MGOMBEA wa CCM uchaguzi jimbo la Arumeru Mashariki, Sioi Sumari
Sioi akiwa na baadhi ya viongozi wa mkoa wa Arusha na Wilaya ya Arumeru alipopita Ofisi ya Makao Makuu ya CCM, Mtaa wa Lumumba Dar es Salaam leo muda mfupi baada ya CCM kumtangaza kuwa mgombea wake baada ya uamuzi wa Kamati Kuu leo.

Michuzi Blog

Tanzanian blog operating since 2005, covering International news and Local News, including Politics, Fashion, Social Scenes, Interviews, Movies, Events, personalities and anything positive happening worldwide. Written in Swahili and English targeting both Swahili and English readers.

Toa Maoni Yako:

Kuna Maoni 11 mpaka sasa

  1. Hongera Kijana.Lakini nyie viongozi wetu.Kwa nini msifikirie Mbunge akishwinda kuendelea na majukumu yake ama kwa kifo,au kuugua,n.k badala ya kuingia gharama nyingine za uchaguzi yule aliyeshika nafasi ya pili katika uchaguzi uliopita achukue hiyo nafasi moja kwa moja na hilo fungu la uchaguzi liende kwenye shughuli za maendeleo katika jimbo hilo au Rais ateu mbunge wa kutoka wabunge wa viti maalum(wako wengi sana)?Serikali ibane matumizi jamani.Nawasilisha.

    David V

    ReplyDelete
  2. ccm hata wakisimamisha jiwe kugombea basi kaa ukijuwa ushindi upo tu

    ReplyDelete
  3. MDAU MBANA MATUMIZI Dr. David V, TATIZO NI KWAMBA WATU WATAANZA KUUWANA ILI KUCHUKUA NAFASI YA MAREHEMU BAADA YA MAZISHI.KURUDIA TENA UCHAGUZI KUNAIMARISHA DEMOKRASIA NA KUNATUNZA UHAI WA MTANZANIA. MSHIDI WA PILI ANATAKIWA KUNADI SERA UPYA BADALA YA KUFIKIRA KUKATISHA MAISHA YA WATU, JAPO SIO WOTE WAPO HIVYO. ILA UTAMADUNI MPYA UNAWEZA KUZALIWA.KUMBUKA SIASA IS THE DIRTY GAME.

    MZEE WA BUSARA

    ReplyDelete
  4. Asante mzee wa Busara nimekuelewa.Kweli utamaduni mpya unaweza kuzaliwa na hasa Tanzania,kumbe bora tuendelee kufanya chaguzi mpya,tusiombee wabunge wetu washindwe kuendelea na majukumu yao.Nilikuwa sijaliona hilo.Asante mkuu.

    David V

    ReplyDelete
  5. Hivi hawa watoto wa vigogo hawajosoma nini, mbona wanang'ang'ania tu kututawala kama baba zao? Watoto wetu sisi hawata pata fursa ya kuwa viongozi nchi hii, angalia Vita Kawawa, Januari Makamba, Nape Nyahue, Adam Malima,Hussein Mwinyi,n.k

    Angalau tungepata mtoto mmoja wa Nyerere mwenye akili kama ya baba yake.

    ReplyDelete
  6. nivizuri kuona vijana wanagombea uongozi likini nina wasiwasi kama hawa jamaa wanauzoefu(work experiances) kwenye private sectors au government kwa muda ili waende bungeni na kufanya mabadiliko ya kweli sio kupokea posho tu

    ReplyDelete
  7. Tatizo kigezo cha kuwa mbunge ni kujua kusoma na kuandika ndhani tungeenda zaidi na AWE NA UZOEFU WA KUFANYA KAZI KTK SECTA BINAFSI AU SEKTA ZA SERIKALI kama hana sifa basi AWE ANGALAU AMEFANYA BIASHARA AMBAYO IMECHANGIA KTK KUKUZA UCHUMI, vinginevyo tutakuwa tunaongeza wabunge ambao wengine kuchangia issue mbalimbali itakuwa kazi kwa kuwa hawana uzoefu wa chochote kati ya hivyo nilivyovitaja, uongozi unaanza kwanza sehemu tunazofanyia kazi kisha tunapanda juu, sio mtu anakuja anatupa story za aliwahi kuwa Head boy au Mwenyekiti wa darasa Form IVA

    ReplyDelete
  8. Wachangiaji mliotangulia mmenifurahisha, mnatoa mawazo yanayoelimisha na kujenga, binafsi mie mengi nilikuwa sijayaangalia kwa upana huo. Asanteni

    ReplyDelete
  9. Patachimbika huko alumeru.

    ReplyDelete
  10. ..........kambi yetu inazidi kuimarika

    ReplyDelete
  11. This comment has been removed by a blog administrator.

    ReplyDelete

Hii ni Blog ya Watanzania popote walipo duniani kwa ajili ya kuhabarisha, kutoa/kupokea taarifa na kuelimisha mambo yote yaliyo chanya kwa Taifa letu. Tafadhali sana unapotoa maoni usichafue hali ya hewa wala usijeruhi hisia za mtu/watu. Kuwa mstaarabu...