Kwa niaba yangu binafsi na kwa niaba ya Wenzangu hapa Ubalozini napenda kutoa shukurani zangu za dhati kwa Watanzania wote walioshiriki kwa wingi katika Uchaguzi wa Viongozi wa Jumuiya ya Watanzania waishio Washington Metropolitan. Nimefurahishwa sana na moyo wa Umoja na Ushirikiano ulioonyeshwa na Watanzania wote waliojitokeza katika mkutano huo wa Uchaguzi.


Aidha napenda pia kutoa shukurani zangu za dhati kwa Kamati ya Mpito, chini ya Mwenyekiti wake Givens Kasyanju kwa kazi kubwa waliyoifanya ya kuandika Katiba mpya, kuandaa na hatimaye kusimamia kufanyika kwa Uchaguzi huu wa kihistoria wa Jumuiya ya Watanzania DMV. Asanteni sana.


Mwisho napenda kuwapongeza kwa moyo wa dhati Viongozi Wapya waliochaguliwa kuiongoza Jumuiya ya Watanzania DMV. Napenda kuwahakikishia ushirikiano usio na mipaka kutoka kwangu binafsi na kwa wenzangu hapa Ubalozini katika kufanikisha kila lililojema kwa manufaa ya Watanzania wote waishio DMV.


Mheshimiwa Mwanaidi Sinare Maajar


Balozi wa Tanzania Marekani na Mexico


Washington, DC.

Michuzi Blog

Tanzanian blog operating since 2005, covering International news and Local News, including Politics, Fashion, Social Scenes, Interviews, Movies, Events, personalities and anything positive happening worldwide. Written in Swahili and English targeting both Swahili and English readers.

Toa Maoni Yako:

Kuna Maoni 8 mpaka sasa

  1. Mh Balozi, tunashukuru kwa kazi nzuri unayofanya, natamani balozi zingine zingeiga mfano wako, Watanzania tunaoishi nje ya Bongo tungekuwa wamoja na tungewekeza nyumbani. Tuliona kazi yako ulipokuwa UK, na kazi imeanza US. Bahati mbaya US ni kubwa sana kulinganisha na UK,lakini tunaamini hautaishia kwa watu wa DC peke yake. Tupo majimbo tofauti na naomba uendeleze na majimbo mengine. Kuna watu wana taaluma mbalimbali na wenye mawazo mazuri ya kuondoa umaskini Tanzania,kwa kuwakutanisha na kuwapa changamoto,tutafanikiwa. Ni matumaini yangu serikali ijayo(Siyo hii iliyopoteza mwelekeo) itakuona na kukupa majukumu makubwa zaidi. Mungu akubariki mama na dada yetu.

    ReplyDelete
  2. nani ameimba huu wimbo ndugu zangu kwenye hii video. wimbo ni huu..

    NAKUPENDA TANZANIA...NCHI YANGU TANZANIA..MOYO WANGU HUJIVUNIA...MIMI NI MTANZANIA

    Nimeutafuta kwenye youtube nimeukosa. labda kwa vile sijui aliyeuimba.

    MSAADA TUTANI WAUNGWANA

    ReplyDelete
  3. Huu wimbo umeibwa na dada mmoja anaitwa Francia Chengula Mtanzania anyeishi UK, ameimba nyimbo nyingine unaitwa Mwanamke, angalia youtube http://www.youtube.com/watch?v=F390bwm2-Uo

    nenda itune na utafute francia Chengula, utapata wimbo huu wa Nakupenda Tanzania kwa bei rahisi

    ReplyDelete
  4. Francia Chengula anaishi UK, tafuta huu wimbo itune au Amazon MP3 utaupata. pia type jina lake youtube utaona video zake

    ReplyDelete
  5. kama kweli unataka mbona haujaweka contact zako ili upewe. ukigoogle Francia chengula utapata all the details na huo wimbo

    ReplyDelete
  6. Mdau hapa juu ,aliyeimba wimbo ni Iddiamini.

    ReplyDelete
  7. Michuzi nimemjibu huyu mtu hapo juu kuhusu nani kaimba huu wimbo lkn bado haujapost, mtangazie biashara mwanamuziki wetu. watu wasitumie tu wimbo wake halafu mumbaji hajulikani, naomba upost ile comment niliyojibu nani kaimba huu wimbo. Asante

    ReplyDelete
  8. SHUKRANI waungwana wote kwa msaada wenu. Nimepata kumuona dada yangu Francia Chengula. HATA HIVYO video ya WIMBO wake NAKUPENDA TANZANIA SIKUWEZA KUIPATA KWENYE YOUTUBE ZAIDI YA PALE ALIPOIMBA KWENYE MKUTANO WA DIASPORA LONDON. BUT ITUNE WEBSITE HELPED ME OUT BIG TIME. I GOT HER VOICE IN MY MUSIC BANK AS OF NOW. BY THE WAY....HONGERA WANA WA DMV KWA KUTEKELEZA DEMOKRASIA YA UCHAGUZI. I AM YOUR JIRANI IN OBAMALAND.

    ReplyDelete

Hii ni Blog ya Watanzania popote walipo duniani kwa ajili ya kuhabarisha, kutoa/kupokea taarifa na kuelimisha mambo yote yaliyo chanya kwa Taifa letu. Tafadhali sana unapotoa maoni usichafue hali ya hewa wala usijeruhi hisia za mtu/watu. Kuwa mstaarabu...