Katibu Mkuu wa Umoja wa Mataifa, Ban Ki Moon akiwa na Dkt Asha-Rose Migiro katika hafla ya kumuaga rasmi iliyofanyika leo katika Makao Makuu ya Umoja wa Mataifa baada ya kumaliza muda wake kama Naibu Katibu Mkuu wa Umoja wa Mataifa
Dkt Asha-Rose Migiro akiongea katika hafla hiyo ya kumuaga rasmi
Katibu Mkuu wa Umoja wa Mataifa, Ban Ki Moon akiongea katika hafla hiyo
Dkt Asha-Rose Migiro baada ya kupokea zawadi ya maua katika hafla hiyo ya kumuaga rasmi
·
*Yamshukuru kwa mchango wake katika kutetea afya ya wanyonge
· *Yasema alikuwa na mchago mkubwa sana katika vita dhidi ya malaria, ukimwi, kifua kikuu na afya ya wanawake na watoto
· *Ban ki Moon asema alikuwa si mtu wa makuu na mtu wa watu
Na Mwandishi Maalum
Mashirika ya Umoja wa Mataifa yanayohusika na masuala ya Idadi ya Watu ( UNFPA),Ugonjwa wa Ukimwi ( UNAIDS) na Mpango wa kupambana na Ugonjwa wa Malaria ( RBM) jana jumanne yaliandaa tafrija kamambe ya kumshukuru na kumuaga Naibu Katibu Mkuu wa Umoja wa Mataifa, Dkt. Asha-Rose Migiro.
Tafrija hiyo ya aina yake na ambayo mgeni rasmi alikuwa Katibu Mkuu wa Umoja wa Mataifa, Ban Ki Moon, akiambatana na mke wake na kuhudhuriwa pia na wadau mbalimbali akiwamo Mtendaji Mkuu wa UNDP Bi Helen Clark, mabalozi wanaoziwakilisha nchi zao katika UM, sekta binafsi na taasisi za kiraia imefanyika hapa makao Makuu ya Umoja wa Mataifa.
Akizungumza wakati wa tafrija hiyo, Katibu Mkuu Ban ki Moom ameleezea baadhi ya sababu zilizomsukuma kumteua Dkt. Asha- Rose Migiro kuwa msaidizi wake wa karibu.
“ Nilianza kumfahamu Asha- Rose Migiro wakati huo sote tukiwa mawaziri wa mambo ya nje katika nchi zote. Uwezo wake na uelewa wake wa mambo ulinivutia sana, lakini nilivutiwa zaidi pale nilipofahamu kwamba aliwahi kuwa waziri anayehusika na masuala ya wanawake na watoto. Nikajiridhisha kwamba huyu ndiye alikuwa ananifaa kuwa msaidizi wangu wa karibu” akasema Ban Ki Moon na kuufanya umati ulihohudhiria tafrija hiyo kushangilia kwa nguvu.
Kama hiyo haitoshi, Ban Ki Moon amemuelezea Dkt. Asha- Rose Migiro kama msaidizi wake wa karibu ambaye licha ya kufanya kazi kwa uadilifu mkubwa lakini ni mtu ambaye alikuwa hana makuu na wala hata siku moja hakujikweza.
“ Katika kipindi chote ambacho Migiro amekuwa msaidi wangu wa karibu, amenisaidia katika mambo mengi, ni mtu muadilifu sana, ni mtu aliyekaribu sana na watu, aliyeamsha matumaini na kuwapa tabasamu watu waliokuwa katika mazingira magumu. Daima amekuwa mstari wa mbele kunisaidia na hakuna hata siku moja alipojikwenza. Na kwa sababu hii anastahili tafrija hii” akasisitiza Ban Ki Moon.
Aidha Ban Ki Moon akamuelezea Asha- Rose Migiro kama kiongozi ambaye daima alitoa kipaumbele cha aina yake katika masuala ya afya ya jamii eneo alilotumia uwezo wake wote, maarifa yake yote kama naibu katibu mkuu kupigania afya ya wanawake na watoto na watu wote walio katika mazingira magumu
Kwa upande wao waandaaji wa tafria hiyo na wakizungumza kwa nyakati tofauti wamemuelezea Naibu Katibu Mkuu, kama kiongozi ambaye mchango wake umesaidia sana katika kuihamasisha jumuiya kimataifa kuweka mkazo wa aina yake katika kushughulika afya ya jamii.
Bw. Michel Sidibe, Mkurugenzi mtendaji wa UNAIDS yeyé alimuelezea Asha- Rose Migiro kama dada yake ambaye sifa zake zinaazia mbali.
“ Asha- Rose Migiro ni dada yangu, ni dada ambaye anasifa za kipekee, ni mwanamke wa kwanza aliyefaulu kwa daraja la kwanza katika sheria kutoka chuo kikuu cha dar es Salaam, ni mwanamke wa kwanza kuwa waziri wa mambo ya nje nchini Tanzania, na ni mwanamke wa kwanza kutoka afrika kuwa naibu Katibu Mkuu wa Umoja wa Mataifa” akasema Bw. Sidibe kauli iliyoamsha tena makofi kutoka kwa wageni waalikwa.
Hakuishia hapo, Michel Sidibe akamuelezea Migiro kama kiongozi aliyefanya kazi kwa karibu na Shirika lake katika kuhakikisha kwamba maambukizi ya virusi vya ukimwi yalikuwa yakipungua ikiwa ni pamoja na kupatika kwa tiba ya uhakika kwa waathirika.
“ Tunakila sababu leo hii kumshukuru kwa namna alivyoshirikiana nasi, na ingawa unaondoka lakini tambua kwamba mchango wake utaendelea kukumbukwa na kuenziwa” akasisitiza Bw. Michel Sidibe.
Naye Mkurugenzi Mtendaji wa Shirika la Umoja wa Maifa la Idadi ya Watu, Dr. Babatunde Osotimehin amesema juhudi kubwa zilizoonyeshwa na Naibu Katibu Mkuu katika kushughulikia masuala ya afya ya jamii, kumefanikisha kupunguza kwa kiasi kikubwa idadi ya vifo vya wanawake vitokanavyo na uzazi hali kadhalika vifo vya watoto wachanga chini ya miaka mitano.
“Katika kipindi cha uongozi wako, umefanikisha sana katika kuhamasisha jumuia ya kimataifa kuongeza misaada yao na kutoa kupaumbele katika afya ya mama na mtoto, tunakushukuru sana kwa hili, na Mungu aendelee kukubariki” akasema Dr. Babatunde Osotimehin.
Kwa upande wake, Bw. Herve Verhoosel, Mwakilishi wa Mapango wa kupunguza Malaria, yeyé alimuelezea Dkt. Asha-Rose Migiro kwamba chini ya uongozi wa Ban Ki Moon, ameweza kujenga misingi bora ya ushirikiano na muamko miongoni mwa wadau mbalimbali katika kuhakikisha kwamba kunakuwapo na uhusiano kati ya sekta za umma za zile za binafasi katika kutimiza malengo ya afya ya jamii ikiwa ni pamoja na kasi ya kupunguza malaria
Akiwashukuru waandaji wa tafrija hiyo, Naibu Katibu Mkuu amemshukuru Katibu Mkuu Ban Ki Moon kwa kumuamini kuwa msaidizi wake wa karibu katika kipindi cha miaka mitano na nusu.
Akasema ingawa yeyé amejituma na kutekeleza majukumu yake kwa ukamilifu, lakini amefanya hivyo kwa kuwa Ban Ki Moon alimuamini kwamba anaweza. Na kwamba daima ataendelea kuienzi heshima hiyo.
Akatumia fursa hiyo kumueelezea Ban Ki Moon kama kiongozi ambaye amekuwa mstari wa mbele kuhakikisha kwamba kila mtoto angalau alikuwa analala kwenye chandarua, akina mama wajawazito walikuwa hawapotezi maisha kutoka na uzazi.
Aidha Migiro amewashukuru kwa moyo wa dhati wasaidizi wake wa karibu aliofanya nao kazi akiwa naibu katibu mkuu na kwamba bila wao asingefika hapo alipo, akawashukuri pia wadau mbalimbali wakiwamo mabalozi kwa ushirikiano wa hali na mali waliompatiwa muda wote wa miaka mitano na nusu


karibu nyumbani kipenzi chetu, umeiwakilisha Tanzania vyema,pamoja na kuitangaza Tanzania dunia nzima Mungu akubariki na akupe afya njema daima.
ReplyDeleteWell come Home our sisy, for all the best you have done you deserve congratulation, you do the best lol...
ReplyDeletewell done Asha Rose Migiro, nafuata nyayo zako..
ReplyDeleteAngalieni namna kuagwa UN kulivyo simple, hakuna stage lilipambwa maua,viti ni vya kawaida hamna pedera, wala matambara hakuna maua ya gharama, na Asha Rose hakupewa hata kitabu, kapewa mauwa tu ambayo bei ni $30. Hebu tusome mfano huo, na nguo aliyovaa ya kawaida tu, bazee la bei kidogo. Hakuna kikundi cha ngoma (Huku vikundi vinacost 250,000 na 10% juu). Yaani ndio maana bajeti haitoshi. Petty cash ya boss ya kunulia sambusa na cake, apple basi secretary na messenger ndio hiyo hiyo. Na hamtaki kuacha.
ReplyDeleteWell done Dr Asha Rose Migiro, unakaribishwa home kishujaa na kama Mh. Dr JK akikupa post msaidie mama kumaliza muda wake salama. All z best
ReplyDeleteanony hapo juu umenigusa! mambo huko majuu simpo simpo tu! a biggup mama!
ReplyDeleteMawaziri wa CCM Matumbo moto...Mama Migiro lazima apewe nafasi na JK. Karibu Mama...Unayo kazi nyingine ya kupambana na mafisadi.
ReplyDeleteMa Migiro Welcome home, hongera toto la weru weru, umetusafisha nyuso. all the best, Mchango unasubiriwa hapa nyumbani kwa hamu kubwa. We are very proud of you.
ReplyDeleteHAYA HAYA JUNGU LIMEIVA, BAN KI MOON KAKUMWAGIA SIFA TELE ZA UADILIFU, KARIBU KWA MAFISADI, TUNAKUOMBEA MUNGU USIWE MMOJA KATIKA HAO, NAWAONAJE WANAVINYANGANYIRO VYA URAIS 2015 MATUMBO MOTO, MAMA NCHI IMEOZA USIKUBALI HATA KIDOGO KUCHUKUA WATAKUCHAFUACHAFUA TU, HAPA UFISADI NA UVIVU NDIO UNANAFASI UKIWA MCHAPA KAZI HUNA CV. KARIBU TENA.
ReplyDeleteMAMA MAMA MAMA HUYOOOOO KARIBU MHESHIMIWA MIGIRO, KARIBU DADA, HAPA NDIO KWENU JAPO SIFA NI UFISADI, KARIBU MAMA UTOE MCHANGO WAKO PENGINE UTAOKOA JAHAZI, HONGERA SANA KWA KAZI NZURI ULIYOFANYA UN, UMETUFUTA TONGO.
ReplyDelete