Waziri wa Ujenzi Dkt. John Magufuli akitoa ufafanuzi wa mradi wa mabasi yaendao mwendo kasi (DART) mei 2,2012 jijini Dar es Salaam kwa waandishi wa habari hawapo pichani alipotembelea na kuangalia maendeleo ya mradi huo ambao utagharimu shilingi bilioni 288 za kitanzania ambazo zitajumlisha kwa pamoja na ujenzi wa vituo vya mabasi.

Mkurugenzi Mtendaji wa TANROADS Mhandisi Patrick Mfugale akitoa maelezo ya mradi wa DART Mei 2,2012 jijini Dar es Dar es salam kwa Waziri wa Uchukuzi Dkt. John Magufuli (wapili kushoto) pamoja na Kaimu Mkuu wa Mkoa wa DSM Mwantumu Mahiza, (kushoto). Mradi huo ukikamilika utasaidia kupunguza msongamano wa magari na kurahisisha usafiri kwa wakazi wa jijijni.
Waziri wa Ujenzi Dr, John Magufuli (mwenye koti jeusi) akikagua upanuzi wa barabara ya Mwenge- Tegeta leo jijini Dar es Salaam. (mwanamke ni ) Kaimu Mkuu wa Mkoa wa DSM Mwantumu Mahiza,na Katibu Mkuu wa Wizara ya Ujenzi Balozi Hebert Mrango (mwenyetai)
Baadhi ya sehemu ya ujenzi wa daraja huko mbezi- mwenge- Tegeta.Picha na Mwanakombo Jumaa- MAELEZO
---
NA MAGRETH KINABO – MAELEZO
WAZIRI wa Ujenzi , Dk. John Magufuli amemtaka mkandarasi wa ujenzi wa Barabara ya Mabasi yaendayo kasi(DART) yenye urefu wa kilomita 21 na vituo vya mabasi 29 kutoka Kimara hadi Kivukoni iliyoko Jijini Dares Salaam kufanya kazi usiku na mchana ili kuhakikisha
Kauli hiyo imetolewa na Waziri Magufuli leo wakati alipotembelea miradi hiyo miwili ili kungalia shughuli za ujenzi ambapo alifurahishwa na kazi hizo huku akiwataka wamalize kwa muda unaotakiwa.
“Mkandarasi unatakiwa kufanya kazi usiku na mchana ili kazi ikamilike kabla ya wakati kampuni yenu ni kubwa kama kuna matatizo yoyote mtuambie sisi serikali ili tuweze kuyashughulikia,” alisema Waziri Magufuli.Waziri Magufuli pia ametoa muda wa siku saba kwa Shirika la Ugavi wa Umeme Tanzania(TANESCO) na Mamlaka ya (DAWASA) kuondoa miundombinu yao haraka ili kuepusha ucheleweshaji wa mradi wa DART.
Waziri wa Magufuli alitembelea ujenzi huo katika maeneo ya Jangwani na Ubungo, ambapo alisema itagaharimu sh. bilioni 240 na ikijumwuishwa na ujenzi mwingine wa vituo utagharimu jumla ya bilioni 288 ambazo zimetolewa na Serikali na Benki ya Dunia.
Awali Meneja wa mradi , Frank Rohde kutoka kampuni hiyo , alisema changamoto inayoukumba mradi huo ni ucheleweshaji wa vifaa vya ujenzi huo kutoka bandarini ambapo vimekaa kwa muda wa siku saba.
Akizungumzia kuhusu tatizo hilo Waziri Magufuli alisema atazungumza na Wizara ya Fedha na Mamlaka ya Mapato(TRA) ili vifaa hivyo vitolewe haraka.
Aidha Waziri Magufuli amemtaka Mkandarasi na Mshauri wa upanuzi wa barabara ya Mwenge hadi Tegeta kutoka kampuni ya Konoike ya Japan kuhakikisha wanamaliza ujenzi wa barabara hiyo yenye urefu wa kilomita 12 inayogharimu sh. bilioni 88 kwa muda unaotakiwa na kuacha kusingizio cha mvua kama wanavyodai kuwa umechelewa kwa asilimia saba.
“Mvua zilinyesha siku tatu haiwezi kuwa sababu kuna nchi mvua inayesha muda mrefu kuliko Tanzania na ujenzi wa barabara unaendelea. Sijaridhika na hiyo sababu ninyi nchi za nje mnaweza kujenga hata mvua ikiwa inayesha. Ni lazima wafidie muda … kuongeza kazi ya ujenzi hakutakuwa na ongezeko la muda wala mtaji,” alisisitiza.
Wakati huohuo Waziri Magufuli alitumia nafasi kuwataka wakazi wa Jiji hilo waliojenga katika maeneo ya hifadhi za barabara hizo kuondoka wenyewe kwa kuwa sharia ni msumeno.“ Tukikuta mradi unakwamishwa sisi tutabomoa.
Akizungumzia kuhusu mradi DART , Afisa Mtendaji wa DART Cosmas Takule alisema utatengeneza ajira 80,000 na kusaidia abiria 406,000. Mradi huo utakamilika katika kipindi cha miezi 36.Kwa upande wake Kaimu Mkuu wa Mkoa wa Dares Salaam , Mwamtumu Mahiza alitka ajira hizo ziwe kwa vijana wa jiji hilo.
Huyu mzee anafaa sana kuwa waziri mkuu, kwa kweli JK ampe hiyo kazi, Nchi itanyoooka..
ReplyDeletejamaa anakubalika kua rais sema wana mbania mafisadi kwani wanajua atawatoa nishai
ReplyDeletesafety helmet must be worn all the time.
ReplyDeleteKaka,
ReplyDeleteHao waheshimiwa mbona wanaogopa kuvaa hayo maHELIMENT? Kuna nini ?
Jamani eeee, mpo, kuna msukuma mmoja ni mhasibu wa Tannesco yuko makao makuu Ubungo, huyu bwana ana nuka harufu ya ufisadi,nafikiri ,mpaka hapo atakapo kamatwa , atakutwa tayari kisha fungua benki yake binafsi, kama mpaka tumsubili waziri huyu huyu tu mmoja kuinyoosha nchi,basi naye atachoka tu. mimi nashauri Magufuri ,baada ya kazi za barabara ,ahamie wizara ya madini,wizara ambayo Tannesco iko chini yake,ili akapambane ana kwa ana na huyu mhasibu, ni mwizi na ana nuka mavi ya ufisadi.
ReplyDeleteMimi napendekeza ujenzi huu uendane na vivuko vya chini au juu kwa ajili ya kuokoa maisha ya watu.Wazee na watoto wangongwa sana nchini kwetu jamani!!!!!
ReplyDeleteHongera kwa kazi nzuri serikali yetu,hasa kwa wazo la mabasi yaendayo kasi,kweli Dar na miji mingine mikubwa itapendeza na Tanzania watapapenda wengi.
Ushauri ni kwamba tusiishie hapo iwe ni jambo au kazi endelevu kwa kila sehemu.
ni kweli anafaa kuwa PM, ila kwa nchi yetu hii atajiwa na mijitu ya ajabu ajabu halafu itambadilisha. Lakini hapo alipo panamfaa tena sanaa. Hongera sana Dr. John Pombe Magufuli
ReplyDeleteWatanzania huwa hawapendi wachapa kazi...huona noma saaana
ReplyDeleteRAISI MTARAJIWA 2015:
ReplyDeleteTusihangaike bure watu wakakanyagana na wakatoana damu,
MNyonge mnyongeni na haki yake mpeni.
Kwa anavyojituma kwa nini asipate?
Yanini tuangukie kwa GALACHA?
Ni zamu yake Chapa ya Ng'ombe Mwana Maduhu!
Ili nchi ipige hatua kwa maendeleo na ili CCM isianguke na kupoteza Utawala,
Tunapendekeza Raisi Mtarajiwa awe Mhe.John P.Magufuli !
CCM Tusipompa Magufuli, pana wasiwasi Chadema watatusumbua sana 2015!
ReplyDeleteKwa kuwa hawa CHDM hawana sifa za kuichukua nchi inabidi tujipange kwa maamuzi mazito na kwa hili tuache Uswahiba!