Mdau akipumua baada ya kupanda mahindi katika shamba lake Moshi vijijini, tayari tayari kwa msimu wa kilimo ambapo msimu wa kilimo cha masika ambapo wananchi wa mkoa wa \kilimanjaro wako mstari wa mbele kuwania faida za mvua ndefu zinazoanza mwezi huu
 Kilimo kwa mistari
Kilimo mkoani Kilimanjaro

KWA HABARI KAMILI KUHUSU MSIMU WA 
MVUA ZA MASIKA MSIMU HUU

Michuzi Blog

Tanzanian blog operating since 2005, covering International news and Local News, including Politics, Fashion, Social Scenes, Interviews, Movies, Events, personalities and anything positive happening worldwide. Written in Swahili and English targeting both Swahili and English readers.

Toa Maoni Yako:

Kuna Maoni 5 mpaka sasa

  1. Kabla sijafika mkoa wa Kilitime nilidhani hawa jamaa ni maarufu kwenye biashara tu,na elimu na nilidhani ni wavivu..Hawa jamaa kwenye Kilimo wako fit ni kishenzi.Nenda huko vijini huko ndani..asubuhi wanaamkia kwenye Mashamba.Mbege hiyo wanakunywa kwa adabu mara nyingi ni saa za mchana baada ya shuguli za Mashambani.Ila usiku vijijini wanalewa vibaya sana...wengine wanaimba njiani.Kuna na kelele za KOMBA basi inapendeza.Wale tuliokulia vijijini tunaifahamu sana hii ya kuimba njiani kwa walevi.

    David V

    ReplyDelete
  2. Jembe la mkono katika karne ya 21, bado tuko nyuma sana!

    Tungewapatia wakulima hawa vifaa vya kilimo vya bei nafuu ambavyo vingeweza kuwasaidia kwa kweli tungepiga hatua kubwa sana.

    Hongera kwa kufanikisha kazi ngumu ya kilimo bila ya kukata tamaa.

    ReplyDelete
  3. Kilimo cha namna hii hakitatupeleka mbali. Kuna wasomi wengi wenye "Ph.D" (za kweli na za kununua internet) kwenye serikali yetu, lakini hakuna hata mmoja aliyewaambia kuwa "economies of scale "haipatikani ukilima heka tano na jembe. "Kilimo Kwanza" kinahitaji ardhi kubwa, fedha na trekta pamoja na elimu ya kilimo.

    Huyu mwanakijiji pengine hata darasa la saba hajamaliza na analisha watu 20 na ardhi hii. Atatajirika lini?

    Pia, umuhimu ni kuzingatia kuwa hakuna hata nchi moja duniani imekuwa tajiri kwa kuuza mazao ya kilimo. Utajiri unatokana na elimu ya juu kutumika kujenga viwanda na kuzalisha bidhaa na kuuza nje kama magari. Kilo moja ya machungwa ni dola moja, gari mmoja la kawaida ni dola 10,000. Nani atatajirika haraka?

    ReplyDelete
  4. Ardhi ililaaniwa tangu awali mapato yake ni kwa jasho na malipo yake ni kidogo,tuwaunge mkono wakulima kwa kuwape vifaa na pembejeo.Kipindi hiki wakuu wa nchi wamekaa kimya hakuna anayemsaidia mkulima lakini mavuno yakipatikana wanapanga bei.

    ReplyDelete
  5. NI kweli kilimo cha jembe la mkono hakiwezi kutupeleka mbali, ila kutokana na mazingira sehemu zingine ni ngumu/haiwezekani kulima kwa kutumia trekta/power tiller. labda mchangiaji hapo juu atueleze tutumie nyenzo gani kulima kwenye miteremko ya mlima kilimanjaro au kule kwenye milima ya upare. inabidi tusilaumu au kushutumu kila kitu wengine wanachofanya bila kujua hali halisi ya eneo husika.
    sehemu zilizoonyeshwa kwenye picha sio sehemu ambazo wakazi wa huko wanalima kwa ajili ya biashara bali ni kwa ajili ya matumizi yao. sehemu zinazoliwa kwa biashara ni moshi chini, tambarare za kia na vifaa vya kisasa kama matrekta ndio vinavyotumika

    ReplyDelete

Hii ni Blog ya Watanzania popote walipo duniani kwa ajili ya kuhabarisha, kutoa/kupokea taarifa na kuelimisha mambo yote yaliyo chanya kwa Taifa letu. Tafadhali sana unapotoa maoni usichafue hali ya hewa wala usijeruhi hisia za mtu/watu. Kuwa mstaarabu...