Rais Jakaya Mrisho Kikwete, aliye katika mapumziko mafupi jijini Arusha, akiwa katika mazoezi yake ya kila asubuhi na jioni ya kutembea kilomita 3 kabla ya kufanya mazoezi ya viungo na kuingia gym, katika kuuweka mwili wake katika hali ya ukakamavu na afya. Wakaazi wengi wa Arusha ambao wamemuona akitembea wamesisimkwa na kufurahishwa sana na hatua hiyo ya kiongozi mkuu wa nchi kuwa mstari wa mbele katika kuonesha kwa vitendo umuhimu wa kujenga afya kwa mazoezi ya kila siku, na kutaka kila mtu, si viongozi tu, kuiga mfano hai huo kwa kuanza kufanya mazoezi kila siku bila kushurutishwa  ili kulinda afya zao.
PICHA NA IKULU
 

Michuzi Blog

Tanzanian blog operating since 2005, covering International news and Local News, including Politics, Fashion, Social Scenes, Interviews, Movies, Events, personalities and anything positive happening worldwide. Written in Swahili and English targeting both Swahili and English readers.

Toa Maoni Yako:

Kuna Maoni 13 mpaka sasa

  1. AnonymousJune 04, 2012

    aaaaaahhhhhhhhhhh

    ReplyDelete
  2. AnonymousJune 04, 2012

    Hii ni safi sana,ni muhimu kwa kiongozi wa nchi kuwa katika hali nzuri ya iafya ili aweze kuudu hali ya kazi yake.

    Keep it up Dkt J. Kikwete.

    Hiyo Dkt. ni kwa vile wau wa michuziblog wanaipenda saana. teh teh.

    ReplyDelete
  3. AnonymousJune 04, 2012

    Naona Jamaa pembeni wako loaded!

    ReplyDelete
  4. AnonymousJune 04, 2012

    mzee shikamoo naomba hiyo traksuit nimeipenda mzee

    ReplyDelete
  5. Tumuunge mkono Rais Jk kwa kufanya mazoezi ni muda mrefu sana sijawahi ona picha ya rais wetu akila tiz kama hivi. Nakumbuka ya Mwisho ilikuwa ya Mzee wetu Mwinyi tena akiwa Iringa nazani ni barabara ya Nduli Hongera rais

    ReplyDelete
  6. AnonymousJune 04, 2012

    Nimefurahi sana kumwona amiri jeshi wetu mkuu na mpendwa akiongoza kwa mfano. Mtu ni afya.

    ReplyDelete
  7. AnonymousJune 04, 2012

    Mazoezi hasa kwetu sisi wafanyakazi tunaoshinda tumekaa maofisini tukiwa tunafanya kazi ni muhimu sana. Kukaa kwa masaa mengi kunapunguza siku za kuishi hapa duniani. Mazoezi yanachangia kwa kiasi kikubwa kuimarisha afya na kujikinga na magonjwa shime tujenge tabia ya kufanya mazoezi kwa manufaa yetu na ya taifa letu.

    ReplyDelete
  8. AnonymousJune 04, 2012

    Mkuu you have made my day!

    ReplyDelete
  9. AnonymousJune 04, 2012

    Hahahaha!KITAMBI NOMA CLUB(ARUSHA)Mpo juu namwona mdau Robert ngoboma kwa pembeni.....good!!!

    ReplyDelete
  10. AnonymousJune 04, 2012

    Big up Raisi. Imebaki kutengeneza miundo mbinu ili asilimia zaidi ya wananchi waanze kula tizi .
    Siyo mpaka kuwe na JKT kama zamani.

    ReplyDelete
  11. AnonymousJune 04, 2012

    Hongerasana Mhe. Rais kwa kuonesha mfano kwa vitendo. washauri maafisa wako serikalini waelewe vitambi nomaa! wengi wanapata vitambi muda mfupi baada ya kupata vyeo...

    Mie binafsi naona NOMAA kubwa kuona wanajeshi, awe askari wa polisi au JW au magereza loh wengi vitambi mbele hata magwanda hayakai vizuri.

    ReplyDelete
  12. AnonymousJune 04, 2012

    Baba Mkuu wa Nchi Rais JK,hongera kwa hili,sasa tunakuomba tabia hii lazima uipereke katika jeshi la Polisi, Baba kule Jeshi la Polisi ni noma sana,kuna maofisa wa vyeo vya juu sana wanavitambi.
    Baba chonde chonde,vibosile wa Polisi wanashindana kwa vitambi aka makaburi ya kuku,tena maofisa hao wamenona mno baba !.katika maofisa wote wa jeshi la polisi wanaofanya vizuri na wako gado ni kina Ras Makunja pekee yao,wao wakati wowote wapo tayari kwa fujo aka muziki

    ReplyDelete
  13. AnonymousJune 05, 2012

    Sawa Kiongozi cha kuongeza ni kuwarudishia Mateja JKT ili nao watoe unga kwenye damu zao na kuwa fit kiafya kama wewe Mhe.Raisi !!!

    ReplyDelete

Hii ni Blog ya Watanzania popote walipo duniani kwa ajili ya kuhabarisha, kutoa/kupokea taarifa na kuelimisha mambo yote yaliyo chanya kwa Taifa letu. Tafadhali sana unapotoa maoni usichafue hali ya hewa wala usijeruhi hisia za mtu/watu. Kuwa mstaarabu...