HABARI ILIYOTUFIKIA HIVI PUNDE TOKA MKOANI KILIMANJARO,INAELEZA KUWA MWANAFUNZI ALIEKUWA MAJERUHI KWENYE AJALI YA GARI ILIYOTOKEA KATIKA SHULE YA SEKONDARI YA KOROGWE GIRLS MKOANI TANGA HIVI KARIBUNI,AITWAYE ZAHRA JUMANNE AMEFARIKI DUNIA MCHANA HUU KATIKA HOSPITALI YA KCMC MJINI MOSHI.
MWANAFUNZI HUYO AMBAYE ALIUMIA VIBAYA SANA NA MPAKA KUPELEKEA KIFO CHAKE BAADA YA KUGONGWA NA GARI LILILOKUWA LIKIENDESHWA NA MMOJA WA WANAFUNZI WA SHULE HIYO.
TUTAENDELEA KUPEANA TAARIFA KADRI ZITAKAVYOKUWA ZINATUFIKIA HAPA GLOBUNI.
jamani Zahra!lala pema mama..inauma na kuumiza sana,mwenyezi mungu awape nguvu na faraja wazazi na ndugu za marehemu
ReplyDeleteMama yangu wee!!!! Hiki kizahazaha kimekuwa hivi tena.
ReplyDeletePoleni sana Ndugu na jamaa wote kwa msiba huu.
janeth k dms
ReplyDeletejamani Mungu amuweke mahala pema peponi, nawapa pole wafiwa ,tushukuru Mungu kwa kila jambo.
inna lilah waina ilaih rajiuni...mipango ya Allah, lakn inaumiza sana ukizingatia sababu iliyosababisha ajali...kibibi kama ana akili atalia sana tu, sana...ila asije akakufuru tu
ReplyDeletewhat a bad ending to this already sad story.
ReplyDeleteDaaa! Mungu ailaze roho ya marehemu mahali pema peponi!
ReplyDeleteHakuna mipango ya Mungu hapa. Tujifunze kuwa responsible na actions zetu. Hiyo ni negligent homicide na ni lazima mhusika awajibishwe. Hata kama haitamrudisha marehemu iwe fundisho kwa wengine wenye tabia ya kushow off vitu wasivyoweza. Nna hasira kweli basi tu. Mungu watie nguvu jamaa namarafiki wa binti huyu.
ReplyDeleteNikweli kabisa, nakubaliana na wewe....wakati mwingine hatuwi makini na mambo hatari kama haya hasa ya vyombo vya moto....ikitokea, utasikia ni mipango ya Mungu....huyu msichana alitaka kuonyesha wenzake kuwa yeye ndo sana, hana leseni ya kuendesha gari (sidhani kama anayo) halafu tunasema bahati mbaya, kama ana akili timamu hapa hakuna bahati mbaya.
ReplyDeleteKwanza kabisa huyu jamaa aliye mgonga binti huyu ahukumie na apewe adhabu kali sana kwasababu huwezi kumgonga mtu shuleni mpaka akafa kwani shuleni sio kwenye highway alikuwa anakimbiza gari in residential area haki ya mungu its so sad . RIP
ReplyDeleteInna Lillah wa Inna Ilayhi Rajiuuuun!
ReplyDeleteMungu mwenyewe ndo anajua na ndio mtoa hukumu, wadau hapo juu ambao mmekuwa wakali kwamba huyu mhusika apewe adhabu kali nyie ni miungu wa dunia; hebu jiweke wewe kwenye viatu vya binti aliyesababisha ajali je ungeomba iwe vipi.
ReplyDeleteNimeumia sana kusoma habari za binti huyu ambaye alikuwa afanye mitihani yake ya kumaliza form 6 tarehe 8/2/2012. Hili liwe ni fundisho kwa jamii kwani ni uzembe wa hali ya juu huu. Kama shule ingekuwa imeandaa eneo la kuegesha magari yote haya yasingetokea. Mungu wape faraja ya pekee wazazi wa binti huyo.
ReplyDeleteInnalillah wainaillaihi rajiun, kilz mtu ataondoka duniani kwa muda na sababu aliyopangia. Hiyo ajali ngio ilikuwa sababu ya kifo chake, haliwi jambo isipokuwa kwa idhini ya muumba wetu. Na sidhani kama huyo binti alikusudia kumuua mwenzake, wengine wanaondoka kwa maradhi wengine kwa ajali tusifikie kukufuru kila mwanadamu ana mwanzo na mwisho wake wengine huondoka wadogo wengine wazee kwa hiyo tuwe na subra na umshukuru Mungu kwa yote hayo ya kesi waachiwe polisi na mahakama!
ReplyDeleteInabidi msichana aliyeendesha gari bila leseni achukuliwe hatua na pia kaka wa msichana aliyemruhusu mdogo wake kwa kumpatia funguo akaendesha gari akijua kuwa mdogo wake hajui kuendesha na hana leseni naye kaka mtu achukuliwe hatua kwa uzembe.
ReplyDeletewewe anony wa Mon Feb 06, 02:14:00 AM 2012 seems hii habari hauifahamu so no right to comment, aliekuambia amegongwa kwa speeding car nani? duh kweli story yaweza geuzwa miguu juu kichwa chini fasta!
ReplyDeleteMACHOZI YANANITOKA TU SINA CHA KUSEMA ZAIDI POLENI WAZAZA WAKE!
ReplyDeleteMwenyezi mungu watie nguvu na moyo wa uvumilivu ndugu, jamaa, marafiki na wapendwa wote wa Zahra. RIP baby.
ReplyDeleteLakini pia kwa wote wenye tabia ya kiherehere cha kuendesha magari au kutumia mashine bila ujuzi kama alivyofanya mwanafunzi huyu wanasitahili adhabu kali. Je hapa atasema kaua bila kukusudia? Familia nyingi zina watu wazima/vijana/watoto wa namna hii. Hli liwe fundishooo!!! Inauma sana
polisi wanasemaje kuhusu ajali na kifo cha binti Zahara? Kamanda Massawe wa Tanga anasema hajui wamshitaki nani... mwenye gari au kibibi!
ReplyDeleteRIP Zahra! Kweli mungu ni mpangaji wa yote.
ReplyDeleteHuyo jamaa aliyetuma saa 07:20 am haelewichanzo cha ajali, amekurupuka tu kuanska kwa sababu naye anajua kuandika.Labda nimfahamishe, Wanafunzi wa kidato cha sita walikuwa kwenye graduation, mmmoja kati yao alitembelewa na baba yake akiwa na gari, alichukua (mtoto)ufunguo wa gari na kuanza kuosha jina ndipo ajali ikatokea ya kuwagonga vibaya wanafunzi wenzake na baadhi ya raia wengine akiwepo mpiga picha maarufu aitwaye Ngoswe)wa mjini Lushoto, Hatimae mmoja wa majeruhi ndio huyo ameaga dunia.Hakuna cha high hapo
ReplyDeleteInna lillah wa Ina ilayhi Rajiuuun. pole sana kwa familia.
ReplyDeletehusna
Ee Mungu wa Rehema wape faraja ya kweli wafiwa na wote walioguswa na msiba huo. Ifude
ReplyDeleteMay her soul R.I.P................pole kwa wanandugu jamaa na marafiki wote.
ReplyDeleteMaafa yanayotokana na uzembe tusimsingizie Mungu. Mmiliki wa gari anatakiwa ashitakiwe kwa uzembe wa kutoangalia gari lake. Na huyo binti awajibishwe kwa ubishoo wake. Mungu ailaze roho ya marehemu mahali pema peponi na awape nguvu wafiwa katika kipindi hiki cha huzuni. Kwa kweli inauma na inasikitisha sana. TUACHE UBISHOO JAMANI. VITU VYA MOTO NI HATARI HATA KAMA UMEVIZOEA.
ReplyDeleteInna Lillah wa Inna Ilayhi Rajiuuuun! Sisi sote ni waja wake na tutarejea kwake, na kila mmoja kwa safari yake aliyoandikiwa. Mwenyezi Mungu aiweke roho ya marehemu mahali pema peponi, Amin.
ReplyDeleteSo sad story,jina la bwana lihimidiwe
ReplyDelete