Meneja Uhusiano wa Airtel Tanzania Jackson Mmbando akikabidhi moja kati ya kompyuta 20 zilizotolewa na Airtel kwa chuo kukuu cha Dodoma (UDOM) kwa Makamu Mkuu wa chuo hicho Profesa Idrisa Kikula (kulia) jana wakati wa hafla fupi ya makabidhiano iliyofanyika chuoni hapo. anaeshuhudia ni Mkuu wa wilaya ya Bhahi Bi Betty Mkwasa (kati). Airtel imetoa vitabu 104 na computer 20 vyote vina thamani ya milioni 25/- TZS ikiwa ni muendelezo wa Airtel katika kuchangia sekta ya Elimu nchini.
Mkuu wa wilaya ya Bhahi Bi Betty Mkwasa, akiwa na Makamu Mkuu wa chuo cha Dodoma (UDOM) jana pamoja na wafanyakazi wa Airtel na baadhi ya wanafunzi wa IT chuoni hapo wakiwa wameshikilia vitabu vilivyotolewa msaada na Airtel kwa chuo hicho wakati wa hafla fupi ya makabidhiano ya vitabu 104 na kompyuta 20 vyote vyenye thamani ya milioni 25/- TZS toka Airtel ikiwa ni muendelezo wa Airtel kuchangia sekta ya Elimu nchini.
Mko juu Airtel..Nimewakuta jijini Ouagadougou,Burkina Faso.Line ile ile ya TZ....rate zile zile za TZ..Keep it up
ReplyDeleteDavid V