Paka akiwa uwanja wa Anfield wa Bwawa la Maini usiku wa kuamkia leo wakati wa mechi na Totenham iliyoisha 0-0. Inaelekea Spurs walitaka sana ushindi hadi kuja na mnyama huyu aliyesababisha mechi isimame kwa dakika nne

Michuzi Blog

Tanzanian blog operating since 2005, covering International news and Local News, including Politics, Fashion, Social Scenes, Interviews, Movies, Events, personalities and anything positive happening worldwide. Written in Swahili and English targeting both Swahili and English readers.

Toa Maoni Yako:

Kuna Maoni 20 mpaka sasa

  1. Manyau nyau wa liverpool..

    ReplyDelete
  2. Mentality ya mswahili bwana... kila kitu kuhusisha na uchawi...

    ReplyDelete
  3. hahahahah, nimechekaje jamani, nao wamo ankal

    ReplyDelete
  4. Hapana, wenzetu si washirikina kama sisi Waafrika. Nakumbuka mwaka 2004 Morogoro mjini paka alichomwa moto akiwa hai hadharani na hamna hata kiongozi mmoja wa dini au wa siasa Tanzania nzima aliyekemea ushenzi na ukatili huo uliofanywa hadharani na kutolewa katika gazeti la Majira jumapili. Ujinga na ushirikina ni chanzo kikubwa cha ushenzi. Tuache kuwa washirikina. Tuko karne ya 21, tumwabudu Mwenyezi Mungu peke yake na tukabali kuwa sayansi, teknolojia na uchapakazi (si uchawi) ndio ukombozi wetu. Ahsante sana Ankal Michu (mdau wa fulana maarufu) kwa kuchapisha maoni yangu.

    ReplyDelete
  5. Mnasema soka la africa tu ndo uchawi unatumika! hii nini?

    ReplyDelete
  6. watu bwana, eti spurs walitaka washinde, aliekuambia niwao walimleta huyo nyau nani? nyau wewe pumbavuuuu

    ReplyDelete
  7. Ingekuwa Bongo huyo paka lazima angeuawa kwa kusingiziwa 'mwanga'.

    ReplyDelete
  8. he he heee mngeomba na nyinyi mbebwe chealse mlijiona mko juu ha ha haaa sisi ndio red devil bwana wala hatukubebwaaa ni raha tuuuuu ha ha haaaa! man u daimaaaaa!

    ReplyDelete
  9. Huyo paka kaja na mwenyewe humo sio kila kitu uchawi mbona hivyo wajameni itakuwaje sasa ,nafikiri Ulaya ndio bara la kwanza kwa kuwa napaka wengi zaidi ya ulimwengu wote na wanatunzwa na wana haki sio kama kwetu huko ushenzini kama si uchawi ni chakula swain wakubwa watanzania!

    ReplyDelete
  10. we mdau wa Tue Feb 07, 09:18:00 AM 2012, HAPA NI JUST JOKES , vichwa vingine mnachelewa kuelewa kweli kweli!!!!dah

    mdau-changose

    ReplyDelete
  11. ingekuwa bongo sasa hivi kesha kuwa marehemu

    ReplyDelete
  12. hawana muda huo wakuchezea na kutafuta ushirikina kwenye michezo ni juhudi na maarifa ndiyo inayo tumika kwenye michezo

    ReplyDelete
  13. Wale "Stewards" walimbeba baadae sijui walimpeleka wapi.Lingekuwa pambano la S na Y kingekuwa kizaaa.Timu zimejaa wasomi lakini Imani za kishirikana kibao.Mwesi upo hapo??

    David V

    ReplyDelete
  14. Usitake kusema mentality za kiswahili hata mtangazaji jana kasema wapo wanaofikiria Uchawi kwahiyo hata wazungu wanafikiria hivyo, Manchester United wana mchawi wa karne mpya Howard WEBB, ila Ankal kaleta Mada kwa kufurahisha chukue au acha juu yako. Huyo Nyau wa Zanzibar au Tanga au Bagamoyo itakuwa Italy Lol. Ndosi.

    ReplyDelete
  15. wewe Anon wa 09:18:00 AM

    nani kakudanganya kuwa ni mentality ya mswahili? I wish ungewasikia commentators wa chanel niloangalizia mechi jana, nayo ni ya haohao waingereza.

    ReplyDelete
  16. Huu Mfugo utakuwa umechomoka kwenye Kapu la Babu Rednap, kaumbuka mi huamini yule mzee sio bure anajua vituzi vya kibagamoyo hawezi kuwa anagaa kila msimu, kumbe yumo bana

    ReplyDelete
  17. huyo ni nyau wa dalglish hata comentator alijoke hivyo. hata wazungu wana hisia na matendo hayo ya kishirikina kama sio neno superstitious ambayo maana yake ni "convinced that performing or not performing specific actions brings good or bad luck, that some events or phenomena are omens, and, generally, fearfully believing in a supernatural dimension to events" limetoka wapi? nakumbuka nilimsikia comentator akisema "it's not even a black cat so it doesn't bring any lucky" hao jamaa weupe kwa uchawi wanatuzidi sana sisi. wakati sis tunaogopa paka mweusi wao ndio wanaona ni safi huyo.

    ReplyDelete
  18. http://thekop.liverpoolfc.tv/_My-Pet-the-Kopite/photo/14650616/173471.html?enlarge=true


    Huyo juu Kopi Endi Pasti atakuwa ndio huyo nini? @ Ankal

    ReplyDelete
  19. Hata ukimwangalia huyo paka sura yake kafanana na K.Danglish

    ReplyDelete
  20. Uchawi upo Ulaya na unatumika sana.mfano kuna gazeti www.ukmetro.co.uk kuna ukurasa wa waganga wa jadi.

    miaka mtano iliyopita Uingereza walifanya sensa za waganga na wachawi ambao ni registered.wachawi walikuwa na idadi ya watu mia nane.waganga walikuwa maelfu.

    hata Ancelloti aliyekuwa kocha wa Chelsea aliwahi kusema kuwa Drogba anatumia uchawi hakuna mchezaji atakayeweza kuchukua namba yake na ushahidi uko Shivshenko alishindwa,Mutu alishindwa na sasa Torres.

    Jose Morninnho anatumia sana uchawi amewahi kwenda Mombasa kutafuta waganga na hata Uingereza imetawala nchi nyingi kwa nguvu za uchawi. malkia huwa anafanya matambiko nyumbani kwake Windsor.

    kuna mganga wa kihindi anaitwa Meera andika First indian lady to combine the powers and secrets of tarot.simu yake +447590894770.

    au Mr.soreba spiritual healer love and relationship specialist huyu anatoka spain.Simu yake +447961038985 jaribuni ku google mtajiona mambo.

    na huyu paka atakuwa wa Reidnapp kwa vile ana kesi mahakamani ameamua kuwakilishwa na paka uwanjani jana hakuwepo uwanjani.

    wazungu wanafanya sana ushirikina.msiwaone wazungu ni watu tofauti na sisi.wana mapungufu yao zaidi yetu.

    ReplyDelete

Hii ni Blog ya Watanzania popote walipo duniani kwa ajili ya kuhabarisha, kutoa/kupokea taarifa na kuelimisha mambo yote yaliyo chanya kwa Taifa letu. Tafadhali sana unapotoa maoni usichafue hali ya hewa wala usijeruhi hisia za mtu/watu. Kuwa mstaarabu...