Makamu wa Rais wa Jamhuri ya Muungano wa Tanzania, Dkt. Mohammed Gharib Bilal, akisalimiana na Rais Mstaafu wa awamu ya pili, Ali Hassan Mwinyi, wakati alipowasili kwenye viwanja vya Mnazi Mmoja katika shambrashambra za mkesha wa sherehe za Maulid, jijini Dar es Salaam jana Februari 04, 2012 usiku.
Makamu wa Rais wa Jamhuri ya Muungano wa Tanzania, Dkt. Mohammed Gharib Bilal(katikati) Rais Mstaafu wa awamu ya pili, Ali Hassan Mwinyi na Waziri Mkuu Mstaafu, Edward Lowasa, wakiwa katika sherehe za mkesha wa Maulid, zilizofanyika usiku wa kuamkia leo, jana usiku Februari 04, 2012, katika viwanja vya Mnazi Mmoja jijini Dar es Salaam.
Makamu wa Rais wa Jamhuri ya Muungano wa Tanzania, Dkt. Mohammed Gharib Bilal, akiteta jambo na Waziri Mkuu Mstaafu Edward Lowasa, wakati wakiwa katika sherehe za mkesha wa Maulid, zilizofanyika usiku wa kuamkia leo, jana usiku Februari 04, 2012, katika viwanja vya Mnazi Mmoja jijini Dar es Salaam.
Muumin wa dini ya kiislam kutoka Msikiti wa Suni Hanafi wa jijini Dar es
Salaam, Muzamil Chaki, akiimba Qaswaida jukwaani kutoa burudani wakati wa mkesha wa sherehe za Mauilid zilizofanyika katika Viwanja vya Mnazi Mmoja jijini jana usiku Februari 04, 2012.
Makamu wa Rais wa Jamhuri ya Muungano wa Tanzania, Dkt.Mohammed Gharib Bilal,
akisalimiana na Muumin wa dini ya kiislam kutoka Msikiti wa Suni Hanafi wa jijini Dar es
Salaam, Muzamil Chaki, baada ya muumini huyo kumaliza kutoa burudani ya Qaswaida jukwaani, wakati wa mkesha wa sherehe za Mauilid zilizofanyika katika Viwanja vya Mnazi Mmoja jijini jana usiku Februari 04, 2012.Picha na Muhidin Sufiani-OMR

Michuzi Blog

Tanzanian blog operating since 2005, covering International news and Local News, including Politics, Fashion, Social Scenes, Interviews, Movies, Events, personalities and anything positive happening worldwide. Written in Swahili and English targeting both Swahili and English readers.

Toa Maoni Yako:

Kuna Maoni 7 mpaka sasa

  1. Mzee Lowassa hapo nakuvulia kofia, yaani una ratiba ya shughuli zote za dini zote!

    Jaribu kupata na sherehe wa Wahindu ukamilishe ratiba yako

    ReplyDelete
  2. Lowassa kiboko, duh! Ungepiga basi na kofia kama Lyatonga.

    ReplyDelete
  3. big up lowasa wetuuu

    ReplyDelete
  4. Mheshimiwa Lowasa kweli wewe ni mtu wa watu licha ya magumu yote unayozushiwa. Usife moyo ipo siku.

    ReplyDelete
  5. Duh! Jamaa kweli anautaka u prezdaa.

    ReplyDelete
  6. Mtumaini Mungu. Ikiwa imeandikwa, hakuna kilichoko chini ya jua kitakachokuzuia. Mengine yooote ni maneno, ambayo, kama bin-
    Adam kamwe hutaweza kuwachagulia ya kuongea!

    ReplyDelete
  7. Lowassa ahsante kwa kuthamini na kujali Imani mbali mbali za Dini!

    ReplyDelete

Hii ni Blog ya Watanzania popote walipo duniani kwa ajili ya kuhabarisha, kutoa/kupokea taarifa na kuelimisha mambo yote yaliyo chanya kwa Taifa letu. Tafadhali sana unapotoa maoni usichafue hali ya hewa wala usijeruhi hisia za mtu/watu. Kuwa mstaarabu...