Laxim Darts Club ya Tukuyu (Wanyambala) wanawashukuru wale wote ambao wamechangia kwa hali na mali katika kupatikana kwa Jezi bin Uzi mpya wa Club kwa wachezaji wote wa darts. Wanachama na wachezaji wanawashukuru sana sana kwa michango yao na Mungu awaongezee zaidi ili waweze kutusaidia tea na tena, na wale ambao hawakupata nafasi wakati huu nao tunawaombea wapate na watusaidie. Ni juhudi zako Anko Michuzi kupitia blog hii ya jamii ulipotutoa mwaka jana mwishoni kuwa Laxim Darts Club wanaomba misaada ndipo wafadhili mbali mbali wamejitokeza.
Home
Unlabelled
Laxmi Darts ya Tokyo yatoa shukrani kwa waliotoa msaada wa Uzi Mpya
Subscribe to:
Post Comments (Atom)
sasa hii klabu ipo Tokyo Tanzania......au Tukuyu Japan. Au huko Tukuyu kuna Tokyo........hebu tuwekane wazi kipengele hiki
ReplyDeletehahaaa.. Tokyo ndo Tukuyu!!!.. duh!?
ReplyDeleteMdau kwa kukusaidia tu Tukuyu ndio Tokyo ya bongo kama ilivyo Segerea(Dar ) ambayo ni senegal, Bagamoyo= Baltimore, Kisarawe= Kingstone, Ukonga=UK ,Chanika=Charlote city, Loliondo=London, Arumeru=Armenia, list inaendelea mdau kaa mkao wa kula Lol.
ReplyDeleteYeah Banyamabala nawaona, chapa kazi. Dah nimemiss Laxmi Bar ngoja nije. Kocha
ReplyDelete