Na. Luppy Kung’alo, Jeshi la Polisi Dodoma.

Jeshi la Polisi Mkoa Dodoma linamshikilia mtu mmoja aliyefahamika kwa jina la Daniel s/o Lusega miaka (42) kabila mkaguru na mkazi wa Morisheni kata, tarafa na wilaya ya kongwa kwa tuhuma za kumchinja mke wake na kumuua.

Kamanda wa Polisi Mkoa wa Dodoma Kamishna Msaidizi Mwandamizi wa Jeshi la Polisi Bw. ZELOTHE STEPHEN alisema Tukio hilo limetokea tarehe 25/06/2012 muda (08:00hrs) wa saa mbili asubuhi leo, katika eneo la Morisheni Kata, Tarafa na Wilaya ya Kongwa.

“Mtuhumiwa alikwenda kuripoti mwenyewe katika kituo cha Polisi cha Wilaya ya Kongwa kuwa amemchinja na kumuua mke wake kwa sababu hamsikilizi.” alieleza Kamanda Zelothe.

Bw, Zelothe alisema mtuhumiwa huyo wakati anaripoti tukio hilo katika kituo cha Polisi alikuwa na barua mkononi ikieleza madai hayo kwa marehemu mke wake, ikiwa na anuani ikielekeza kwa Afisa Usalama wa wilaya ya Kongwa, lakini barua hiyo ameikabidhi katika kituo cha Polisi.

Kamanda ZELOTHE STEPHEN alimtaja mwanamke huyo aliyeuwawa kuwa ni Telophena w/o Machimo umri miaka (34) kabila Mkaguru, muuza mgahawa na Mkazi wa Morisheni wilayani kongwa.

Kamishna Msaidizi Mwandamizi wa Jeshi la Polisi, Bw. ZELOTHE STEPHEN alisema askari walikwenda kukagua eneo la tukio na kukuta marehemu amechinjwa kwa kukatwa koromeo na akiwa katika dimbwi la damu pamoja na kisu kilichotumika kikiwa kando yake.

Kamanda huyo wa Jeshi la Polisi Mkoa wa Dododma alisema chanzo cha mauaji hayo ni wivu wa mapenzi kwa kuwa mtuhumiwa alikuwa akimtuhumu marehemu kwa kutembea nje ya ndoa pia kwa kutoleta matumizi ili hali merehemu ni muuza mgahawa katika eneo hilo.

Hata hivyo Kamanda Zelothe alisema mtuhumiwa huyo ana historia ya ugonjwa wa akili kwa mujibu wa maelezo ya wanandugu na viongozi wa kijiji wa eneo hilo.

Mtuhumiwa amekamatwa na anashikiliwa katika kituo cha Polisi Wilayani Kongwa na atafikishwa mahakamani kujibu tuhuma zinazo mkabili, alisema Bw. Zelothe.

Michuzi Blog

Tanzanian blog operating since 2005, covering International news and Local News, including Politics, Fashion, Social Scenes, Interviews, Movies, Events, personalities and anything positive happening worldwide. Written in Swahili and English targeting both Swahili and English readers.

Toa Maoni Yako:

Kuna Maoni 5 mpaka sasa

  1. AnonymousJune 25, 2012

    kwa sababu hamna talaka au?

    kutaliki na kuuwa lipi ovu saana?

    tutambue kuwa talaka ipo na hamna haja ya kuuwa mzazi wa wanao.

    ReplyDelete
  2. AnonymousJune 25, 2012

    Mdau wa kwanza unaposema hamna haja ya kuua kwa sababu talaka ipo unakosea, japo naamini hukukusudia. Ni kwamba talaka iwepo au isiwepo, ni marufuku kuua.

    ReplyDelete
  3. AnonymousJune 26, 2012

    Mtuhumiwa ana matatizo ya akili? inakuwaje akumbuke kuandika barua na ajipeleke mwenyewe kituo cha polisi? hiyobarua aliiandika kabla au baada ya mauaji? Jamani tunakwenda wapi?

    ReplyDelete
  4. AnonymousJune 26, 2012

    eti alikuwa haleti matumizi....wanaume wa siku hizi bana...wapi ule mstari mwanaume atakula kwa jasho? fanyeni kazi bana acheni kututegemea, tunazaa kwa uchungu inatoshaaaa. Hata kama tunafanya kazi tutahudumia tukipenda sio lazima.

    ReplyDelete
  5. AnonymousJune 26, 2012

    Dalili za kiyama.

    ReplyDelete

Hii ni Blog ya Watanzania popote walipo duniani kwa ajili ya kuhabarisha, kutoa/kupokea taarifa na kuelimisha mambo yote yaliyo chanya kwa Taifa letu. Tafadhali sana unapotoa maoni usichafue hali ya hewa wala usijeruhi hisia za mtu/watu. Kuwa mstaarabu...