Makamu wa Rais wa Jamhuri ya Muungano wa Tanzania, Dkt. Mohammed Gharib Bilal, akisalimiana na Rais Mstaafu wa awamu ya pili, Ali Hassan Mwinyi, wakati alipowasili kwenye viwanja vya Mnazi Mmoja katika shambrashambra za mkesha wa sherehe za Maulid, jijini Dar es Salaam jana Februari 04, 2012 usiku.
Makamu wa Rais wa Jamhuri ya Muungano wa Tanzania, Dkt. Mohammed Gharib Bilal(katikati) Rais Mstaafu wa awamu ya pili, Ali Hassan Mwinyi na Waziri Mkuu Mstaafu, Edward Lowasa, wakiwa katika sherehe za mkesha wa Maulid, zilizofanyika usiku wa kuamkia leo, jana usiku Februari 04, 2012, katika viwanja vya Mnazi Mmoja jijini Dar es Salaam.
Makamu wa Rais wa Jamhuri ya Muungano wa Tanzania, Dkt. Mohammed Gharib Bilal, akiteta jambo na Waziri Mkuu Mstaafu Edward Lowasa, wakati wakiwa katika sherehe za mkesha wa Maulid, zilizofanyika usiku wa kuamkia leo, jana usiku Februari 04, 2012, katika viwanja vya Mnazi Mmoja jijini Dar es Salaam.
Muumin wa dini ya kiislam kutoka Msikiti wa Suni Hanafi wa jijini Dar es
Salaam, Muzamil Chaki, akiimba Qaswaida jukwaani kutoa burudani wakati wa mkesha wa sherehe za Mauilid zilizofanyika katika Viwanja vya Mnazi Mmoja jijini jana usiku Februari 04, 2012.
Makamu wa Rais wa Jamhuri ya Muungano wa Tanzania, Dkt.Mohammed Gharib Bilal,
akisalimiana na Muumin wa dini ya kiislam kutoka Msikiti wa Suni Hanafi wa jijini Dar es
Salaam, Muzamil Chaki, baada ya muumini huyo kumaliza kutoa burudani ya Qaswaida jukwaani, wakati wa mkesha wa sherehe za Mauilid zilizofanyika katika Viwanja vya Mnazi Mmoja jijini jana usiku Februari 04, 2012.Picha na Muhidin Sufiani-OMR
Mzee Lowassa hapo nakuvulia kofia, yaani una ratiba ya shughuli zote za dini zote!
ReplyDeleteJaribu kupata na sherehe wa Wahindu ukamilishe ratiba yako
Lowassa kiboko, duh! Ungepiga basi na kofia kama Lyatonga.
ReplyDeletebig up lowasa wetuuu
ReplyDeleteMheshimiwa Lowasa kweli wewe ni mtu wa watu licha ya magumu yote unayozushiwa. Usife moyo ipo siku.
ReplyDeleteDuh! Jamaa kweli anautaka u prezdaa.
ReplyDeleteMtumaini Mungu. Ikiwa imeandikwa, hakuna kilichoko chini ya jua kitakachokuzuia. Mengine yooote ni maneno, ambayo, kama bin-
ReplyDeleteAdam kamwe hutaweza kuwachagulia ya kuongea!
Lowassa ahsante kwa kuthamini na kujali Imani mbali mbali za Dini!
ReplyDelete