Kijana mdogo wa miaka 17, Jackson Thobias aliyekuwa akisoma kidato cha nne ESACS Academy, amefariki kwa kugongwa na treni maeneo ya kwao kipawa, aligongwa akiwa anasikiliza music kwa headphones huku akichati katika simu yake wakati akitembea kwenye reli.
Pamoja na mlio mkubwa wa treni, na juhudi za watu kumpigia kelele kuwa kuna treni inakuja nyuma yake, Jackson hakusikia.
Marehemu Jackson ndio aliye shinda kwenye Tokelezeiyer Inter-School concert iliyoandaliwa na group ya Friends 4 Friends tarehe 12 may 2012, pia alishinda dougie competition wakati 5select Event ya EATV ilipotembelea ESACS wiki mbili zilizopita.
Alikuwa ni kijana mwenye kipaji na ndoto nyingi katika umri mdogo wa miaka 17, Mungu aipumzishe roho ya marehemu Jackson Thobias kwa amani.
Amen.


Mungu aipumzishe pema roho ya kijana mdogo Thobias.
ReplyDeleteVile vile vijana tafadhalini chukueni hadhari kwani ajali ya aina hizi huwa zinatokea sana Ulaya, hasa kwenye barabara, lakini hapa kwetu nadhani ndiyo ya kwanza.
Eh Mola ailaze roho yake mahali pema peponi.Mola ametoa na Mola ametwaa, jina lake siku zote lihimidiwe.Poleni sana wafiwa Mola awape nguvu katika kipindi hiki kigumu.
ReplyDeletemdau sweden
Mchango wa wachawi katika jamii za kiafrika ni kuumiza watu kwa wivu tu!
ReplyDeletewewe mdau unaesema ajali kama hizi zinatokea sana ulaya ni ulaya gani uliyokaa? Tutajie. Usichanganye vile vifo vinavyotokea kwa madereva huku ulaya wanaovuka sehemu za treni kwa haraka na hatimae hugonwa.Lakini HAKUNA WATU ULAYA WANAOTEMBEA NJIA YA TRENI WAKAWA WANASIKILIZA MP3 HALAFU WAKAGONGWA !!!!!!
ReplyDeleteKatika tukio hili kinachosikitisha ni kuwa kijana wetu alijisahau kama wanavyojisahau wengi huko bongo.Tujitahidi tukio hili liwe ni la mwisho maana hakuna sababu yoyote ya kimsingi kutembea relini na kusikiliza mp3 bila kujua nini kinachokujiri.
MWENYEZI MUNGU AMLAZE MAHALA PEMA AMEN
Hakika hakuna aijuaye siku yake ya mwisho. Kijana mdogo huyu ametutoka kama mchezo tu. Nimeguswa mno na jambo hili. Mungu mwenye Rehema ailaze Roho ya marehemu mahali pema peponi. Amen. Ichube
ReplyDeleteELIMU YAKE NA VIPAJI VYAKE VILIKUWA BADO HAVIJAMKOMBOA KIFIKRA. AU ALIKUWA NA MATATIZO FULANI YA KIAKILI. MAANA KATIKA HALI YA KAWAIDA HATUTEGEMEI KIJANA WA MJINI, UMRI MIAKA 17, ANASOMA SECONDARI AWE ANATEMBEA KWENYE RELI AKIWA AMEZIBA MASIKIO.
ReplyDeleteINASIKITISHA KUONA WENYE VIPAJI WANAKUFA KTK MAZINGIRA YA KIZEMBE KIASI HIKI. REST IN PEACE.