Mbunge wa Ludewa (CCM), Deo Filikunjombe akisaini karatasi inayokusanya saini za wabunge za kutokuwa na imani na Waziri Mkuu kwa lengo la kuwasilisha kwa Spika mjini Dodoma. Kulia ni Naibu Kiongozi wa Upinzani Bungeni, Kabwe Zitto.


UKUSANYAJI saini za wabunge kwa ajili ya kuwasilisha azimio la kutokuwa na imani na Waziri Mkuu umechangamkiwa lakini kuna mgawanyiko baina ya wabunge wa CCM kwa kuwa baadhi yao wanapinga azimio hilo. 

Hadi jana saa 9 alasiri, wabunge watano wa CCM ndiyo walikuwa wamesaini akiwemo Mbunge wa Ludewa, Deo Filikunjombe, aliyesaini akikanusha kutumwa na mtu kwa kusema hana haja na uwaziri, kama ambavyo baadhi ya wabunge walivyowatuhumu kuwa wanaoshinikiza azimio hilo wanataka uwaziri. 

Wanaoponda hoja hiyo wanasema haina mashiko, kwa kuwa Waziri Mkuu, Mizengo Pinda hahusiki na uteuzi wa mawaziri. 

Mbunge aliyezungumza hadharani na waandishi akipinga, ni wa Simanjiro, Christopher ole Sendeka (CCM) ambaye amemtetea Pinda kwamba ni mtendaji mzuri na hajavunja maadili yoyote kiasi cha kuruhusu hoja ya kumwondoa kuwa na mashiko. 

Mwenyekiti wa Kamati ya Bunge ya Hesabu za Mashirika ya Umma (POAC) na Mbunge wa Kigoma Kaskazini, Kabwe Zitto (Chadema) ndiye aliyeongoza kazi hiyo jana na hadi saa 9, zilishakusanywa saini 66 za wabunge kutoka vyama vyote isipokuwa United Democratic Party (UDP) ambacho mbunge wake ni John Cheyo ambaye pia ni Mwenyekiti. 

Akiongozana na Filikunjombe, Zitto aliwaambia waandishi wa habari kwamba hadi muda huo, idadi ya wabunge wa CCM waliosaini ni watano, CUF 12 na wengine ni waTLP, NCCR-Mageuzi na Chadema. 

BOFYA HABARI LEO KUSOMA ZAIDI

Michuzi Blog

Tanzanian blog operating since 2005, covering International news and Local News, including Politics, Fashion, Social Scenes, Interviews, Movies, Events, personalities and anything positive happening worldwide. Written in Swahili and English targeting both Swahili and English readers.

Toa Maoni Yako:

Kuna Maoni 1 mpaka sasa

  1. RAIS KAMA ANAIPENDA TANZANIA NA SISI WANANCHI WAKE AMABO TULIMTHAMINI SANA SANA NA KUMPA KILA AINA YA SUPPORT WA KIPINDI CHAKE CHA PILI NA CHA KWANZA, ALISAFISHE TAIFA. INCHI INADIDIMIA MIKONONI MWAKE. ONDOA MAWAZIRI AMBAO UTENDAJI WAO UNAMASHAKA, ACHA WALIO WEMA NA WACHAPA KAZI. LASIVYO WABUNGE WAKIENDELEA NA MALALMIKO YAO UTALAZIMIKA KUJA KULIVUNJA BILA KUPENDA.

    ReplyDelete

Hii ni Blog ya Watanzania popote walipo duniani kwa ajili ya kuhabarisha, kutoa/kupokea taarifa na kuelimisha mambo yote yaliyo chanya kwa Taifa letu. Tafadhali sana unapotoa maoni usichafue hali ya hewa wala usijeruhi hisia za mtu/watu. Kuwa mstaarabu...