Waziri wa Ujenzi Dkt. John Magufuli akitoa ufafanuzi wa mradi wa mabasi yaendao mwendo kasi (DART) mei 2,2012 jijini Dar es Salaam kwa waandishi wa habari hawapo pichani alipotembelea na kuangalia maendeleo ya  mradi huo ambao utagharimu shilingi bilioni 288 za kitanzania ambazo zitajumlisha kwa pamoja na ujenzi wa vituo vya mabasi.

Mkurugenzi Mtendaji wa TANROADS Mhandisi Patrick Mfugale akitoa maelezo ya mradi wa DART  Mei 2,2012  jijini Dar es Dar es salam kwa Waziri wa Uchukuzi  Dkt. John Magufuli (wapili kushoto)  pamoja na  Kaimu Mkuu wa Mkoa wa DSM Mwantumu Mahiza, (kushoto). Mradi huo ukikamilika utasaidia kupunguza msongamano wa  magari na kurahisisha usafiri kwa wakazi wa jijijni.

Waziri wa Ujenzi Dr, John Magufuli (mwenye koti jeusi) akikagua upanuzi wa barabara ya Mwenge- Tegeta leo jijini Dar es Salaam. (mwanamke ni )  Kaimu Mkuu wa Mkoa  wa DSM Mwantumu Mahiza,na Katibu Mkuu wa Wizara ya Ujenzi Balozi Hebert Mrango (mwenyetai)


Baadhi ya sehemu ya ujenzi wa daraja huko mbezi- mwenge- Tegeta.Picha na Mwanakombo Jumaa- MAELEZO
---
NA  MAGRETH KINABO – MAELEZO

 WAZIRI wa  Ujenzi , Dk. John Magufuli amemtaka mkandarasi wa ujenzi  wa Barabara ya  Mabasi yaendayo kasi(DART) yenye urefu wa kilomita 21 na vituo vya mabasi 29 kutoka Kimara hadi Kivukoni iliyoko Jijini Dares Salaam kufanya kazi usiku na mchana ili kuhakikisha

Kauli hiyo imetolewa  na Waziri Magufuli leo wakati alipotembelea miradi hiyo miwili  ili  kungalia shughuli za ujenzi ambapo alifurahishwa na kazi hizo huku akiwataka wamalize kwa muda unaotakiwa.
 
“Mkandarasi unatakiwa kufanya kazi usiku na mchana ili kazi ikamilike kabla ya wakati kampuni yenu ni kubwa kama kuna matatizo yoyote mtuambie sisi serikali ili tuweze kuyashughulikia,” alisema Waziri Magufuli.Waziri Magufuli pia ametoa muda wa siku saba kwa Shirika la Ugavi wa Umeme Tanzania(TANESCO) na  Mamlaka ya  (DAWASA) kuondoa miundombinu yao haraka ili kuepusha ucheleweshaji wa mradi  wa DART.
 
Waziri wa Magufuli alitembelea ujenzi huo katika maeneo ya Jangwani na Ubungo, ambapo alisema itagaharimu sh. bilioni 240 na ikijumwuishwa na ujenzi  mwingine wa vituo utagharimu jumla ya bilioni 288 ambazo zimetolewa na Serikali na Benki ya Dunia.
Awali Meneja wa mradi , Frank  Rohde kutoka  kampuni hiyo ,  alisema changamoto inayoukumba mradi huo ni ucheleweshaji wa vifaa vya ujenzi huo kutoka bandarini ambapo vimekaa kwa muda wa siku saba.
 
Akizungumzia kuhusu  tatizo hilo Waziri Magufuli alisema atazungumza na Wizara ya Fedha na Mamlaka ya Mapato(TRA) ili vifaa hivyo vitolewe haraka.
 
Aidha Waziri Magufuli amemtaka Mkandarasi na Mshauri wa upanuzi wa barabara ya Mwenge hadi Tegeta kutoka kampuni ya Konoike  ya  Japan   kuhakikisha wanamaliza ujenzi wa barabara hiyo yenye urefu wa kilomita 12 inayogharimu sh. bilioni 88 kwa muda unaotakiwa na kuacha kusingizio cha mvua kama wanavyodai kuwa umechelewa kwa asilimia saba.

“Mvua zilinyesha siku tatu haiwezi kuwa sababu kuna  nchi mvua inayesha muda mrefu kuliko Tanzania na ujenzi wa barabara unaendelea. Sijaridhika na hiyo sababu ninyi nchi za nje  mnaweza kujenga hata mvua ikiwa inayesha. Ni lazima wafidie muda … kuongeza kazi ya ujenzi hakutakuwa na ongezeko la muda wala mtaji,” alisisitiza.
 
Wakati huohuo  Waziri Magufuli alitumia nafasi kuwataka wakazi wa Jiji hilo waliojenga katika maeneo ya hifadhi za barabara hizo kuondoka wenyewe kwa kuwa sharia ni msumeno.“ Tukikuta mradi unakwamishwa sisi tutabomoa.

Akizungumzia kuhusu mradi DART , Afisa Mtendaji wa  DART Cosmas Takule alisema utatengeneza ajira 80,000 na kusaidia abiria 406,000. Mradi huo utakamilika katika kipindi cha miezi 36.Kwa upande wake Kaimu Mkuu wa Mkoa wa Dares Salaam , Mwamtumu Mahiza alitka ajira hizo ziwe kwa vijana wa jiji hilo.

Michuzi Blog

Tanzanian blog operating since 2005, covering International news and Local News, including Politics, Fashion, Social Scenes, Interviews, Movies, Events, personalities and anything positive happening worldwide. Written in Swahili and English targeting both Swahili and English readers.

Toa Maoni Yako:

Kuna Maoni 10 mpaka sasa

  1. AnonymousMay 03, 2012

    Huyu mzee anafaa sana kuwa waziri mkuu, kwa kweli JK ampe hiyo kazi, Nchi itanyoooka..

    ReplyDelete
  2. AnonymousMay 03, 2012

    jamaa anakubalika kua rais sema wana mbania mafisadi kwani wanajua atawatoa nishai

    ReplyDelete
  3. AnonymousMay 03, 2012

    safety helmet must be worn all the time.

    ReplyDelete
  4. Kaka,

    Hao waheshimiwa mbona wanaogopa kuvaa hayo maHELIMENT? Kuna nini ?

    ReplyDelete
  5. AnonymousMay 03, 2012

    Jamani eeee, mpo, kuna msukuma mmoja ni mhasibu wa Tannesco yuko makao makuu Ubungo, huyu bwana ana nuka harufu ya ufisadi,nafikiri ,mpaka hapo atakapo kamatwa , atakutwa tayari kisha fungua benki yake binafsi, kama mpaka tumsubili waziri huyu huyu tu mmoja kuinyoosha nchi,basi naye atachoka tu. mimi nashauri Magufuri ,baada ya kazi za barabara ,ahamie wizara ya madini,wizara ambayo Tannesco iko chini yake,ili akapambane ana kwa ana na huyu mhasibu, ni mwizi na ana nuka mavi ya ufisadi.

    ReplyDelete
  6. AnonymousMay 03, 2012

    Mimi napendekeza ujenzi huu uendane na vivuko vya chini au juu kwa ajili ya kuokoa maisha ya watu.Wazee na watoto wangongwa sana nchini kwetu jamani!!!!!

    Hongera kwa kazi nzuri serikali yetu,hasa kwa wazo la mabasi yaendayo kasi,kweli Dar na miji mingine mikubwa itapendeza na Tanzania watapapenda wengi.

    Ushauri ni kwamba tusiishie hapo iwe ni jambo au kazi endelevu kwa kila sehemu.

    ReplyDelete
  7. AnonymousMay 03, 2012

    ni kweli anafaa kuwa PM, ila kwa nchi yetu hii atajiwa na mijitu ya ajabu ajabu halafu itambadilisha. Lakini hapo alipo panamfaa tena sanaa. Hongera sana Dr. John Pombe Magufuli

    ReplyDelete
  8. AnonymousMay 03, 2012

    Watanzania huwa hawapendi wachapa kazi...huona noma saaana

    ReplyDelete
  9. AnonymousMay 03, 2012

    RAISI MTARAJIWA 2015:

    Tusihangaike bure watu wakakanyagana na wakatoana damu,

    MNyonge mnyongeni na haki yake mpeni.

    Kwa anavyojituma kwa nini asipate?
    Yanini tuangukie kwa GALACHA?

    Ni zamu yake Chapa ya Ng'ombe Mwana Maduhu!

    Ili nchi ipige hatua kwa maendeleo na ili CCM isianguke na kupoteza Utawala,

    Tunapendekeza Raisi Mtarajiwa awe Mhe.John P.Magufuli !

    ReplyDelete
  10. AnonymousMay 03, 2012

    CCM Tusipompa Magufuli, pana wasiwasi Chadema watatusumbua sana 2015!

    Kwa kuwa hawa CHDM hawana sifa za kuichukua nchi inabidi tujipange kwa maamuzi mazito na kwa hili tuache Uswahiba!

    ReplyDelete

Hii ni Blog ya Watanzania popote walipo duniani kwa ajili ya kuhabarisha, kutoa/kupokea taarifa na kuelimisha mambo yote yaliyo chanya kwa Taifa letu. Tafadhali sana unapotoa maoni usichafue hali ya hewa wala usijeruhi hisia za mtu/watu. Kuwa mstaarabu...