Mshambuliaji wa Timu ya Zamalek, Amr Hassan Zaki, akipiga shuti lililompita mlinda mlango wa Yanga, Shaaban Kado na kutinga wavuni na kufanya matokeo kuwa 1-1 yaliyodumu mpaka mwisho wa mchezo.
Wachezaji wa Zamalek wakipongezana mara baada ya kusawazisha bao lao.
Hivi ndivyo matokeo yalivyokuwa mpaka mwisho wa mchezo wa leo.
Kocha Mkuu wa timu ya Zamalek,Hassan Shehata akizungumza na vyombo vya Habari mara baada ya kumalizika kwa mchezo wa leo,ambapo amesema kuwa Yanga ni timu nzuri na si ya kuibeza kwani wanacheza mchezo mzuri sana na wanajipanga kwenye mchezo wao wa marudiano.
Maskini Yanga...Miaka 77 hiyo.Msikate tamaa mnaweza kuwafunga kwao lakini siyo kwa maneno ni kukomaa.Mechi inaweza kuchezwa nje ya Misri au Misri kwenye uwanja mtupu.Kazi ni kwenu.
ReplyDeleteDavid V
Hapo hakuna kitu. Yanga heri wabakie bongo kuendelea na ligi ya Bongo!
ReplyDeleteNdo mjuwe kuwa uchawi na kipaji ni vitu viwili tofauti. Nawashangaa sana wabongo wanaoshupalia huu mpira wa mwaka 47. Tanga haina wachezaji kweli, wote wale ni wachawi tu, we umeona wapi watu wanacheza tu mpira bila formation halafu utegemee kushinda, si ujinga huu. Yanga na Simba ndiyo wanaua mpira bongo. Wanashindwa kuangalia timu za mikoani zinavyocheza kwa kutumia formation wao bado wanakalia uchawi tu matokeo yake Tz tunaonekana hatujui mpira kumbe hizi timu zinatuua.
ReplyDeleteShughuli ya Yanga imeishia hapa, ngojeeni fitina za ligi ya TZ muwakilishe mwaka mwingine.
ReplyDelete