Na Mwandishi wetu
MKUU wa mkoa wa Arusha Magesa Mulongo ametoa wito kwa wafanyabiashara wa ndani na wa nje ya nchi kutumia fursa za kibiashara katika mkutano wa mwaka wa benki ya maendeleo ya Afrika utakaoshirikisha marais kutoka maeneo mbali mbali unaotarajiwa kufanyika mei 28 hadi juni 1 mjini hapa.
Mulongo ametoa wito huo wakati alipokuwa akizungumza juu ya maandalizi ya mkutano huo unaotarajiwa kujumuisha watu 2000 hadi 3000 kutoka nchi mbalimbali duniani.
“ wafanyabiashara hawana budi kubuni biashara ambazo zitaingiza kipato katika mkutano wa benki ya maendeleo ya Afrika (AfDB)o kwani mkutano huu ni mkubwa sana na utaweza kuwaingizia wananchi vipato vyao “alisema Mulongo.
Aidha alisema ni vema wamiliki wa hoteli pamoja na watoa huduma za utalii kutoa lugha nzuri kwa wageni hao ambao wanakuja kwaajili ya mkutano huo na wengine kutembelea mbuga za wanyama zilizopo Tanzania.
Vile vile aliwataka wamiliki wa hoteli kuwaatadharisha wafanyakazi wao kutoa lugha nzuri kwa wageni mbalimbali wanaokuja jijini Arusha kwaajili ya utalii na shughuli mbalimbali pia wale wanaotoa huduma za utalii nao watoe huduma nzuri ili waweze kupata watalii wengi nchini.
Mkurugenzi wa Kituo cha Mikutano cha AICC, Elishilia Kaaya amesema kituo hicho tayari kimejipangavizuri kupokea ugeni huo ambao jumla ya magavana 80 na marais 10 watashiriki mkutano huo, hivyo kuwasihi wananchi kujitokeza kwa wingi katika mkuatano.
Toa Maoni Yako:
0 comments so far,add yours
Hii ni Blog ya Watanzania popote walipo duniani kwa ajili ya kuhabarisha, kutoa/kupokea taarifa na kuelimisha mambo yote yaliyo chanya kwa Taifa letu. Tafadhali sana unapotoa maoni usichafue hali ya hewa wala usijeruhi hisia za mtu/watu. Kuwa mstaarabu...