Prof. Abdulrahman Salim Msangi |
Baba yetu mpendwa tarehe 5 February 2012 unatimiza miaka 10 tangu ulipotutoka.
Tulikupenda sana ila Mwenyezi Mungu alikupenda zaidi. Tunakuombea na kukumbuka sana hekima, busara na upendo wako kwetu.
Unakumbukwa na mkeo Margareth Msangi, wanao Rehema, Sophia , Amina, Shanura, Hawa, Mainda, Lulu, Kheri na Mustafa pamoja na wajukuu zako wote, ndugu jamaa na marafiki.
Inna Lil’lahi Wa Inna Ilahi Raajioon
poleni Shanura na ndugu zako wote msiba mkubwa, Shanura na mdogo wako mmoja mlisoma Ashira?
ReplyDeleteHivi mara hii imetimia miaka kumi, loh na sisi ndiyo tunakaribia kifo hivyo!
ReplyDeleteMungu amuweke pema peponi.
Mtanzania wa kwanza kupata shahada ya London University mwaka 1957. Wakati huo Makerere University ilikuwa tawi la London University.
ReplyDeleteKwanini Waislamu wa Pwani hawajasoma kama hawa wenzao wa kutoka mrima?
ReplyDeletePoleni kwa yote, ila nasikia faraja kuona msomi kama huyo akiwa na idadi kubwa ya watoto, naona waliorodheshwa hapo ni kama tisa vile. Ila kwa sasa wasomi hawataki na kuwa na watoto wengi kwa kisingizio cha maisha magumu, maisha yamekuwa magumu toka Adam na Hawa waliposhushwa toka mbinguni kwa mtu mwenye imani ya dini. Nasaha yangu kwangu ni kuwa wasomi tuzinduke tuijaze tanzania inahitaji nguvu kazi na ukiangaliza nchi zote zenye maendeleo utaona uwiano wake wa watu ni mkubwa. Tuamke sasa na tuachane na propaganda za mpango wa uzazi, mpango wa uzazi uwe katika spacing ya watoto na sio idadi. Najua waosha vinywa mtanishambulia, lakini huo ndio mtazamo wangu.
ReplyDeleteWe mdudu unayehoji kuwa kwa nini waislam wa pwani hawajasoma kama hao wa mrima una takwimu zozote kuthibitisha ujinga wako au unaandika tu maadam unaweza kubofya vitufe vya maandishi.kaa chini utafute takwimu za waislam wa pwani waliosoma mpaka kiwango cha degree na utapata majibu.sisi sio watu wa kujikweza kwenye kadamnasi ili tupate kujulikana kuwa tupo kama akina ninyi.
ReplyDeleteWa mrima wengi haikuwa tabu kubadili dini!!!! tofauti na wenzao wa pwani
ReplyDeleteFor anyone fortunate to have been touched by the life of Prof. Msangi will forever be grateful for his insights, reflections and wisdom. RIP.
ReplyDeleteMjomba angu amepata Degree B.Sc. in Chemistry kutoka University of Hull Uingereza in 1947 na yuhai mpaka leo amefundisha miaka mingi skuli ya Secondari Lumumba zanzibar. Acheni ujinga watu wa pwani wengi wamesoma na hawakuwa na haja ya kubadilisha zao kingia shule. Nyie ndio wale wanoona mtu amevaa hijabu hakusoma. Huu ni ujinga wa aina fulani ambao unatawala wenzetu.
ReplyDelete