Familia ya Bwana Gabriel Mponzi wa Oysterbay,Jijini Dar-es-salaam.Wanasikitika kutangaza kifo cha mpendwa mtoto wao Jane Mponzi “Mama Melanie” pichani kilichotokea siku ya jumapili tarehe 4/3/2012 katika Hospitali ya Agha Khan Dar-es-salaam.

Ibada ya kumuaga marehemu itafanyika Jumanne tarehe 6/3/2012 nyumbani kwa marehemu Oysterbay, Dar-es-salaam kuanzia saa 6 mchana na marehemu atazikwa Ipamba-Tosamaganga, Iringa siku ya Jumatano tarehe 7/3/ 2012.

Kwa maelezo zaidi kuhusu ratiba ya mazishi, wasiliana na mwenyekiti wa kamati ya maandalizi Dr. Ponziano Mponzi kupitia namba 0767 600 604.

Ndugu, jamaa na marafiki waliopo mbali, wanaweza kutuma michango yao ya kufanikisha safari ya mwisho ya kwenda kumlaza mpendwa wetu mkoani Iringa kupitia:

M-PESA- 0756 -999-900

TIGO PESA- 0713 -123- 617

AIRTEL MONEY- 0784- 615-566

Bwana ametoa na Bwana ametwaa,Jina la Bwana lihimidiwe.

Amina.

Michuzi Blog

Tanzanian blog operating since 2005, covering International news and Local News, including Politics, Fashion, Social Scenes, Interviews, Movies, Events, personalities and anything positive happening worldwide. Written in Swahili and English targeting both Swahili and English readers.

Toa Maoni Yako:

Kuna Maoni 20 mpaka sasa

  1. Rukia MfundaMarch 05, 2012

    RIP Jane Mponzi. Poleni familia ya Mponzi, Mungu awape imani na nguvu katika kipindi hiki kigumu. Bwana ametoa na Bwana ametwaa, Jina la Bwana lihimidiwe. Amina

    ReplyDelete
  2. Bwana ametoa na Bwana ametwaa Jina la Bwana lihimidie Tulikupenda sana Mpedwa wetu Jane ila Mungu anakupenda zaidi

    ReplyDelete
  3. R I P Jane kipenzi cha wengi

    ReplyDelete
  4. Vickie ChellouMarch 05, 2012

    Rest in peace love,Jane utakumbukwa sana

    ReplyDelete
  5. mungu akujali mapumziko ya amani Jane! nakumbuka tulivyokuwa wadogo jamani heeeee! lakini ndio hivyo kila nafsi itaonja mauti!

    ReplyDelete
  6. Poleni wafiwa may she RIP

    KWANINI hamumuziki next kwa marehemu mumewe? najua mumewe Herry Makange alifariki 32 days baada ya ndoa yao na kuzikwa Kibaha.

    nimesikia huruma kwa nini hamumuziki pamoja na mumewe, labda nae angefurahia as mumewe alifariki end 2008.

    nauliza tu, maana pia ni karibu na Dar. Poleni

    ReplyDelete
  7. Poleni sana familia ya Mponzi,ndugu,jamaa na marafiki.

    RIP "Mama Mela"

    David V

    ReplyDelete
  8. RIP dear jane,smile and keep on smiling.for yourlife was with a smile.your in him that grants me and strength and everlasting life
    baba s

    ReplyDelete
  9. Poleni sana familia ya Mponzi,Mzee Mponzi,Grace,Benny,Mellanie na wengine wote,mungu awape nguvu,subira na imani katika kipindi hiki kigumu cha majonzi.This world is not our home we are just passing through.
    Rest in peace love "mama" Mellanie
    Abbu Omar,Tokyo,Japan.

    ReplyDelete
  10. Dennis LondoMarch 05, 2012

    RIP Jane, kipindi kifupi tulichosoma wote pale Jitegemee JKT nilipata bahati ya kipekee kukufahamu kama mtu wa watu. Ucheshi, upendo na ukarimu wako kwa kila mtu ilikuwa ni sifa kuu uliyonayo. Umetangulia nasi tupo njiani. RIP Jane.

    ReplyDelete
  11. tulikupenda lakini Mwenyezi Mungu amekupenda zaidi. Pole nyingi kwa familia.
    Pumziko la milele umpe ee bwana na mwanga wa milele umuangazie, apumzike kwa amani. AMINA.

    ReplyDelete
  12. jamani so cute RIP japo sikufahamu, mtuambiege basi kilimsibu nini mpendwa wetu

    ReplyDelete
  13. R.I.P Jane poleni familia ya Mponzi mwenyezi mungu awape nafuu ya machungu, uvumilivu na faraja wakati huu mgumu.

    ReplyDelete
  14. Kazi ya Mungu, Haina makosa. RIP mama Melanie. Raha ya Milele umpe ee bwana na mwanga wa milele umwangazie apumzike kwa amani, AMEN.

    ReplyDelete
  15. Jane alikuwa jirani yetu kule Oysterbay, Msasani road. Pole sana Grace na familia yenu yote. Rest In Peace Jane.

    ReplyDelete
  16. Nimesikitika kwakua marehemu Kheri makange nilimfahamu jamani inauma sana hasa mtoto wao kubaki yatima. naomba anayejua atujuze nini kimemuu.

    ReplyDelete
  17. RIP Jane, you will be missed for your good heart.

    ReplyDelete
  18. My schoolmate at Oysterbay Primary, may you rest in peace.

    ReplyDelete
  19. it was a sudden death caused by heart attack

    ReplyDelete
  20. Pumzika kwa amani Jane, family yenu naijua vizuri, umelala karibu na mama yako jamani!!!

    ReplyDelete

Hii ni Blog ya Watanzania popote walipo duniani kwa ajili ya kuhabarisha, kutoa/kupokea taarifa na kuelimisha mambo yote yaliyo chanya kwa Taifa letu. Tafadhali sana unapotoa maoni usichafue hali ya hewa wala usijeruhi hisia za mtu/watu. Kuwa mstaarabu...