Kampuni mpya ya Kitanzania ijulikanayo kama Mobile Ticketing Limited kwa kushirikiana na Mitandao ya simu za mkononi Vodacom Tanzania,Airtel, Zantel na Makampuni ya Mabasi inayofuraha kuwatangazia watanzania wote kuwa hivi karibuni itazindua huduma mpya na rahisi ya kukata tiketi (ticket) za mabasi yaendayo mikoani na nchi Jirani kupitia simu ya mkononi.

 Huduma hii inajulikana kwa Jina la "Ticket popote" ni ya kipekee na ya kwanza kuzinduliwa hapa nchini Tanzania.

Mobile Ticketing Limited inatambua usumbufu waupatao abiria wakati wanataka kusafiri na mabasi ya Kwenda Mkoani na Nchi Jirani . Huduma hii inalenga kuondoa utaratibu wa kizamani uliokuwa na usumbufu ambapo abilia alitakiwa kufika kwenye ofisi za basi husika ili kukata ticket, kuzidishiwa nauli na madalali (wapiga debe) hasa wakati wa msimu wa sikukuu za mwisho wa mwaka, kuuziwa ticket moja mtu zaidi ya mmoja au kuuziwa ticket ya basi lisilokuwa na safari. 

Huduma hii mpya ya kukata ticket kwa njia ya ki"electronic" itasaidia kwa kiasi kikubwa kuondoa huu usumbufu, ambapo abilia ataweza kupata tiketi popote pale alipo, kama atakuwa anapata mtandao wa simu husika.

Kupitia njia hii ya ki"electronic" mteja atapiga *150*04# kupata menu ya kukata/kubuku Ticketi na kisha kulipia kwa njia ya M-PESA au mitandao mingine ya Airtel na Zantal ambapo makubaliano na mambo ya kiufundi yapo katika hatua za mwisho. Mteja atatumiwa SMS baada ya malipo kuthibitishiwa na hapo hapo Mteja atapata number ya Ticket, number ya kiti (Seat number) Namba ya basi atakalosaifiri nalo, tarehe, muda wa kuondoka na kituo anachoteremkia .

Abiria anaweza kutumia hii meseji kama ticket kwa ajiri ya kupanda Basi(Bus). Kwa abiria wanaohitaji kupata ticket za karatasi (Phyisical ticket) watatakiwa kufika kwenye ofisi zetu Ubungo stendi ya mabasi au Ofisi za basi husika, pia tupo kwenye hatua za mwisho kukamilisha upatikanaji wa tiketi kupitia mashine za Selcom Paypoint kama wanavolipia bidhaa nyinginezo za DSTV, LUKU DAWASCO.

Mpaka sasa Makampuni ya mabasi yapatayo 10 kama ; (Metro, Prince, Muro, Saibaba, Ngorika, ABS, Zuberi, NBS na Spider) tayari yamejiunga na huduma hii.Mabasi Haya yanafanya safari zake katika mikoa ya Mwanza,Arusha,Tabora, Mtwara.Singida,Dodoma na nchi za Jirani.

Michakato inaendelea ili kuipanua huduma hii kufikia wateja wa mitandao yote ya Simu,Makampuni yote ya mabasi, Mikoa yote nchini na vyombo vingine vya usafiri kama Treni na meli ndani ya muda mfupi.

Huduma kama hii ilishajaribiwa na kufanikiwa katika nchi nyingine za kiafrika kama Nigeria na Kenya. Kwa kuwa watanzania wengi wanajua kutumia vizuri simu za mkononi, nimatarajio yetu kuwa huduma hii itawanufaisha na itaokoa muda wenu ambao huwa mnapoteza kwa ajili ya kwenda kukata tiketi.

Kampuni inawaomba wadau wote hususani serikari na vyombo vya Habari kuhamasisha umma kuhusu matumizi ya huduma hii kwani faida zake ni pamoja na kuokoa muda, nguvu, fedha na rasilimali nyingine.

Mobile Ticketing Limited ni Kampuni mpya iliyoanzishwa Mwezi May 2011, Inamilikiwa asilimia 100% na wajasiliamali wakitanzania ..Imesajiriwa na BRELA, TCRA na TRA.

Ina ofisi Ubungo Stendi ya Mkoa na Makao makuu yake yapo Makuburi Jirani na EPZA.

Michuzi Blog

Tanzanian blog operating since 2005, covering International news and Local News, including Politics, Fashion, Social Scenes, Interviews, Movies, Events, personalities and anything positive happening worldwide. Written in Swahili and English targeting both Swahili and English readers.

Toa Maoni Yako:

Kuna Maoni 7 mpaka sasa

  1. AnonymousMay 21, 2012

    Haya ni mapinduzi makubwa sana!! na hongereni kwa wazo hili, mnastahili pongezi sana. Kuna umuhimu mkaweka point kadhaa zaidi ya Ubungo ili wanaotaka ticket za makaratasi wapate mapema badala ya kwenda hadi Ubungo tena!!

    Wazo zuri sana, wapiga debe sasa hapo ni kifo cha mende,nasikitika sana!

    ReplyDelete
  2. AnonymousMay 21, 2012

    kwa mwandishi wa habari hii....Wasafiri wa mabasi wanaitwa ABIRIA sio abilia..

    ReplyDelete
  3. AnonymousMay 21, 2012

    hongereni sana ni mwanzo mzuri pia itasaidia kundoa usumbufu unaojitokeza kwa abiria hasa kipindi cha sikukuu

    ReplyDelete
  4. AnonymousMay 21, 2012

    Makao makuu ya hii kampuni yapo makaburini!!!

    ReplyDelete
  5. Hongereni sana hii inahitajika tumechoka kelele zile na kuibiana

    ReplyDelete
  6. AnonymousMay 21, 2012

    Vishoka, madalali na wapiga debe poleni sana. Bado pale kwenye boti za zanzibar na vituo vya daladala siku zenu zinahesabika.

    ReplyDelete
  7. AnonymousMay 21, 2012

    wewe hapo juu ni makuburi na si makaburi,soma vizuri

    ReplyDelete

Hii ni Blog ya Watanzania popote walipo duniani kwa ajili ya kuhabarisha, kutoa/kupokea taarifa na kuelimisha mambo yote yaliyo chanya kwa Taifa letu. Tafadhali sana unapotoa maoni usichafue hali ya hewa wala usijeruhi hisia za mtu/watu. Kuwa mstaarabu...