwasababu huwezi kumgonga mtu shuleni mpaka akafa kwani shuleni sio kwenye highway alikuwa anakimbiza gari in residential area haki ya mungu its so sad . RIP

    ReplyDelete
  10. Inna Lillah wa Inna Ilayhi Rajiuuuun!

    ReplyDelete
  11. Mungu mwenyewe ndo anajua na ndio mtoa hukumu, wadau hapo juu ambao mmekuwa wakali kwamba huyu mhusika apewe adhabu kali nyie ni miungu wa dunia; hebu jiweke wewe kwenye viatu vya binti aliyesababisha ajali je ungeomba iwe vipi.

    ReplyDelete
  12. Nimeumia sana kusoma habari za binti huyu ambaye alikuwa afanye mitihani yake ya kumaliza form 6 tarehe 8/2/2012. Hili liwe ni fundisho kwa jamii kwani ni uzembe wa hali ya juu huu. Kama shule ingekuwa imeandaa eneo la kuegesha magari yote haya yasingetokea. Mungu wape faraja ya pekee wazazi wa binti huyo.

    ReplyDelete
  13. Innalillah wainaillaihi rajiun, kilz mtu ataondoka duniani kwa muda na sababu aliyopangia. Hiyo ajali ngio ilikuwa sababu ya kifo chake, haliwi jambo isipokuwa kwa idhini ya muumba wetu. Na sidhani kama huyo binti alikusudia kumuua mwenzake, wengine wanaondoka kwa maradhi wengine kwa ajali tusifikie kukufuru kila mwanadamu ana mwanzo na mwisho wake wengine huondoka wadogo wengine wazee kwa hiyo tuwe na subra na umshukuru Mungu kwa yote hayo ya kesi waachiwe polisi na mahakama!

    ReplyDelete
  14. Inabidi msichana aliyeendesha gari bila leseni achukuliwe hatua na pia kaka wa msichana aliyemruhusu mdogo wake kwa kumpatia funguo akaendesha gari akijua kuwa mdogo wake hajui kuendesha na hana leseni naye kaka mtu achukuliwe hatua kwa uzembe.

    ReplyDelete
  15. wewe anony wa Mon Feb 06, 02:14:00 AM 2012 seems hii habari hauifahamu so no right to comment, aliekuambia amegongwa kwa speeding car nani? duh kweli story yaweza geuzwa miguu juu kichwa chini fasta!

    ReplyDelete
  16. MACHOZI YANANITOKA TU SINA CHA KUSEMA ZAIDI POLENI WAZAZA WAKE!

    ReplyDelete
  17. Mwenyezi mungu watie nguvu na moyo wa uvumilivu ndugu, jamaa, marafiki na wapendwa wote wa Zahra. RIP baby.

    Lakini pia kwa wote wenye tabia ya kiherehere cha kuendesha magari au kutumia mashine bila ujuzi kama alivyofanya mwanafunzi huyu wanasitahili adhabu kali. Je hapa atasema kaua bila kukusudia? Familia nyingi zina watu wazima/vijana/watoto wa namna hii. Hli liwe fundishooo!!! Inauma sana

    ReplyDelete
  18. polisi wanasemaje kuhusu ajali na kifo cha binti Zahara? Kamanda Massawe wa Tanga anasema hajui wamshitaki nani... mwenye gari au kibibi!

    ReplyDelete
  19. RIP Zahra! Kweli mungu ni mpangaji wa yote.

    ReplyDelete
  20. Huyo jamaa aliyetuma saa 07:20 am haelewichanzo cha ajali, amekurupuka tu kuanska kwa sababu naye anajua kuandika.Labda nimfahamishe, Wanafunzi wa kidato cha sita walikuwa kwenye graduation, mmmoja kati yao alitembelewa na baba yake akiwa na gari, alichukua (mtoto)ufunguo wa gari na kuanza kuosha jina ndipo ajali ikatokea ya kuwagonga vibaya wanafunzi wenzake na baadhi ya raia wengine akiwepo mpiga picha maarufu aitwaye Ngoswe)wa mjini Lushoto, Hatimae mmoja wa majeruhi ndio huyo ameaga dunia.Hakuna cha high hapo

    ReplyDelete
  21. Inna lillah wa Ina ilayhi Rajiuuun. pole sana kwa familia.

    husna

    ReplyDelete
  22. Ee Mungu wa Rehema wape faraja ya kweli wafiwa na wote walioguswa na msiba huo. Ifude

    ReplyDelete
  23. May her soul R.I.P................pole kwa wanandugu jamaa na marafiki wote.

    ReplyDelete
  24. Maafa yanayotokana na uzembe tusimsingizie Mungu. Mmiliki wa gari anatakiwa ashitakiwe kwa uzembe wa kutoangalia gari lake. Na huyo binti awajibishwe kwa ubishoo wake. Mungu ailaze roho ya marehemu mahali pema peponi na awape nguvu wafiwa katika kipindi hiki cha huzuni. Kwa kweli inauma na inasikitisha sana. TUACHE UBISHOO JAMANI. VITU VYA MOTO NI HATARI HATA KAMA UMEVIZOEA.

    ReplyDelete
  25. Inna Lillah wa Inna Ilayhi Rajiuuuun! Sisi sote ni waja wake na tutarejea kwake, na kila mmoja kwa safari yake aliyoandikiwa. Mwenyezi Mungu aiweke roho ya marehemu mahali pema peponi, Amin.

    ReplyDelete
  26. So sad story,jina la bwana lihimidiwe

    ReplyDelete

Hii ni Blog ya Watanzania popote walipo duniani kwa ajili ya kuhabarisha, kutoa/kupokea taarifa na kuelimisha mambo yote yaliyo chanya kwa Taifa letu. Tafadhali sana unapotoa maoni usichafue hali ya hewa wala usijeruhi hisia za mtu/watu. Kuwa mstaarabu...