Leo machana katika kipita shoto cha barabara ya Kilwa road jijini Dar es salaam lori la Mamlaka ya bandari limepata ajali kwa kuingia mtaroni.Kwa bahati nzuri hakuna aliyepoteza maisha wala kujeruhiwa. Chanzo cha habari hakikuweza kujulikana mara moja
Mdau wa Globu ya Jamii.

Michuzi Blog

Tanzanian blog operating since 2005, covering International news and Local News, including Politics, Fashion, Social Scenes, Interviews, Movies, Events, personalities and anything positive happening worldwide. Written in Swahili and English targeting both Swahili and English readers.

Toa Maoni Yako:

Kuna Maoni 4 mpaka sasa

  1. AnonymousJune 15, 2012

    Barabara ya Kilwa Road!!!!! upo sawasawa kweli??

    ReplyDelete
  2. AnonymousJune 15, 2012

    Hivi jamani hii mitaro ni lazima ikae wazi? Ukiiangalia ni mikubwa sana na imesababisha ajali nyingi sana hadi sasa. Gari ndogo ikidondoka humo inaingia yote. Kwa nini isifunikwe ili hata dereva akishindwa kulidhibiti gari lake basi litoke tu nje ya barabara badala ya kutumbukia katika jimtaro namna hii?

    ReplyDelete
  3. AnonymousJune 15, 2012

    Ukiachia uzembe wa baadhi ya madereva na ubovu wa magari, lakini hata ujenzi mbaya wa miundo mbinu ya barabara huchangia ajali na kusababisha misiba ama vilema kwa watumiaji wa barabara.

    Hii mitaro isiozibwa ama kuwekewa kingo ni faida kwa nani kama siajali kama hizi.

    kwako muandishi; Chanzo cha habari ama ajali hakikuweza kujulikana mara moja.

    ReplyDelete
  4. AnonymousJune 15, 2012

    Du mambo ya kazini jamaa Dereva amemshikia mtu 'babu' anayekaribia kustaafu lakini aliyekwenda kidogo Likizo!

    Sasa Dereva Kijana mgeni ile anapewa Lori anafika Mzunguko,,,ahhh jamaa hakuona kona wala mzunguko wowote, ila kati kati ya barabara anaona ng'ombe anakuja anakimbia mbele yake!

    Ohhh jamaa asiliingize Lori mtaroni?

    ReplyDelete

Hii ni Blog ya Watanzania popote walipo duniani kwa ajili ya kuhabarisha, kutoa/kupokea taarifa na kuelimisha mambo yote yaliyo chanya kwa Taifa letu. Tafadhali sana unapotoa maoni usichafue hali ya hewa wala usijeruhi hisia za mtu/watu. Kuwa mstaarabu...