Mtoto ISSA ISMAIL, UMRI – Miaka 14

Anasoma Kidato cha Kwanza- B Shule – Sekondari ya Pugu Station,Amepotea April 16 nyumbani kwao Gongolamboto mwisho wa lami. Aliondoka asubuhi saa 11:30 kuelekea shule na hajaonekana tena hadi leo.

Mara ya mwisho alikua amevaa nguo za shule shati nyeupe na suruali ya kaki Tunaomba yoyote atakayemuona atoe taarifa kupitia simu numba :

0656 986 836
0713 902 547
0782 275 621

Au atoe taarifa kituo chochote cha Polisi au kwenye mtandao wako. 

Asante!

Michuzi Blog

Tanzanian blog operating since 2005, covering International news and Local News, including Politics, Fashion, Social Scenes, Interviews, Movies, Events, personalities and anything positive happening worldwide. Written in Swahili and English targeting both Swahili and English readers.

Toa Maoni Yako:

Kuna Maoni 8 mpaka sasa

  1. Loh Poleni sana wazazi/walezi..hope atapatikana akiwa salama...Kwa sisi wazazi inaumiza kweli kwa sababu mtoto wa Form I kama huyu ana uwezo wa kujieleza kwao,wazazi wake, nk.Anapopotea inaleta mawazo mengine..Kitu kingine wazazi tuwe na kawaida ya kuwakaririsha watoto wetu wa umri huu namba zetu za simu..Kuna wakati watoto wanapotea,wanapatikana wanaulizwa unafahamu namba ya mama yako...??XXX,Unafahamu namba ya mama yako....?XXXX.Wale wadogo zaidi ndiyo hatari zaidi..nilipotelewa na mmoja ilikuwa hatari..akiulizwa kwenu ni wapi..Nyumbani..baba yako anaitwa nani...Baba..Mama yako??..Mama.

    David V

    ReplyDelete
  2. umri ni miaka 14 au 4??????????

    kama ni miaka 14, tunaomba icha ya sasa ili tukimuona tumtambue kwa haraka

    mdau

    Mnyagatwa USA

    ReplyDelete
  3. Inshallah atapatikana, ila picha mbona anaonekana mdogo kwa umri wa miaka 14? au hakuna picha zake za karibia na umri wa 14?

    ReplyDelete
  4. poleni sana ndugu zetu kwa hii taarifa, je hakuna picha ya hivi karibuni inayoonesha mtu mwenye umri wa miaka 14? kwani nona hii picha hapo juu niyakitambo kiasi. asante

    ReplyDelete
  5. Picha mbona haiendani na umri?

    Hivi mmeshindwa kupata picha yake ya sasa?

    Kwa nini?

    ReplyDelete
  6. Jamani picha zinapigwa wakati wa X-mas, ubatizo komunyo ya kwanza au kipaimara. Sasa tufanyeje hapa. Angalau kuna picha ila ni utata kumtambua kwa haraka.Hopeful atapatikana salama yarabi!
    Poleni wazazi wenzangu.

    ReplyDelete
  7. are you guys serious?

    ReplyDelete
  8. Tafuteni hata picha za pasport alizopeleka shuleni

    ReplyDelete

Hii ni Blog ya Watanzania popote walipo duniani kwa ajili ya kuhabarisha, kutoa/kupokea taarifa na kuelimisha mambo yote yaliyo chanya kwa Taifa letu. Tafadhali sana unapotoa maoni usichafue hali ya hewa wala usijeruhi hisia za mtu/watu. Kuwa mstaarabu...