Mkurugenzi Mkuu wa Mfuko wa Taifa wa Bima ya Afya,Emanuel Humba akitoa maelezo ya Mradi wa Mama Mjamzito na Mtoto Mchanga mkoani Tanga wakati wa uzinduzi wa mradi huo kwa wadau mbalimbali wakiwemo wafadhili wa mradi huo ambao ni Benki ya Ujerumani (KfW).
Mkuu wa Mkoa wa Tanga,Mh. Chiku Gallawa akiteta jambo na Mkurugenzi Mkuu,Emanuel Humba. kushoto ni Mwakilishi wa KfW,Dk Kai Gesing.
Naibu Mkurugenzi Mkuu wa NHIF, Hamis Mdee akifafanua jambo kwa Mkurugenzi Mkuu wa Mfuko huo Emanuel Humba kabla ya uzinduzi.
Mkurugenzi wa Uendeshaji wa NHIF, Eugen Mikongoti kulia na Meneja wa Kanda ya Kaskazini Mashariki,Chris Mapunda wakifuatilia hotuba ya Mkuu wa Mkoa.
Akina mama wajawazito ambao tayari wameanza kunufaika na mradi huo kwa kupata matibabu kupitia Kitambulisho cha NHIF.
Mkuu wa Mkoa wa Tanga,Mh. Chiku Gallawa Akikabidhi kadi kwa akina mama wanaonufaika na mradi huo.

Michuzi Blog

Tanzanian blog operating since 2005, covering International news and Local News, including Politics, Fashion, Social Scenes, Interviews, Movies, Events, personalities and anything positive happening worldwide. Written in Swahili and English targeting both Swahili and English readers.

Toa Maoni Yako:

Kuna Maoni 2 mpaka sasa

  1. Natambua kuwa mfuko huu upo serikalini, je huduma hii ni kwa wajawazito na watoto wasio wanachama? Je huduma hii ni ya kudumu au ya muda tu kwa mama wajawazito na watoto.Je kuna kiasi chochote cha pesa kinachotolewa kila mwezi au ni bure?

    ReplyDelete
  2. huo mradi kwa Tanga tu na Da es Salaam unakuja?nomba utujuze kaka michuzi kwa wajazito DSM tunapata shida sana

    ReplyDelete

Hii ni Blog ya Watanzania popote walipo duniani kwa ajili ya kuhabarisha, kutoa/kupokea taarifa na kuelimisha mambo yote yaliyo chanya kwa Taifa letu. Tafadhali sana unapotoa maoni usichafue hali ya hewa wala usijeruhi hisia za mtu/watu. Kuwa mstaarabu...