Ofisa wa polisi jamii mkoa wa Arusha Afande Mary Lugola akiwa anaongea na wananchi wa kata ya Elerai  Picha na Habari na Woinde Shizza wa Globu ya Jamii Arusha



POLISI Mkoa wa Arusha, umewataka wananchi kuwafichua wahalifu mapema kabla ya kufanya uhalifu.

Ofisa Mkuu wa Polisi Jamii wa mkoa huo,  Afande Mary Lugola, ambaye pia ni mlezi wa polisi jamii Kata ya Elerai, alisema hayo wakati akitoa mafunzo kuhusu polisi jamii kwa wananchi wa kata hiyo.

Alisema kila mwananchi anatakiwa kuwafichua wahalifu ambao wanaishi karibu nao au mtu ye yote ambaye anamuonea wasiwasi kuwa ni muhalifu au anatarajia kufanya uhalifu kabla ya madhara hayajatokea.

Alisema polisi watatoa ushirikiano wa hali na mali  iwapo mwananchi atatoa taarifa  kuhusiana na uhalifu wa aina yoyote.

“Ukiwa una taarifa yo yote ya uhalifu iwe ni mtu anauza bangi au anauza gongo au anataka kwenda kuiba sehemu, toa taarifa kwa polisi na sisi tutamfichua mapema na kumchukulia hatua kabla ya mtu huyo hajafanya tukio lolote la uhalifu,” alisema.

Kuhusu malalamiko ya unyanyasaji yanayofanywa na Wamasai kwa maelezo ya kutekeleza mila zao, Mary alisema polisi kawa kushirikiana na polisi jamii watahakikisha kwamba unyanyasaji huo hauendelei kufanywa kwa kigezo cha kudumisha mila.

Katika kutekelea mila za Kimasai, hususan, jando, inadaiwa kuwa baadhi yao wananyanyaswa kwa kuvalishwa mabati, magunia, kuzomewa na mambo mengine kadhaa.

“Napenda kuwaambiwa wananchi hawa ambao wamekuwa wakifanyiwa vitendo hivi kuwa ili kumrahisishia polisi  kazi yake na ishughulikiwe mapema ni lazima mtu yule amfahamu mtu aliye mfanyika kitendo hicho japo kwa sura ili aweze kuchukuliwa hatua za kisheria,”  alisema.

Michuzi Blog

Tanzanian blog operating since 2005, covering International news and Local News, including Politics, Fashion, Social Scenes, Interviews, Movies, Events, personalities and anything positive happening worldwide. Written in Swahili and English targeting both Swahili and English readers.

Toa Maoni Yako:

Kuna Maoni 2 mpaka sasa

  1. Polisi Jamii na Libeneke Arusha,

    Sawa kazi ni nzuri sana, isipokuwa Sheria za Kiraia na Taratibu za Haki za Msingi za kibinaadamu ni lazima zizingatiwe.

    Nilishuhudia hapa Dar Es Salaam siku moja pale Mzunguko wa Shule ya Uhuru pembeni ya ukuta njia ya Ilala ilikuwa saa 2:30 za Usiku alijibanza jamaa mmoja anakojoa ukutani Polisi Jamii walitokea wakamkamata wakaanza kumpa kipigo Jamaa akawaweleza kuwa anakojoa pale kwa dharura yeye ni Mgonjwa wa Kisukari na dawa alikuwa nazo mkononi na Vyeti (kwa kawaida Wagonjwa wa Kisukari hukojoa kupita kiasi) Polisi Jamii hawakumuelewa wakamkokota hadi Polisi Posti ya Relini karibu na Kamata/Scandinavia Terminal kufika pale Afande wa Zamu Kaunta alipomhoji na alipoona vielelezo Jamaa kweli ni Mgonjwa wa Kisukari alimwachia.

    ReplyDelete
  2. Sheria za Kiraia na Haki za Msingi za Kibinaadamu,Kuthamini Utu wa watu zaidi na Ustaarabu.

    Wamasai Arusha, Dumisheni Mila na Jadi ila kwa njia za Kistaarabu na Kidiplomasia zaidi kuliko Mabavu na Umorani wa Manyatta na kwenye Maboma, Mbugani.

    ReplyDelete

Hii ni Blog ya Watanzania popote walipo duniani kwa ajili ya kuhabarisha, kutoa/kupokea taarifa na kuelimisha mambo yote yaliyo chanya kwa Taifa letu. Tafadhali sana unapotoa maoni usichafue hali ya hewa wala usijeruhi hisia za mtu/watu. Kuwa mstaarabu...