Waziri wa Maendeleo ya Mifugo na Uvuvi, Dk. David Mathayo David ( kulia) akisikiliza hoja mbalimbali za wafugaji wa jamii ya kimasai wa Kijiji cha Wami Sokoine, Wilayani Mvomero, Mkoani Morogoro alipofanya ziara ya siku moja kusikiliza kero na kutoa majawabu ya msingi kwa jamii hiyo.
Waziri wa Maendeleo ya Mifugo na Uvuvi, Dk. David Mathayo David ( kushoto) akiongozana na Mmoja wa Maofisa wa Mkuu wa Uzalishaji wa Tendaji Trading ,Alon Hoven,( kati kati) kwakitoka kuangalia hali ya mitambo ndani ya Kiwanda cha Tanzania Pride Meat, ambacho kimesimamisha uzalishaji wa nyama kwa muda mrefu ( wa kwanza kulia ) ni Mwenyekiti wa CCM Wilaya ya Mvomero, Pololet Mgema, Kiwanda hicho kwa sasa kimepata wawekezaji wapya wa Kampuni ya Tendaji Trading na The Zubair Corporation na kipo eneo la Nguru wa Ndege, Wilaya ya Mvomero, Mkoa wa Morogoro.
Waziri wa Maendeleo ya Mifugo na Uvuvi, Dk David Mathayo David ( kulia) akibadilishana mawazo na baadhi ya wawekezaji wapya wa Kiwanda cha Pride Meat wa Kampuni ya Tendaji Trading na The Zubair Corporation, ( wa kwanza kushoto) ni mmoja wa Maofisa Wakuu wa Uzalishaji wa Tendaji Trading , Eran Hovev.Waziri huyo alikitembelea Kiwanda hicho kilichopo eneo la Nguru wa Ndege, Wilaya ya Mvomero, Mkoa wa Morogoro.Picha zote na John Nditi wa Globu ya Jamii,Morogoro.

Michuzi Blog

Tanzanian blog operating since 2005, covering International news and Local News, including Politics, Fashion, Social Scenes, Interviews, Movies, Events, personalities and anything positive happening worldwide. Written in Swahili and English targeting both Swahili and English readers.

Toa Maoni Yako:

Kuna Maoni 1 mpaka sasa

Hii ni Blog ya Watanzania popote walipo duniani kwa ajili ya kuhabarisha, kutoa/kupokea taarifa na kuelimisha mambo yote yaliyo chanya kwa Taifa letu. Tafadhali sana unapotoa maoni usichafue hali ya hewa wala usijeruhi hisia za mtu/watu. Kuwa mstaarabu...