Asalam Aleykum,
Kwanza kabisa namshukuru Allah kwa kutujaalia afya njema na kutuneemesha sote kwa neema ndogo ndogo na kubwa kubwa, kama ambavyo amekuajilia kutambuliwa kimataifa kwa kazi muadhama inayofanywa na blog ya jamii. Hongera kwako binafsi na wote wanaifanya blog ya jamii kuwa kikombe cha chai na pia msuwaki wa kabla ya kulala!
Hoja yangu ni kuwa nadhani sasa kuna haja ya kuwepo kwa Makaburi ya Taifa ya Watu Mashuhuri waliotoa michango mikubwa kwa taifa letu.
Naandika hili nikiwa nimeguswa sana na kifo cha Marehemu Steven Charles Kanumba, kijana ambaye Taifa limemkubali kuwa ni Mtu Mashuhuri.
Nadhani ni vema watu wanaostahili kuendelea kuenziwa kwa michango yao kwa Taifa wakawa na mahali maalumu kitaifa pa kupumzika milele.
Naomba kuwasilisha hoja na kama hoja hii ina mshiko basi naviomba vyombo vinavyohusika viifanyie kazi maramoja.
Mdau Issa Majid Maggidi


Ingefaa Tanzania isondoke katika misingi ya usawa. Binafsi siafiki wazo hili
ReplyDeleteMakaburi ya watu maarufu ni wazo la kitoto sana.
ReplyDeletehakuna hata haja ya kujadili !!
mtu maarufu kuliko wazazi wa mtu ni mtu wa aina gani ??
Kifo ni kifo na ndio haki ya mtu yeyite dunia nzima , ni zawadi ambayo kila mtu ataipata ..
MAKABURI YA WATU MAARUFU NI YALE YA WAZAZI POPOTE YWALIPO.''ni mawazo yangu ''
Nawaunga mkono comment no1&2.Hakuna haja.Toa mawazo hayo kabiisa
ReplyDeleteNyerere was a champion of social justice .Every body is equal hata hapa USA hakuna hayo . Michael Jackson amezikwa na watu wa kawaida tu ila location ya kaburi hilo lilipo ndio bei . Haya mambo ya umaarufu yameanza lini . Nyerere founded this country na hatukuwa na hayo . Good suggestion but azikwe kwenye nyumba yake kama wanaogopa mwili wake kuibiwa .
ReplyDeleteMdau Issa Majid Maggidi Muogope mola wako ndugu yangu. Makaburi ya watu mashuhuri yatatusaidia nini ndugu yangu? huu ndo mwanzo wakuanza kuabudu makaburi sasa. Kuna watu muhimu kama mitume wa mwenyezi mungu humu ulimwenguni? i.e, Mussa, Ibrahim, Yahya (John the Baptist) na wengineo wengi tu hatujui makaburi yao yako wapi! (Sijamtaja Muhammad kwa kua tunajua kaburi lake liko wapi) Mtazamo wako unaonekana umekuwa ni wa hisia (Emotional) zaidi kulikoni kuangalia why we need makaburi ya watu unaodai ni mashuhuri. Kumbuka mashuhuri kwako anaweza kua si mashuhuri kwa wengine.
ReplyDeleteMajid wewe tutakuzika Nyeregete tu!Lol
ReplyDeleteMungu alitaka wote tuwe sawa ndo maana wote tunaingilia sehemu moja tokea hapohapo na wote tutaonja mauti, sasa mambo gani tena ya kuanza kutengana oooooooh hawa wanajulikana sana na michango yao ni minene ktk jamii ivo wapewe kipaumbele juu ya wapi miili yao italala.huu ni ubaguzi. ni mawazo yangu.
ReplyDeleteHuyu mtu alietoa wazo hili sababu ya kifo cha Kanumba nadhani hana akili nzuri, kanumba ni maarufu na wala si Mashuhuri ajaribu kutofautisha hayo, wapo watu mashuhuri waliofanya hata wewe uweze kupata nafasi ya kutoa mawazo yako hapa kwa uhuru leo lakini hawajapata nafasi ya kulala sehemu ya watu mashuhuri unayoitaka wewe, sote tunasikitika na msiba wa kanumba, sidhani ni kwasababu alikuwa mashuhuri bali sababu ilikuwa ghafla mno. Alale pale panapostahili binadamu kulala maana "Umashuhuri kaburini hausaidii"
ReplyDeleteMtu akishakufa umaarufu wake ndiyo umeishia hapo.
ReplyDeleteHuko tuendako sote tuko sawa mbele ya Mwenyezi Mungu.
Mie naona Bw. Issa amechanganyikiwa na kifo cha Kanumba. Kwanza hamna neema ndogo na kubwa bali neema ni neema tu. Pili hamna mtu maarufu aliyekufa, uaarufu ukiwa hai. Ukishaaga dunia ndo basi. Ni kufuru hata mbele ya Mungu na ni kuchochea matabaka ktk jamii.
ReplyDeletewatu siku hizi wanajengewa marumaru ya ghotofa kutoka ardhini. Unataka nini tena zaidi. Kila wiki kuna change of flowers. umaarufu gani tena unataka nenda katembelee kinondoni, pale mbuzi haingii kula majani. Unataka kjuongeza kufuru nyingine. Mwisho wa siku inabaki mifupa firauni ndio alieahidiwa kuwa ushahudi wa uweza wa Mwenye Mungu subhana kwamba hautaoza maisha.
ReplyDeleteMijitu ya ya namna hii ndio inarudisha nyuma maendeleo ya ulimwengu huu, litazame kwanza eti tuwe na makaburi ya watu mshughuri. Kubwa zima hata dini yako huijui. Hawa ndio mwisho a siku watakuja kusema utumwa ni bora kuliko kuwa huru mawazo kama haya Michuzi next time usiwe hewani maana unaharibu hata thamani ya blog yako kwa kweli. Thanks
ReplyDeletekaka naona umeanza kuchanganyikiwa..kuna mtu mashuhuri zaidi ya wazazi wa mtu au wanae?
ReplyDeleteBasi tafuteni hata nchi ya watu mashuhuri. Kweli huu ni uzoba wa hali ya juu. Hao watu mashuhuri ni wapi zaidi ya kuwa mafisadi na wachafuzi wa maadili kama Kanumba.
ReplyDeleteDuh! hii kali kwa kweli. Tunaanza kubagua hata wafu?, maana duniani huku kuo ndiyo mchezo utasikia masaki, oysterbay. Kwa kweli mtu akiisha fariki anabaki yeye na mungu wake ukimzika majini, jangwani au kaburi la dhahabu he's gone.
ReplyDeleteAlizikwa Dr Omary ali Juma (makamu wa rais) kijiji kwao Wawi tena kwa kutumia jeneza lilelile na shuka ileile iliyochanika wanayoitumia wengine. Huu umaarufu tuufanyie duniani mbele ya mungu maarufu ni yule aliyeishi duniani kwa misingi anayotaka mwenyezimungu.
kaka naona umechanganyikiwa!!!
ReplyDeleteWhat a load of bullshit. Huyu aliyeandika haya makala atakuwa hana akili hata chembe! Kwanza huyo anayesema anayemsema mtu 'mashuhuri' alikuwa anatoka na binti aliyekuwa "under age" (kwani walianza kabla ya mwaka huu). Sasa ni maadili gani hayo ya ku-deserve "umashuhuri" au u-role model? Sina kusudi la kumlaumu marehemu, lengo langu ni kukuonyesha kwamba binadamu wote ni sawa na hakuna aliye mkamilifu. Kila binadamu ana mazuri yake na mapungufu yake, na yule ambaye wewe unamwona 'mashuhuri' kuna wengine wanamwona wa kawaida tu kwa sababu kama nilizozitaja hapo juu.
ReplyDeleteKuna watu huko TZ wanahangaika jinsi ya kupata elimu kwa kuwa hata uwezo wa kununua vitabu na madaftari hawana ukiachilia mbali school fees au hata mlo wa siku, halafu leo wewe unatuletea 'upuuzi' huu?? Kweli saa nyingine inafika wakati unaona ni jinsi gani sisi waTanzania tumelala! Kazi kuabudu 'ucelebrity' tu! Grow up man. Unaopaswa kumwabudu Mola peke yake!!
Kaburi ni kaburi tu, hakuna umashuhuri,
ReplyDeleteHumo enda kila mtu, na sote yetu safari,
Cheo mali siyo kitu, ni "amali' iwe nzuri,
Sianze gawanya watu, tamchukiza "Qahhari"
Hoja nyingine haina haja ya kuzileta humu, kama ni kifo watu wanafiwa na wapendwa wao wa karibu zaidi, achilia mbali hao watu maarufu au mashuhuri na wanazikwa popote pale almuradi kustirika kaburini, umashuhuri hausaidii kitu wala kutengewa sehemu ya watu mashuhuri hakusaidii lolote, kinachokufaa ni AMALI zako njema ulizozitenda duniani, mali na swahiba zako wote watakusindikiza na kurudi, lakini AMALI zako ziwe nzuri au mbaya, ndio zitakazokutendea haki huko, haijalishi umezikiwa kwenye eneo la watu mashuhuri au laa!
ReplyDeleteAcha mawazo yako ya kifisadi wewe Issa Majid Maggidi.
ReplyDeleteHuyu jamaa naona alikuwa anataka kuchokoza watu tu. Ila kama yuko serious na mawazo yake, basi namchukulia kama mtu mwenye mapungufu kifikra. Kimsingi mtu akishakufa amekufa. Hakuna kifo cha tajiri na cha masikini. Hivyo hata kwenye kuwazika hakuna sababu ya kuwagwa.
ReplyDeleteHata hivyo ukisema kanumba alikuwa mashuhuri naona unakosea. Kwa kawaida sisi binadamu tumekuwa na hulka ya kuwaona wasanii kana kwamba wao ndio watu watu mashuhuri tu. Hii ni kwa sababu fani yao inahitaji kujitangaza na hivyo wakajikuta wametazamwa na watu wengi na kuwafanya wajulikane zaidi. Kujulikana sana kunaweza kusifanye mtu aonekane wa maana kuliko wengine. Wapo watu ambao watoa mchango wao mkubwa sana kwa taifa hili na hakuna aliyewaita mashuhuri. Hata wanapokufa huwezi kuona kiongozi wa ngazi za juu amehudhuria mazishi yao hata kama alikuwa anawafahamu. Hii ni kwa sababu kazi zao hazikuwa za kuoneshwa kwa watu wengi.
Huyu Issa Majid Maggidi hajakosea sana. Kuna kitu alitaka kuwasilisha. Swali - Je ni kitu gani hicho? Inaonyesha ni msomi na si rahisi sana akakurupuka. Ukisoma kwa umakini utaona anaonyesha kutaka mchango wa mtu uthaminiwe au ukumbukwe. Ninafikiri angejiuliza swali kama -kuna umaarufu gani kwenye mwili mtu kabla hajahitimisha na makaburi ya watu muhimu. Ni kwa kiasi gani makaburi ya watu muhimu yatatoa msukumo chanya utakoweza kubadilisha mitazamo na tabia za watu waweze kuwaiga hao watu maarufu? Kama makaburi hayataweza ni kitu kipi kinaweza kufanyika kiwe kama kumbukumbu ya yale mema aliyoyafanya mtu?
ReplyDeleteEmmanuel
Jitu kama ili alishindwi kusema inatakiwa kuwe na club ya watu maarufu tu, bongo yenyewe hayo makaburi ya meshajaa kila sehemu
ReplyDeleteWewe Issa Majid nataka kukuuliza marehemu Kanumba alikuwa na umashuhuri gani kama si umaarufu?. alikuwa mashuhuri Nyerere aliyejulikana dunia nzima na kazikwa kwao butiama itakuwa Kanumba?.sasa kwa makosa ya kuleta mawazo yako finyu katika blog ya jamii adhabu yako ni kuwa ukifa tutakuzika kwenye dampo la Tabata au machinjio ya vingunguti. ffyyyyy msonyo.
ReplyDeleteHuyu jamaa mtoa mada ninawasiwai hili sio jina lake kaweka habari hii tu hapa kuoona nini reaction ya watu.
ReplyDeleteWEWE JAMAA TANZANIA SIO INDIA, KAMA ANGEKUWA YEYE MAREHEMU ANA KIWANJA CHAKE KIKUBWA AU SHAMBA ANGEZIKWA KWAKE HAYA MAMBO YAKO KIASILI HASA VIJIJINI,
ReplyDeleteMDAU KONGO
Kaka mjengwa mawazo gani hayo ndugu lol...mimi nilikuwa mpenzi wa blog yako ila kama ideas zako na uwezo wako wa kufikiri ndo kam huu...sisomi tena blog...kaka michuzi pleaseee next time usitulete mada za ajabu kam hii ya mjengwa
ReplyDeleteMDAU CANADA
Siungi mkono hoja.
ReplyDeleteHuyu Issa Majid Maggid hili siyo jina lake, na ukiwa na akili za kipolisi utagundua kwamba yeye huyohuyo baadaye akajiita Emmanuel na kutoa maoni kana kwamba ni mtu mwingine kabisa.
ReplyDeleteNdugu zangu katika Blog hii ya Jamii, Engineer Issa Majjid Maggidi (anaishi Dubai) namfahamu tokea tukiwa wadogo kule kijijini kwao Pongwe, Tanga. Huyu siyo yule Majid Mjengwa wa Nyeregete Village.
ReplyDeleteKama kweli huu ujumbe ameuandika yeye, basi atakuwa ameteleza tu kwani ana elimu zote (ya dunia na Dini yake).
Moja ya michango yake ya thamani katika blog hii ni ule uliohusu Jumuia Ya Afrika Mashariki takriban miaka 2 au 3 iliyopita, na kuungwa mkono na wengi wetu ikiwemo serikali yenyewe.
ISSA JITOKEZE KUTETEA HOJA YAKO.
Hamim - USA
Kwa hoja hii kuanzia leo nakubadilisha majina yako kutoka Mjengwa-Mbomoa na Mjid-kuwa Gaidi maana ni hoja ya kipuuzi mno.
ReplyDeleteHii hoja mdau kama ungeitafakari kwa undani zaidi wewe mwenyewe ungeona wala haina haja ya kujisumbua kuiweka hapa.
ReplyDeleteBinadamu wote sawa, ardhi ndio hiyo hiyo, udongo ni huo huo na safari ya mwisho kwa viumbe wote hai ni hiyo moja tu!
Kutenganisha huko sio tu ndio mwanzo wa kujenga matabaka katika jamii bali ni kudhalilisha na kushusha heshima ya utamaduni wetu.
Tuepuke kabisa mawazo kama haya yasiyo na faida yoyote.
Umenisikitisha saana wewe Issa Majid Maggidi. Hivi kuna kifo cha Mtu mashuhuri na mtu asiye mashuhuri? Unaweza sema sasa hata mtu mashuhuri azaliwe na watu maalumu.. Unaweza sema afanye kazi maalumu. aisee pole sana ndugu. nakushauri uondoe hili bango lako kwenye hii blog maana linazidi kukutweza. wewe si yule maggidi nnayemjua.
ReplyDeleteHope umeelewa!!
Mdau
Watu mashuhuri wa jinsi gani NGONO? KISIASA, KIELIMU, UTAJIRI AU kivipi? Binadamu wote ni sawa bana hakuna ataezikwa mbinguni jeuri ya binadamu ni kifo ndo mana hata ukiwa tajiri vipi utakwenda chini kama ulivyo zaliwa kila kitu utaacha duniani!
ReplyDeleteBRO, UMETUSIKITISHA SANA KUSEMA TAIFA LINAMTAMBUA KAMA MTU MASHUHURI HAPANA JAMAA NI MAARUFU TU HAPA TANZANIA SIDHANI KAMA LEO UKIMULIZA DAVID CAMEROUN UNAMJUA STEVEN KANUMBA ATASEMA NDIO, LAKINI YUMKINI UKIMULIZA UNAMJUA MWL.JULIUS KAMBARAGE NYERERE ATASEMA YES I KNOW HIM VERY MUCH. SASA HOJA YA KUWA NA MAKABURI YAO WATU MAARUFU HUO NI UTUMWA AMBAO TULIUPIGA VITA KWA NGUVU ZOTE HAKUNA MAARUFU, WALA MASHUHURI MBELE YA MWENYEZI MUNGU KILA MTU ATATOA HABARI ZAKE MWENYEWE KUWA ULIFANYA NINI HAPA DUNIANI HAIJALISHI ULIZIKWA KINONDONI AU MAKABURI MAARUFU UNAYOYASEMA. MWISHO KILA MTU UNAYEMUONA DUNIA HII NI MASHUHURI NA MAARUFU KWA WAKATI WAKE MBELE ZA MUNGU AWE KILEMA AU MZIMA WA VIUNGO KWA HIYO HOJA YAKO HUJAIPIMA HATA KAMA UMETAKA KUONA REACTION ZA WATU UNAONESHA JINSI GANI USIVYOPIMA UNACHOTAKA KUSEMA HAIJALISHI JINA NI LAKO KWELI AU LA MWENDAWAZIMU.
ReplyDeleteanaogopa kifo! Uwoga tu ndio unaosumbua huwezi kupingana na mungu akiamua jambo lake. Eti ooo mvalishe marehemu suti na kaburi jenga sementi kabisa ili mwili usiharibike. Tutarudi kwa udongo na kuoza kuko pale pale acha uoga.
ReplyDeleteHuyu Issa Maggigi?kwanini umetuchafua sisi Watanzania namna hii?hapa dunia tiishi kwa matabaka mpaka kwenye makaburi tena?This is very sad,itabidi uombe msamaha kwenye hii blogger.thanks mdau london.
ReplyDeleteKama kweli unhisi kuna kitu kizuri amekifanya, kuna namna ambavyo watu huenziwa wanapokufa. Tusubiri kama kuna ukumbi hata mmoja wa filamu utabaduilisha jina na Kuijiita Kanumba, au kama kuna uawanja wa Mpira wa miguu utaitwa Kanumba na ua kama Kuna bara bara itaitwa Kanumba. Hakuwa maarufu wala mashuhuri. Ni namna tu ya kifo ilivyotokea ndio imewafanya watu kuwa na huzuni sana. Emotions ndio zimewajaza watu pale uwanjani na nyumbani kwake. Emotions ndio na flow za kisiasa ndio zilizomfanya Rais awahi nyumbani kwa marehemu kusaini kitabu, na emotion hizo hizo ndio zimekufanya na wewe ukaandika mada hii. Kanisa Katoliki huwa lina utaratibu wa kutangaza watakatifu. Ili utangazwe kuwa ni mtakatifu, wanakuacha kwa miaka kumi baada ya kifo chako bila hata kukujadili ili mjadala juu yako unapoanza, emotions ziko chini na watu wanazungumza hali halisi, wakichambua mazuri yakio na mabaya yako. Leo mabaya ya Kanumba hayazungumzwi, kwa kuwa kila mtu yuko kwenye emotions.
ReplyDeleteTUWAWEKEE NA VIYOYOZI NA TV NDANI HALAFU KILA MMOJA ATAWEKEWA SATALITE DISH NJE YA KABURI AENDELEE KUWA UPDATED, UBAGUZI WA AINA GANI UMEPOST??? UNATAKA NDUGU WATAKAOBAKI WAENDELEE NA WAJISIFU KWA MAHALI JAMAA YAO ALIPOZIKWA KAMA VILE WATU WANAVYOJISIFU KUTOKANA NA MAKAZI WAKATI TUPO HAI. KWA MUNGU WOTE SAWA BROO
ReplyDeleteHOJA YA HAJA: TUWE NA MAKTBA KUU YA KILA ALIYEKUWA RAIS WA JAMHURI YA MUUNGANO WA TANZANIA
ReplyDelete